Nimechanganyikiwa, sikujua kama mwisho utakuwa hivi

achana nae makasabraka mkubwa huyo hana shukurani kraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 

usitoe hukumu kwa kusikiliza upande mmoja Dada yangu siyo vyema.
 
Siamini katika kuvumilia ndoa yenye mateso kwa kisingizio cha watoto! Je, siku umevunjwa miguu na mikono plus kutobolewa macho na kutundikwa ukimwi juu, nani atawalea hao watoto? (hiyo reason hainiingii akilini kabisa). Come on lady, u deserve a better life my dear......step out of that marriage!! Umemvumilia miaka yote hiyo angekuwa ni mtu wa kubadilika angeshabadilika, haya maisha ya kuishi kwa kujipa matumaini yatakugharimu ndugu!
 
Naigopa hata kutoa comments zangu hapa manake ni story ya upande mmoja. Naogopa yasije yakatokea kama yale ya The One and The One's Wife kuja kuzodoana hapa jamvini, manake mume alimwaga ugali mke akaamua kumwaga mboga.na sijui wamepotelea wapi hawa wadau, nahisi wamehama jamvini.
 
Ki ukweli hali ya sasa ni mbaya, maradhi ni mengi, lakufanya inatakiwa uangalie kama umethibitisha kuwa jomba ni mlevi wa ngono temana nae. Hakuna cha subra yavuta heri kwa kipindi hiki, "subira yavuta kifo" kwani maisha peke ako huwezi.? Sepa atakuua uo boya.
 
.....hivi sijui kwa nini mungu huwapa wanaume majuha kama hao!!kuwa na moyo mgumu,fanya maamuzi mazito!machozi hata samaki anayo lakini hatuyaoni kwa sababu yanaenda na maji
 
Hakuna jambo baya katika ndoa kama ngono ikiingia. Tendo la ngono ndio ndoa yenxewe. Hata wakatoliki ambao kuvunja ndoa ni mwiko, kukiwa na malalamiko yahusuyo ngono katika ndoa basi ndoa yaweza kuvunjwa. Nakushauri kama unaweza kujitenga na huyo bwana jitenge. Wanaume hatubadiliki.
 
Mpige chini huyo jamaa ishi uishivyo atakutesa mpaka lini????
 
kumuombea sawa but maandiko yanasema jisaidieni nami nitawasaidia

Hiyo si kweli hakuna maandiko kama hayo kwenye Biblia, watu wengi huwa mnapenda kuutumia huu msemo lakini haupo kwenye maandiko bwana
 
wewe....wewe...nadhani bado hujakua vzr!

Ni kweli kabisa,hajakuwa vizuri hivyo hajaona mabo ya dunia wala kusikia habari za ndoa zinazovunjika,mara nyingine kuvunja ndoa ni bora na kuna faida saana kwa wanandoa wenyewe na watoto pia,angalia mazingira unayoishi mambo mengine hayavumiliki ,ina maana unataka ateseke maisha yake yoote yaliyobaki,kama muumba atampa miaka zaidi ya 60 fikiria atateseka kwa miaka mingapi,wanawake msikubali kuteswa ,kudhalilishwa na kunyanyaswa kwani hata mungu hapendi,usidhulumu na usikubali kudhulumiwa vyote hivyo ni dhambiiiiiiiiiii
 
unapozungumzia kutengana na mwenza kwa umri huo ni lazima utajiingiza kwenye mahusano mengine na hii utaifanya kwa sababu utakuwa na uko katika msongo wa mawazo .. swali linakuja ni mahusiano mangapi utaingia baada ya kuvunja ya msingi (ndoa)

kwani kuna ubaya akiingia kwenye uhusiano mwingine kama akiamua?
 
kwani kuna ubaya akiingia kwenye uhusiano mwingine kama akiamua?


Nafikiri hakuna ubaya wowote kama akiingia kwenye mahusiano mengine,

nadhani BPM alikuwa anataka kumaanisha kwamba.........je hayo mahusiano mengine ndo itakuwa kama peponi?

hakutakuwa na shida/ugomvi/misukosuko wala nini..........................je ni kweli....?
 
mpendwa huyo hakuwa na mapenzi na wewe toka mwanzo alikuja kwako kwa ajili ya material things tu ndio maana anakusumbua achana nae watoto nini bana bora uhangaike nao mwenyewe kama ulivyo zoea kuliko kuendelea kuwa na huyo mtu. atakuua na ukimwi huyo
 

bila hayo hakuna mahusiano....hivyo ndio vikorombwezo vyenyewe but hua vinatofautiana, kwenye mahusiano mengine anaweza akapata wa tofauti kabisa na huyu ana akapata zaidi ya huyu, haitabiriki! yotre ni kumuomba Muumba akupe mwenye hofu nae! na Mungu msaidie apate wa kumpa faraja/raha zilizobalia umu duniani....mimekumic!
 
Unaonaje ukimshauri/kumshawishi na yeye aje aombe ushauri humu kwenye JF ili tupate kujua upande wa pili wa shilingi? Manaake hizi kesi za upande mmoja mara nyingi siyo rahisi kuamusa kwa haki.
 

ndo mana nakupenda mamaa kigogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…