Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Unachoka kwasababu vyote hapo vinatumia mafuta

Kula vyakula vya kuchemsha hutokinai
 
Aina za upishi ni nyingi sanaaa unaweza pika kiazi mviringo kwa namna ya kipekee na usichoke kula....ni vile tumezoea mapishi ya mazoea.

Ila tuuuuu mapishi masotojo yanahitaji muda na pesa.
Exactly, ukila vyakula vya mchemsho mfano ndizi, viazi etc ni ngumu sana kukinai...tatizo ni vyote hapo anapika kwa mafuta
 
Corn flakes unanunua.. unachemsha maziwa fresh, unaweka kwa kibakuli afu unaweka vijiko kadhaa vya hiyo cornflakes mlo tayari

Nimemaanisha hizo ndizi ni bukoba, mshale, au mzuzu?
😂😂 Mi sijui kutofautisha aina za ndizi
 
Kupika ni Sanaa ukiiwezea hiyo Sanaa hutokinai.
Simple recipe.
Ndizi chemsha na chumvi tu.
Kuku au nyama yoyote
Mchemshe na vitunguu. Akiiva badala ya kuunga.
Saga kitunguu kimoja
Kata kitunguu kimoja
Kwangua karot moja
Hoho moja nzima
Weka vyote na pilipili acha vichemke mpaka viive.
Mchicha chnganya na Chinese.
Katakata
Hoho
Karoti
Kitunguu
Baada ya hapo kamulia limao au ndimu chnganya vyote pika.
Pakua msosi wako halafu nipe mrejesho.
 
Gentleman,
ukijihisi hutaki au unachukia mambo ya dunia hii, basi hiyo maana yake ya dunia hii ndio unayaaga taratibu hivyo kuelekea kwa baba 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…