Latifa my dear,
pole sana!
Sioni sababu ya kujiua wala kumkatili mwanao maisha.
Leo ujauzito wako,mtoto ni zawadi,wapo walio kwenye ndoa hawajapata watoto,kwanini wewe umkatae wakati tayari yupo njiani?
USIJIUE,USITOE MIMBA.
Jingine lakini gumu kulikubali ni kuhusu kumshirikisha huyo mwanaume kuhusu hali yako.
Vyovyote iwavyo huyo ni baba yake kwa maelezo yako,mwambie ukweli kua umegundua uongo wake na huwezi kuendelea katika uhusiano huo. Mwambie khs ujauzito,usijali atapokeaje ila kikubwa umemwambia na ujipange kulea
la tatu khs kuwafuata waliokua wanakutaka ukawakataa,SIKUSHAURI!
Wao watatumia matatizo yako kukupata na aliye timamu atahoji mbona ulimkataa wakati ule huna ujauzito unamwendea leo?
Ni wazi atajua kilichokupeleka kwake sio mapenzi ila matatizo yako,anaweza kukuendesha atakavyo ukawa mtumwa wake.
Jitahidi leo mimba yako kwa sasa,kama bado wana nia ya dhati nawe watakuja hata ukishajifungua(MUNGU AKUJALIE)
Lakini pia hujataja dini yako,kama nyote ni waislam usikate tamaa mapema,anaweza kuamua kukuoa haraka ila ndio ujue uke wenza.
Pia umri nao,kama bado binti mdogo bado una nafasi ya kupata mume wako hata kama utakua na mtoto,
ila
kama una umri wangu mie hata usiogope kuwa utaleta aibu nyumbani,huu sio umri wa kutoa mimba,ni ujinga.
Nakutakia kila la heri,Mungu akusaidie mambo yako yaende vizuri.