Nimechanganyikiwa, sikujua kama mwisho utakuwa hivi

Nimechanganyikiwa, sikujua kama mwisho utakuwa hivi

Dada pole kwa umri wako miaka 32 akili yako imekomaa,pili huyo mume hakupendi nenda kanisani muachane naye biblia imeruhusu kuachana kama mume au mke ni mzinzi,kwani siku hizi kuna ukimwi je akikuletea?hatuombi, ila kumbuka umesema kipato chako kinatosha kutunza familia kaa pembeni mpe muda kama wa mwaka 1 uone je atajirekebisha?kama ndio mrudie kama la mpotezee lea watoto wako dada ila kuachana sio shughuli ndogo itakugharimu kuna mambo mengi utakutana nayo maswali pia utaulizwa sana na marafiki,ndugu na
Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More
Mkuu hakuna mwanadamu anayeweza kuvunja ndoa ya kikristo! Ni kifo pekee! Kanisa linaweza kuwatenganisha tu ktk mazingira yatayoonesha ndio njia iliyobaki kwa usalama wenu.Yesu alitamka alichounganisha Mungu mwanadamu asivunje.wanaonukuu ule mstari Yesu anaposema isipokuwa kwa uasherati kwa mujibu wa tafsiri kutoka lugha asilia ya ilipoandikwa injili ni inawezekana kwa wale ambao wanaishi ktk maisha ya uasherati(bila ndoa) ndio maana hata ukiishi na mwanamke miaka 20 ukaamua kufunga ndoa na mwingine inayotambulika ni yule ulimpeleka kanisani tu! Hivyo kanisa linapowatenganisha kama nilivyoanisha hapo juu hakuna atayeruhusiwa kuoa au kuolewa na ukifanya mapenzi nje ya mume/mke wa ndoa ni uzinzi tu! Hata ukienda kufunga serikalini au bomani ni uzinzi bila kibali cha Mungu(hapa nawasema wakristo wenzangu).hivyo ndio ninavyofahamu kwa mujibu wa kanisa Katoliki na mafundisho ya ndoa niliyohudhuria.dada pambana kwa njia zote kumbadili Mumeo,huyo ndio uliyepewa na mkapata kibali cha ndoa takatifu,hakuna kinachoshindikana mbele ya Mungu ila washirikishe viongozi wa kanisa mwanzo mwisho watakupa muongozo mzuri tu.hizo ndo shida na raha za ndoa,shida za ndoa si kulala njaa tu! Pambana na kila lakheri!
 
Sijui nianzie wapi?? naandika kwa masikitiko makubwa, miaka 7 iliyopita niliolewa na mwenzangu ambaye nilimpenda baada ya urafiki wa miaka kama 5 japo baadhi ya ndugu zangu hawakupenda niolewe nae coz hana kazi na wala hakusoma aliishia std7 na mimi ni graduate, hakuwa mtu wa kujishughulisha na biashara wala kuajiriwa bali mishen town tu, ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona.
Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi sikulijali hili, lakini tatizo la shughuli kutokuwa na shughuli maalumu nililiona lakini mwenzangu alisisitiza kuwa hawezi kusoma labda biashara japo hakuonyesha juhudi niliamini angebadilika maisha yakaendelea. mie ni muajiriwa nakipato cha kuweza kuitimizia familia hata peke yangu. Niliingia kwenye ndoa nikiamini akiwa mume na baba angebadilika

Tumeingia kwenye ndoa ndio naanza kuona matatizo mengi hap tuna watoto wawili, si muaminifu kwa pesa za watu wala zangu akiazima basi inabidi nilipe kufunika aibu, ni muongo mara nyingi ni uongo usio na sababu sijui ninini?? yote tisa kumi kesi za wanawake ni kibao na ameshaattempt kuoa mara mbili yeye nikazikamata kwenye mtandao, anakaogonjwa na wanawake wazuri na weupe (hata mimi ni mweupe na mzuri lol) so kila nikimkamata ni ugomvi tu na mwisho anaomba mara msamaha lakini anarudia tena. Biashara nilimuanzishia japo biashara yenyewe alikuja kushindwa akafanya eneo la biashara ndio kituo cha kukutana na wanawake wake mpaka nikawa naogopa kupita hiyo mitaa.

Mbali na yote haya jamaa ni abuser, physically, verbally, and emotionally,, huwa napigwa mie nikijaribu kuargue kuhusu tabia yake au mambo ya ndani, pia ananihisi hisi na anapenda kunicontrol kama mtoto. kuna events nyingi sana nikiandika nitawachosha

Sasa wandugu imefikia kipindi mimi mapenzi yameisha na tunawatoto 2, tumejenga (90% ni mchango wangu), gari (90% mchango wangu) na kulisha familia 90% ni mimi, mapenzi yameisha kabisa sio mchezo sidhani kama yatarudi na ninataka kuachana naye, ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu, japo wanae kweli anawapenda sana. Natamani nisiondoke lakini ninavyomjua huwa anaomba msamaha zikipita wiki mbili mwezi vituko vinarudi pale pale so naogopa na umri unakimbia natakiwa niwe na misimamo mapema kwani naona hata kwa malezi ya watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia. naomba nikiri udhaifu wangu katika kupenda naomba msinirushie sana mawe kwa hilo kwa nimeshajua wapi niliteleza.

Naombeni ushauri utakaonisaidia mimi na watoto wangu, based on your experiences maana naogopa hata kuwaambia ndugu zangu kwani watanichua haraka, wameshajitolea hadi nyumba ya mimi kuishi na wanangu, na vikao vimeshakaliwa vingi na kila siku wananiambia niachane nae lakini mimi nilikuwa kichwa hakijakaa vizuri bado, yani siamini kama nitaishi hivi maisha yangu bila mume coz sipendi wala sifurahishwi na maisha ya kuwa single parent at my age of 32, na hili ndio linanifanya nifikirie sana kuhusu maamuzi yangu.
Humu watu wengi wanashauri kihisia zaidi,wengine wanabeba hili kama walivyozoea uboifrendi na ugelifrendi lakini tambua msingi mkubwa wa ndoa yenu ni kutambua ndoa ni moja ya sakramenti takatifu,tatizo lolote lilo nje ya uwezo lako lirudishe kanisani.kule utashauriwa vizuri tu.maneno mengine ni machungu lakini lazima tukwambie.njia ya kuuona ufalme wa mbingu ni nyembamba sana na jehanamu ni pana sana.hebu weka mkanda wako wa harusi ukumbuke maswali uliyoulizwa na padre au mchungaji na uone ulikiri nini! Dunia ina mengi sana usikimbie matatizo na ukakimbilia dhambi kwa kujikuta unaanza mahusiano hata kama yatakupa faraja lakini mbele za Mungu ni uzinzi tu na hakuna kitachobadilisha hilo hata kama utatubu labda umuache huyo mtu baada ya kutubu! Ya nini yote hayo? Kanisani ndio suluhisho kama umefika huko.jamani hivi tunaelewa shida na raha za ndoa maana yake nini? Narudia tena pambana sana kubadili tabia ya mzee ikibidi peleka shauri kanisani! usimuache mumeo mkawapa tabu ya kisaikolojia watoto ambao ni zawadi mliopewa na Mungu na siku ya kufunga ndoa wote mlikiri kuwa tayari kuwapokea na kuwalea.
 
Achana naye akili yako itulie ili uweze kuendeleza maisha yako kwa amani, mtu wa aina hiyo anakufanya ushindwe kufikiria vizuri namna ya kuboresha maisha yako na hata kukupunguza ari yako ya kufanya kazi kwa bidii ofisini, wanaume wa siku hizi hata uwe wa kuvutia vipi na mwenye heshima vipi, utashangaa atakavyokuwa anakuzingua, na mara nyingi huyo anayemfuata hata unakuta hakufikii kwa uzuri, sijui ni limbwata au, but siku zote uzuri wa mtu ni tabia, but cha kushangaza tu siku hizi hata uwe na tabia njema na heshima, bado unazinguliwa na kutukanwa, kwa upande wako, cha kwanza onana na wanasheria ili angalau upate uelewa wa mambo ya talaka, mgawanyiko wa mali na malezi ya watoto, hapo pia kikubwa ni kujua mali zipi mtagawana na ni zipi haitakiwi kugawana nae, sio kila mali utatakiwa ugawane naye hasa zile ulizokuwa nazo kabla ya ndoa, si kila mtu unayemwona ana maana, wengine wana hila, hata umtendee wema gani yeye hataonyesha kukujali, kukuheshimu wala kukuthamini, we achana naye, uwe na raha na amani na watoto wako, usiwe na hofu furaha utaipata kwa watoto wako na utakapompata atakayekupenda vya kutosha, kukujali na kukuthamini, achana naye kabisa, na ikiwezekana watoto wapeleke boarding school kama wanasoma ili akili yao itulie zaidi kwenye masomo na watachangamka pia na kufurahi kucheza na kuongea na wenzao shuleni bila kukumbuka sana kasheshe za nyumbani na wewe pia kupata muda wa kuwa bize zaidi na shughuli zako za kimaendeleo, achana naye ule kwa raha, uishi kwa amani, na akili yako iwe huru zaidi kwenye shughuli zako.
 
wanaJF nimejaribu kupitia maoni yenu wote ila mm ntakuwa tofauti, kwanza sii haki kutoa hukumu ya upande mmoja,
kwa hapa kila mmoja anamwona huyo bwana ana hatia sana,
lakini je tutajuaje upande wa pili wa huyu dada? yeye hana makucha? hajatueleza mabaya yake mwenyewe.
Nijuavo ktk nyumba mara nyingi mwanaume hawezi kuwa mkorofi,jeuri au mhuni kama mke wake hamtendei kiburi,
yawezekana huyu dada anamsimanga mumewe kwa kuwa hana elimu au hana hela na mtaji kampa yeye basi kumsema kila siku tutajuaje,
na pia huenda anamkotrol kwa kila kitu,hapo lazima mwanaume aamue kufanya hayo maasi anayofanya kama kisasi.
siku zote wanaume ni kama watoto akiona hatendewi haki ktk nyumba hasira huhamia kwa wanawake wengine.
Kwa vile huyu mwanaume nae hatujamsikiliza sii sahihi kuwa na jibu moja la kumhukumu kwamba ni mkosaji.
Siamini kama huyu dada tena ana jina la kichaga asilimia mia lazima nae ana mapungufu yake kwa mumewe
sisemi mengi hapa ntashambuliwa na wachanga ila wanajijua upande wa kina dada.
namsshauri ajiangalie kwanza yeye kama yuko safi the last resort waende kwenye mabaraza ya usuluhishi wasiposuluhika basi waombe kutengana hata kanisa linaruhusu kutengana au talaka kama sheria ya ndoa 1971 inavosema ili kunusuru maisha yake na watoto. dadangu mbeee hebu na ww tueleze mapungufu yako hapa hauwezi kuwa positive kwa kila kitu mayb alikamata sms zako na mambo mengineyo.
 
;japo baadhi ya ndugu zangu hawakupenda niolewe nae coz hana kazi na wala hakusoma aliishia std7 na mimi ni graduate, hakuwa mtu wa kujishughulisha na biashara wala kuajiriwa bali mishen town tu, ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona.Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi sikulijali hili, lakini tatizo la shughuli kutokuwa na shughuli maalumu nililiona lakini mwenzangu alisisitiza kuwa hawezi kusoma labda biashara japo hakuonyesha juhudi niliamini angebadilika maisha yakaendelea. mie ni muajiriwa nakipato cha kuweza kuitimizia familia hata peke yangu. Niliingia kwenye ndoa nikiamini akiwa mume na baba angebadilika
Hakuna ukweli kwa maelezo yako bibi.
 
Tumeingia kwenye ndoa ndio naanza kuona matatizo mengi hap tuna watoto wawili, si muaminifu kwa pesa za watu wala zangu akiazima basi inabidi nilipe kufunika aibu, ni muongo mara nyingi ni uongo usio na sababu sijui ninini?? yote tisa kumi kesi za wanawake ni kibao na ameshaattempt kuoa mara mbili yeye nikazikamata kwenye mtandao, anakaogonjwa na wanawake wazuri na weupe (hata mimi ni mweupe na mzuri lol) so kila nikimkamata ni ugomvi tu na mwisho anaomba mara msamaha lakini anarudia tena. Biashara nilimuanzishia japo biashara yenyewe alikuja kushindwa akafanya eneo la biashara ndio kituo cha kukutana na wanawake wake mpaka nikawa naogopa kupita hiyo mitaa.
Vitu vya kutunga akuna ukweli.
Pili ujaolewa kwa hiyo unaongerea hisia tu.
Tatu umegraduate nini.? waweza kumaliza naye darasa la saba we ukasoma veta chereani au
 
Sasa wandugu imefikia kipindi mimi mapenzi yameisha na tunawatoto 2, tumejenga (90% ni mchango wangu), gari (90% mchango wangu) na kulisha familia 90% ni mimi, mapenzi yameisha kabisa sio mchezo sidhani kama yatarudi na ninataka kuachana naye, ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu, japo wanae kweli anawapenda sana. Natamani nisiondoke lakini ninavyomjua huwa anaomba msamaha zikipita wiki mbili mwezi vituko vinarudi pale pale so naogopa na umri unakimbia natakiwa niwe na misimamo mapema kwani naona hata kwa malezi ya watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia. naomba nikiri udhaifu wangu katika kupenda naomba msinirushie sana mawe kwa hilo kwa nimeshajua wapi niliteleza.

Naombeni ushauri .

Ndugu ushauri gani mama huyu anataka.
I- We bibi ndo mwenye tattizo kwa kuisi mali mlizonazo we ndo mletaji.
II- We ndo wamyanyasa mwanaume kwa kujiona wamzidi elimu na sijui na kiwango gani
iV- Isije kuwa mali waongwa na madume unaleta kwa bwana wako kama vimbo
V- Mama we siyo mkweli hadithi yako
Vii- Hacha umayala kama kweli umeolewa.
 
Nakutaadharisha atakuletea Ukimwi huyo kuwa makini sana hali mbaya siku hz.......ila akikupiga mbebe peleka lupango tu kwani watoto Luba wabebe kaishi nao kwani kama ulivyosema kila kitu unaprovide wewe sasa wasi wasi wako nini wakati umri wako ni wa kawaida tu 32 sio mkubwa sana...Ila pole sana Mungu yuko pamoja na wewe ubarikiwe sana.
 
Pole sana dear, kikubwa pia kilichochangia sana ni umbali wa elimu yenu, kutoka kwako na yeye, hata ufanye nini kuna vitu hawezi kuelewa kama wewe. Sivizuri kumshauri mtu kuachana na mumewe lakini mi naomba unisamehe kwa kukwambia, ni bora uanze maisha yako mapema kabla hujaletewa vya kuletewa na watoto unaowapenda ukawaachia watu. Mungu atanisamehe kwa hilo, lakini mwanaume akishaanza kukuchanganyia madawa, hata kaa abadilike, kwa kawaida hubadilika kwa dakika tano na kurudia hali yake. Maisha ya single parent si marahisi unapoyaanza kama unavyodhani lakini, ukishaanza utazoea na utaona mambo yako yakienda my dear, hata baraka za mungu ulizokua huzipati kwa urahisi kwasababu ya manung'uniko ya moyo wako juu ya huyo kiumbe utaziona zikija kwa wingi. Cha muhim unapokua single parent ukaendelee kujiheshim ili watoto wako wakakue kwa maadili mema na ya kimungu. Na usiruhusu vi wanaume vinavyokuja nakujidai vinakupenda kumbe nia yao vikuchune viishie. Kwani wanaume wengi wakiona mtu ana mtoto au watoto wanadhani alishazeeka na kakata tamaa, pia ni wakutumiwa tu, vijitu vya aina hiyo visome mapema na usivipe nafasi hata ya kupajua kwako. Itafikia wakati kila jambo litajipanga bila hata wewe kuhisi maumivu, mtu aliekataa kujiendeleza kwa kusoma bila kujali au kuumia roho kwa kuishi na mtu aliemucha mbali vile. Hayuko tayari kwa mabadiliko yeyote, pia hawezi hata changia point mnapokua na rafiki zenu, huyo muombee tu kwa mungu aspate tu magonjwa ila BE CAREFUL WATOTO NIZAWADI KUTOKA KWA MUNGU, ISIWE KISINGIZIO.
 
Maswari mengi sana..?
1-
miaka 7 iliyopita niliolewa na mwenzangu ambaye nilimpenda baada ya urafiki wa miaka kama 5&nbsp sasa ni 2011 toa 7 ni 2004 mmeoana siyo,toa 5miaka 1999 ndo mmekutana.?
2- ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona)-wakati huwo we ulikuwa wasoma au wafanya biashara.?3
3-Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi siku
lijali hili,
)- Je ulikuwa kipofu na ujitambu hili baada au kabla ya ndoa?
4-Mbali na yote haya jamaa ni abuser, physically, verbally, and emotionally,, wamaanisha maumbile yake je ni sifa mbaya au nzuri.?kuna events nyingi sana nikiandika nitawachosha hapo umeficha ukweli
5-
ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu-kutengana kwa muda?,
Je umeomba taraka.? kwani watoto ni wanani?,
Unaisi anoogopa ukali wa maisha ?
Je wazazi wenu na wasimamizi wenu kanisani wanajua >
6-watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia.?????????
7- UMRI WA MMEO.?
8- ???? Unazalilisha wanaume kwa hadithi ya kutunga.?hakuna mtiriko sahihi.Polisi mama utafungwa
 
Asanteni kwa michango yenu, tatizo kubwa mapenzi yameisha kabisa na ikumbukwe mapenzi ndio pekee yaliyotuunganisha, mimi simfuatilii tena na hata yeye anajua mapenzi yameisha,, na nataka kuondoka kweli ndani kabisa ya moyo wangu natamani kuondoka ila nikiwaangalia watoto roho inasita! sio yeye ninayemuhurumia bali ni watoto yani simtamani hata kumuona natamani aondoke asafiri aende mbali huko.
kwenye red; unasema unataka kuondoka?? utaondokaje kwenye nyumba yako dada angu?? yeye ndo aondoke, plz jitambue kwa mchango wako mkubwa wewe ndo unahaki vinginevyo bachelor itakuwa haikusaidii.
pili; yaani mpaka nashangaa jamani, mimi nilikuwa chuo mwaka wa 3, 2008 nikawa na GF mwenye masters,kwakweli alikuwa na pozi balaa na nilijui nikimuoa itakuwa balaa zaidi, yeye alikuwa ananipenda but dharau kwa marafiki zangu na wivu kupitiliza, nikaachana nae nikasema basi ntaoa daraja la chini diploma/degree. sasa inakuwaje std 7 anamsumbua bachelor? kama umegeuza story eeehh? dah i am surprised.....
sisi umetuandikia ila wewe ndo upo field/uwanjani, kama hali ni tete sioni haja ya kujiumiza kila leo, hakuna cha ukaribu na watoto, kama mtu anasumbua unapiga chini. day care school zipo nyingi tu....tuache kulea matatizo
 
daa hiii kesi ninngekuwa hakimu sijui ningeiamuaje maana ngumu sana sana. lakini mimi nashauri kabla ya kuachana mweke chini kwa mara ya mwisho ump[e somo tena somo kweli na umwambie uamuzi wako kama hatabadiliki. kama hujaelewa what i mean sikiliza wimbo wa shaggy unaitwa ultimatum sa mwambie kama yule msichana anayeimba chorus alivyokuwa anamwambia shaggy
 
Wadau wooooooote asanteni sana, im so proud to have you all, nimeongea na mwenzangu pamoja na ndugu zetu wa karibu na tumeamua kujipa muda zaidi tuangaliane lakini huku tukijikinga na kumonitor afya zetu, inauma watoto kuishi bila wazazi wote so nimejitolea nadhani na mwenzangu pia amejitolea kwa moyo, tunamuomba mungu atusaidie katika haya mapito. naomba msinitupe nikirudi tena, natumaini safari hii nitarudi tena kwa heri na si shari. Mzee wa rubisi nashukuru kwa hizo doubts zako lakini kumbuka si kila aliyeko jamii forums ana muda wa kupoteza kuandika story ya uongo, after all niwadanganye itanisaidia nini wakati nahitaji msaada wa ushaur nitatue matatizo yangu na wala hamnijui??? ASANTENI WOTE
 
Kesha ukiomba kwa maana haujui siku wala saa........
 
Pole sana, kuvumilia pasipokuwepo mipango thabiti ya utatuzi wa kile unachuvumilia ni sawa na kukalia moto ukidhani utazimika. nakushauri urudishe moyo wa mapenzi ndipo uombe ushauri kwani kusema mapenzi yameisha kabisa ni kwamba tayari jibu/maamuzi unayo. Taswira ya hayo ulikuwa nayo tangu uchumba na niwazi ulijipanga kukabiliana nayo. Hebu tumia fimbo uliyonayo hao wanawake anaowatafuta ni kwakuwa ana cha kuwapa akikosa atakoma ama atahamia kwa atakayemshika mkono kwa kupenda kilichokuvutia wewe na sasa hukihitaji tena. Mvalie miwani ya mbao bila kumwonyesha dharau.
 
Bila kuficha wala kung'ata maneno,wewe ni mwanamke fisadi,mwenye dharau na mwongo. Miaka 5 ya urafiki usimjue tu mwenzako,haya 7 yrs ya ndoa unakuja na mapya! Kumbuka mwanamke mpumbavu ndo pekee huivunja nyumba kwa mikono yake. Mpende mumeo,mjali mumeo,mheshimu mumeo na kuwa mwaminifu kwa mumeo uone kama ataenda kupiga pai sehemu nyingine.
 
Humu watu wengi wanashauri kihisia zaidi,wengine wanabeba hili kama walivyozoea uboifrendi na ugelifrendi lakini tambua msingi mkubwa wa ndoa yenu ni kutambua ndoa ni moja ya sakramenti takatifu,tatizo lolote lilo nje ya uwezo lako lirudishe kanisani.kule utashauriwa vizuri tu.maneno mengine ni machungu lakini lazima tukwambie.njia ya kuuona ufalme wa mbingu ni nyembamba sana na jehanamu ni pana sana.hebu weka mkanda wako wa harusi ukumbuke maswali uliyoulizwa na padre au mchungaji na uone ulikiri nini! Dunia ina mengi sana usikimbie matatizo na ukakimbilia dhambi kwa kujikuta unaanza mahusiano hata kama yatakupa faraja lakini mbele za Mungu ni uzinzi tu na hakuna kitachobadilisha hilo hata kama utatubu labda umuache huyo mtu baada ya kutubu! Ya nini yote hayo? Kanisani ndio suluhisho kama umefika huko.jamani hivi tunaelewa shida na raha za ndoa maana yake nini? Narudia tena pambana sana kubadili tabia ya mzee ikibidi peleka shauri kanisani! usimuache mumeo mkawapa tabu ya kisaikolojia watoto ambao ni zawadi mliopewa na Mungu na siku ya kufunga ndoa wote mlikiri kuwa tayari kuwapokea na kuwalea.
kwel! Then pia fanya maombi sana atabadilika.
 
Acha kufikiria watoto wewe ndio mwenye watoto katika hali kama hiyo,
Mbona kuna wanawake wengi kwa sasa wao ndio baba wao ndio mama
Piga chini huyo walee wanao! We unafikiri watakuwa wanafaidika nini kama
mambo yenyewe ndiyo hayo? Mama anapigwa wao wanashuhudia acha acha
kabisa.......... Sasa tutaishi kimikataba na si mapenzi tena!

Nathani hii ya mkataba itakuwa pouwa zaidi
 
Back
Top Bottom