Nimechoka kulalia godoro chini

Nimechoka kulalia godoro chini

Pole sana. Ila kama ni kweli ndo hali uliyo nayo napenda kukumbusha kuwa matatizo yako yanachangiwa na ujinga wako mwenyewe. Kipato duni unakimbilia kuoa ili ugundue nini? JINGA SANA. Cha muhimu pambana sana kwasababu hiyo hali ikiendelea lazima huyo mwanamke akuache au atafute mtu mwenye kitanda kizuri.
 
Mkuu!

Niliishawahi kupitia msoto kama huu miaka kitambo! Maisha yalisimama kabisa nikawa sisogei! Kana kwamba kuna mtu alipiga mstari nisivuke hapa! Kana kwamba kuna roho fulani siioni inayozuia nisipige hatua! Nikipata hela majanga yanaibuka na kunirudisha palepale (square one)!

Nikausoma mchezo kwa kutumia uzoefu, nikakomaa na kuwa ng'ang'ari mpaka nikatoboa! Ndio siri ya hii nickname "no retreat no surrender". Kwahiyo mkuu komaa jitathmini wapi unakwama! Wakati mwingine kuwa mbishi na usiendekeze huruma kwa mambo yasiyo na manufaa ya kukupotezea muda na hela!
We mwamba. Tutatusua tu man.
 
Kitanda anasa

FB_IMG_16943545576073176.jpg
 
Mtoa mada umejichanganya mambo yafuatayo.
1. Ulipaswa kununua kitanda na godoro kabla ya kuoa Kwa sababu baada ya kuoa mambo yanakuwaga mengi.
2. Tamaa ya kutereza. Ulitanguliza tamaa ya kugegeda badala ya kujipanga kwanza mwisho wa siku unakuja kulia lia hapa jukwaani.
 
Maisha haya yasikie tu kwa mwenzio

Muda mwingine tunajitahidi kupanga malengo na kuyapambanua yatimie tukipiga hatua 3 mbele tunavutwa na kurudishwa hatua 6 nyuma na matatizo yasiyo epukia

Nimeshalala sana chini na wife mwaka unaenda kukata Sasa bila ya kitanda

Naweka Nia mpaka mwezi huu unaisha nitalala juu ya kitanda hapa nina 35 elfu ngoja nianze kununua mbao niwe naweka mpaka zikienea napeleka kwa fundi sofa.

Hii kazi yangu kwa mwezi inaniingizia angalau si chini ya laki 2 ukitoa 80 ya Kodi ya ofisi na nyumbani,

Shida matatizo yananisonga japo kiafya tunamshukuru Mungu tuko poa
Zipo nchi nyingi sana ambazo watu wake hawatumii vitanda wala makochi, wao hulala chini na hukalia mikeka.
 
Back
Top Bottom