Nimechoka kuajiriwa sekta binafsi, vikampuni uchwara

Nimechoka kuajiriwa sekta binafsi, vikampuni uchwara

nikajiajiri Dar es Salaam.


1730816423340.png

1730816443723.png
 
Naombeni ushauri wadau waliofanikiwa baada ya kuwaza kama mimi. Mimi ni muajiliwa(kibarua) kampuni flani kwa sababu sina mkataba wowote sasa imefika muda kazi nimeifanya kwa muda mrefu sana nimechoka hivyo nataka nimwambie HR wa kampuni anipe barua yangu ya kuachishwa kazi ili niipeleke NSSF nikavute hicho kidogo kilichoko huko nikajiajiri Dar es Salaam.

N:B: Naishi mkoani, nimezaliwa mkoani, nimekulia mkoani lakinj ndoto zangu ni kuishi Dar na kuzeekea Dar.
SIrikalini sasa ipo ppp ambayo ni pete na chanda na hiyo private sector unayoiona uchara hapa sasa sijui majobless unatuacha njia panda gani,ya kigongo busisi,ya makoroboi ya segera,ya makuyuni ama ya wapi?
 
Acha hiyo kazi mkuu. Wanadamu tunaishi kama Simba japo wapo wanadamu wachache wanataka kuishi kama Swala. Sifa ya Simba ni kuwinda na kujitafutia chakula ndio maana anaweza kumla swala. Swala yeye anaamka asubuhi kama mwaajiriwa anakula nyasi na kushiba. Swala hali nyama. Swala angekua anajua kuwinda lazima naye angekula nyama. Kama Simba anaamka asubuhi kutafuta nyama wewe ni nani ushindwe kutafuta nyama. Kumbuka Simba hali nyasi wala majani anakula nyama kama sisi. Akiamka asubuhi anaumiza kichwa apate wapi nyama.

Swala analiwa kwasababu hajui kuwinda. Uhalisia ni kwamba Mungu hakumuumba mwanadamu aajiriwe. Alimuumba afanye kazi za asili. Kazi za asili ni kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara. Na ndio maana mtu akistaafu tu hujikuta anarudi kufanya kazi za asili. Kazi za asili hazina kustaafu hizo ni mpaka mwisho wa maisha ya mwanadamu. Bila kufanya kazi ya asili huwezi kutosha hapa duniani.

Note: Ukishastaafu tu ili ule lazima ufanye kazi za asili. Na ukitaka kuishi kama swala lazima utaliwa.
 
Sisi tuliozaliwa dar tunataka tukazeekee shamba, ndo mana tumenunua kimbiji huko.

Unataka kuja kufanya biashara gani ukishatoa hela yako huko nssf
mawazo yangu pengine hafifu yananifanya nijiulize maswali mbona nyie mnaishi dar basi mi pia nataka nije kufanya mishe kama zenu lakini ziwe za kihalali tu.
 
kampuni yenye uhai inatakiwa kila siku wafanyakazi waingie na kuwacha/wachishwa.

Serikali ndiyo mtu anaganda toka anamaliza shule mpaka anastaafu au anafia hapo hapo.

Ukiona mtu hawachiwi kuondoka na kampuni binafsi elewa kuwa huyo ni mali (asset) muhimu sana.

Mfanyakazi kwenye kampuni binafsi anapimwa kama mali (asset) yoyote ile, kuna "appreciation" na "depreciation". Mali (asset) ikifikia kuwa dhima (liability) haina sababu ya kubaki kwenye kampuni.
Kwa hiyo kwa tathimini yako kulingana na bandiko langu. Je, mimi ni asset au liability?
 
Back
Top Bottom