Nimechanganyikiwa mpaka nakitamani kifo nisaidieni nifanyeje mimi

Nimechanganyikiwa mpaka nakitamani kifo nisaidieni nifanyeje mimi

Pole dada, Mungu anakupenda walau umejua kabla hujajifunga kitanzi feki cha ndoa. Jipange uendelee mbele. Sikushauri kujiattach kwa huyo mwingine, utaishia majonzi tu. Mueleze una mimba na ungependa kama mkiwa marafiki tu (wanaume hawapendi hii, ila ni bora kuliko umdanganye). Maisha yataendelea na utabarikiwa hadi ushangae.
 
habari ndo hiyo,na sio utani its a fact,inshallah one day we will get to know each other,you will see my watoto's na ninawalea mwenyewe.
Najua aina yako mpo sana tu. Hata hivyo hongera kwa kutimiza majukumu. . .
 
Futa mawasiliano na huyo shetani wala usitoe mimba zaa mtoto wako usimshirikishe kwa kitu chochote, wanaume wamaana wamejaa na hawakatai watoto usimuue mwanao kisa huyo pepo endelea na maisha kama kawaida wewe sio wa kwanza kufanyiwa hivyo.
Latifa ,achana na ushauri huu wa Loly,jamaa yako mpe fursa ya kulea mimba hata kama una hasira naye vipi,believe me,i am talking from experience ,omba Mungu uzae salama,we na ba mtoto mtaishia kuwa marafiki hata kama sio urafiki wa malavidavi.
 
.........Pole sana, ilikuwaje ulijiachia hadi ukapata mimba? I know bahati mbaya, ila hakuna mimba inayoingia kwa bahati mbaya.......hivyo ni mpango wa Mungu mtoto kuumbwa. Please usitoe hiyo mimba, hakuna kitu kizuri duniani kama kuwa na mtoto, usifikirie kujiua kwa sasa, ujiue ili uweje? Usikubali mtu akukatishie maisha yako, be strong, utalea tu mtoto.

Fikiria maisha ya mtoto wako huyo aliyo tumboni..........hebu mshirikishe mama yako kama ulivyotushirikisha hapa JF. Naweza sema mama yako ndio faraja yako kwa sasa.
Kwa sasa unaweza kata mawasiliano na huyo mwanaume kwa sababu najua una hasira sana na ukichanganya na mimba ndio kabisaa hasira inazidi.
 
Latifa my dear,
pole sana!
Sioni sababu ya kujiua wala kumkatili mwanao maisha.
Leo ujauzito wako,mtoto ni zawadi,wapo walio kwenye ndoa hawajapata watoto,kwanini wewe umkatae wakati tayari yupo njiani?
USIJIUE,USITOE MIMBA.
Jingine lakini gumu kulikubali ni kuhusu kumshirikisha huyo mwanaume kuhusu hali yako.

Vyovyote iwavyo huyo ni baba yake kwa maelezo yako,mwambie ukweli kua umegundua uongo wake na huwezi kuendelea katika uhusiano huo. Mwambie khs ujauzito,usijali atapokeaje ila kikubwa umemwambia na ujipange kulea

la tatu khs kuwafuata waliokua wanakutaka ukawakataa,SIKUSHAURI!
Wao watatumia matatizo yako kukupata na aliye timamu atahoji mbona ulimkataa wakati ule huna ujauzito unamwendea leo?
Ni wazi atajua kilichokupeleka kwake sio mapenzi ila matatizo yako,anaweza kukuendesha atakavyo ukawa mtumwa wake.
Jitahidi leo mimba yako kwa sasa,kama bado wana nia ya dhati nawe watakuja hata ukishajifungua(MUNGU AKUJALIE)

Lakini pia hujataja dini yako,kama nyote ni waislam usikate tamaa mapema,anaweza kuamua kukuoa haraka ila ndio ujue uke wenza.

Pia umri nao,kama bado binti mdogo bado una nafasi ya kupata mume wako hata kama utakua na mtoto,
ila
kama una umri wangu mie hata usiogope kuwa utaleta aibu nyumbani,huu sio umri wa kutoa mimba,ni ujinga.
Nakutakia kila la heri,Mungu akusaidie mambo yako yaende vizuri.
 
Njoo kwangu nitalea Mimba hiyo!!pole sana ndo ukubwa huo,ma2mizi ya kondomu sijui,ujui dada yangu,njoo kwanga nitalea mimba,Mx
 
....sijawahi kufanya abortion......
au nikae tuu nizae ila nisimshirikishe maana sitaki hata kumtia machoni nimemchukia chuki mbaya.....
ili niwe na amani ni mfute kwenye aliki yangu
Kumfuta akilini huwezi.
Huwezi kuamua nini uwaze.
Kila utakapomuona mtoto utamkumbuka baba, kwa mazuri na mabaya.
 
Acha bro kuna wanaume ving'ang'anizi, mpaka atamuharibia kitumbua chake kwa mwanaume mpya, huyo jamaa mpotezeee! mtose kimya kimya hakuna kumwambia wala nini![/QUO

ni kweli kama bado anakupenda anakuharibia huyo yaani kata connection na yeye chukulilia amekufa, kama anavyosema Bishanga mtoto utampeleka kwa wajomba noo usifanye hivyo mtoto utamuita jina la huyohuyo baba yake ila huyo baba amekufa, sawa?
 
Kitu cha kwanza, inabidi ukubali katika maisha kuna kupoteza mchezo na kuna mchezo unashinda.

Huu mchezo umepoteza, lakini si mwisho wa maisha. Kubali kuwa mtoto ni baraka.
Be proud of yourself.

Achana na baba wa mtoto.
Kutegemea na maumivu uliyonayo amua kama umwambie au umchunie.

kuanza mahusiano mapya, usifanya haraka sana.
Ila unaweza pick kati ya waliokuwa wanakupenda yule unayemwamnini na anaonekana responsible ukamweleza ukweli

mpe muda wa kufikiri na kuamua wakati na wewe ukijipa muda wa kufikiri na kuamua.

Baba halisi wa mtoto hastahili huruma yeyote sababu kwa miaka 2 ashindwe sema ukweli ana mke? Si mwanamme huyo.

Shika imani yako, inasaidia katika wakati kama huu.
Pole sana.
 
Latifa ,achana na ushauri huu wa Loly,jamaa yako mpe fursa ya kulea mimba hata kama una hasira naye vipi,believe me,i am talking from experience ,omba Mungu uzae salama,we na ba mtoto mtaishia kuwa marafiki hata kama sio urafiki wa malavidavi.

Mbona unamkomalia sana Latifa aendelee na jamaa, au ndio wewe uliemwaribia maisha nini? maana humu id ni.............?
 
Tumeona,
Tumeshuhudia,
Tumesikia, mara nyingi tu....
...Kina mama wakitupa mtoto mara baada ya kuzaliwa.
...wengine wakikataa kunyonyesha.
....wengine wakipata ugonjwa wa akili(kichaa) mara baada ya kujifungua mtoto esp. kama alikuwa stress sana wakati wa ujauzito.
Decide wisely.
 
Mbona unamkomalia sana Latifa aendelee na jamaa, au ndio wewe uliemwaribia maisha nini? maana humu id ni.............?

hapana Michael,mi Latifa wala simfaham(though jina lake mashalah),all i am doing ni kusisitiza asikate mawasiliano na ba mtoto,this is important for the child,akue akijua baba ni nani na mama ni nani,hasira za wazazi zisimnyime mtoto fursa hii.
 
hapa sijakuelewa Lizzy ,kivipi asimwambie mwenye mimba? Una maana unataka Latifa acheze kale kamchezo ka kutaifisha mtoto na kumpa u bin wa ujombani?sikubaliani na wewe katika hili,nashauri amwambie jamaa kuwa ana mimba yake lakini hataki mahusiano yao yaendelee ila watunze mimba pamoja in the best way possible.
Latifa,usijiue,mambo madogo sana haya,mi mwenyewe nshawafanyia wanawake madhambi kama haya mara kibao,walizaa na leo tuko marafiki tunalea.We tulia everything will be okay,time is the ultimate healer.

Unamfanyia dhambi huyu kesho unarudia kwa mwingine???
Kumbe huwa mnafanya makusudi maana unajua kama unafanya kosa kwa A kesho unarudia kwa B?
 
Kiranga komo, mkome kuwafungulia kufuli watu ambao hamjaoana, wacheni uzinzi. Sasa nenda kapime kama hajakuachia nao, hizo ndio faida za zinaa.
 
nashukuru sana the boss itabidi nifanye hivyo ila ni rahisi mwanaume kukubali mwanamke mwenye mimba ya mtu mwingine?
sikushauri uanze mahusiano na mwanaume mwingine kwani waweza kuumia zaidi,kaa lea ujauzito lea mtoto, mapenzi yatafuata badae
 
hebu tuliza akili!!

Jaribu kuwasiliana nae kama huwezi kulea mimba na huyo mtoto, mweleze msimamo wako kuhusu mahusiano yenu.kumbuka anaweza kuwa alikuwa anakupenda kweli ingawa ana mke na watoto, wekeni utaratibu wa kulea hiyo mimba na mtoto.

Pili, pumzika na endelea kulea hiyo mimba usifanye maamuzi ambayo utajuta maisha yako yote kila la kheri. Ingawa ni ngumu kuamini upo na mt miaka miwili na unategemea kuolewa nae na hujui kama ana mke, labda ulikuwa hutaki kuamini hadi uone.

Pole sana hilo halikufanyi kutoa uhai wako, mahospitalini watu wanaangaika kuongeza siku za kuishi.

siwezi kuongea nae milele kwanini anidanganye? Hata kama ananipenda kwangu umependo umekwisha atulie na mke wake
 
Kiranga komo, mkome kuwafungulia kufuli watu ambao hamjaoana, wacheni uzinzi. Sasa nenda kapime kama hajakuachia nao, hizo ndio faida za zinaa.

Mbona unamhukumu tena?
Ukweli aambiwe lakini limeshatokea,yupo gizani aoneshwe njia.
 
nifanyeje na hii mimba, sijawahi kufanya abortion naninaogopa san maana najua athari zake
nawaza sijuhi ninywe sumu ya panya nijiondoe duniani?
Now my advice,
Hadi umemention abortion, ni kama tayari una uamuzi.
ila ni woga tu!
I advise you go see a psychiatrist, open to him/her, consider involving your family (mama, baba).
Should you proceed with your decision to abort, PM me i'l recommend one.
Iyo ya red i advise against.

 
Kiranga komo, mkome kuwafungulia kufuli watu ambao hamjaoana, wacheni uzinzi. Sasa nenda kapime kama hajakuachia nao, hizo ndio faida za zinaa.
huyo mama Mchungaji'anakuchana ä live,Mx
 
Back
Top Bottom