Nimechoka kuajiriwa sekta binafsi, vikampuni uchwara

Jambo lolote ukitaka kupiga hatua lazima uwe na mipango ,Dar watu wanaishi kwasababu TU ya riziki ila si kwamba wanapakubali watu ni nyomii kwanini hayo mawazo yako usiyafanyie hapo hapo mkoani
Basi kama wanaishi kwa sababu ya riziki ni dhahiri kwamba riziki zipo na zinapatikana kwa haraka kulinganisha na mikoani.
 
Mwaka 2004 niliwahi kuwa na mawazo kama haya, nilipo chukua NSSF ilikwisha hata sikujua imeishaje.
Leo hii nimerudi, mwaka wa 20 kwenye ajira tuliokua tukiita (kazi za kijinga) na mafanikio nimeyaona aiseee
2004 ndo unaanza kazi duuh we ni mdogo wangu kabisa uwe unanisalimia mkuu
 
Jambo lolote ukitaka kupiga hatua lazima uwe na mipango ,Dar watu wanaishi kwasababu TU ya riziki ila si kwamba wanapakubali watu ni nyomii kwanini hayo mawazo yako usiyafanyie hapo hapo mkoani
Jamaa anapaswa aelewe licha ya dar kuwa na population kubwa ila maisha ni magumu mno! Ushindani wa kibiashara ni mkubwa mno kiasi kwamba hyo hela nsssf inaweza kuisha kabla hajasimama vizuri.
 
Fanya kitu roho inapenda ila ukweli nisiouficha ni kuwa Dar utaenda kupigika mpaka ukumbuke tukampuni uchwara
 
Huu ndio ukweli mchungu uliopo katika sekta binafsi. Watu hawaangalii utu au upendo, kinachojaliwa ni thamani gani unaongeza katika kampani

Haijalishi ulikuwa vizuri hadi kuiingizia pesa nyingi kampuni miaka mitano nyuma. Kama hauingizi tena faida au kuna mtu anafanya vyema kukuzidi ni lazma tu utaondoka
 
Hapana, ndoto zako tu.
kwahiyo kwako wewe mtu competent ni yule anaefikilia kuendelea kuajiliwa kuliko kujiairi akatanua ubongo wake kwa kuwaza nje ya box,hayo nayo ni mawazo ya kimasikini na woga wa maisha
 
kwahiyo kwako wewe mtu competent ni yule anaefikilia kuendelea kuajiliwa kuliko kujiairi akatanua ubongo wake kwa kuwaza nje ya box,hayo nayo ni mawazo ya kimasikini na woga wa maisha
= kuajiriwa.

Mimi hainihusu akijiajiri au akiajiriwa. Nakwenda na mada ilivyo, pitia tena maoni yangu juu huko.

Nisome kwa utulivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…