POle sana ndeo. naomba nikupe ushauri through my experience. kwanza kabisa naomba nikuambie kua, hujakosea kuleta tatizo lako hapa, ila kupata muafaka hapa ni ngumu maana kila mmoja anasema lake. naomba nikuambie kua mimi nilikaa kwenye ndoa miaka 5 na hivi sasa nina miaka 13 nje ya ndoa viery happy with my two kids. kwanza nakupa hongera wewe ni mvumilivu sana, maana mimi ex husband wangu hakua na tabia kama hizi, zake zilipungua kidogo lakini sikuweza kuvumilia. Naamini kwenye kupendana na sio kuvumilia ndio maana niliamua kundoka kungali mapema. niliondoka nikiwa 30 na watoto wangu walikua wadogo. sikuongea na mtu yoyote juu ya matatizo yangu, walioyajua waliona kwa macho yao, na nilisema nitaongea kuhusu maisha yangu ya ndo pindi nikiondoka, na ndicho nilichofanya. sikutaka kushauriwa na na mtu maana mwisho wa siku wanaokushauri wanarudi makwao wanakuachia kero na karaha za ndoa uliyonayo. binadamu yoyote hawezi kubadilika, tabia ni kama kilema. hakubadilishwa na alie mzaa wewe utaweza wapi wakati mmekutana ukubwani. naomba upime mema na mabaya ya huyo baba uone wapi kuna uzito ndio ufanye maamuzi. kama mema ndio yenye uzito kaa, ukivumilia valangati, kama mabaya ndio mazito basi ondoka taratibu na watoto wako kaanze maisha upya. umesoma na una kazi nzuri jiamini kama mwanamke jasiri, utaweza maisha mwenyewe, na utaona tofauti yake. hapo ulipo huwezi kuendelea maana huyo baba kajaa tele kwenye kichwa chako muda wa kuwaza kitu kingine huna. anawapenda watoto wake, amewafanyia nini hao watoto au ni kudhalilisha familia yake kwa kupita akikopa mtaani na kulipiwa madeni na mkewe ambayo hata hujui kafanyia nini? bora useme kakopa akalipa school fees tutamuelewa. kuondoka kwenye ndoa sio kitu kidogo inataka ujasiri wa hali ya juu, lakini naamini kwa elimu yako na uwezo wako utaweza, jiamini. All the best...!!!