Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Naibili

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,878
Reaction score
1,060
Wanajamvi,

Leo nimekuja, mwenzenu yamenifika shingoni

Nina miaka mitatu tangu nimeingi kwenye uchimbaji wa madini huku Chunya, Mbeya.

Nimamiliki karasha, nimeshapoteza zaidi ya milioni 40 katika shughuli hii.

Huwa nnajitahidi kupima miamba kila hatua kama inavyoshauriwa lkn matokeo mara zote huwa kinyume na matarajio.

Mfano unaweza kupima mwamba ukaambiwa ni wastani wa ppm 8 lkn unachokuja kukipata ni wastani wa ppm 1

Wadau wengi hawataki kutoa siri ya wapi wanapitia ili kuhakikisha kile wanachotakiwa kukipata wanakipata.

Tafadhali sana, mwenye kujua namna nnaweza kupata msaada wa kweli tafadhali msaada hapo PM
 
Tunafanya kisasa mkuu, tunatumia maabara bora kabisa, hata sample inachukuliwa kitaalam kabisa
 
Wewe uko theoritical sana hayo mambo hayaendi kisomi kama unavo fikilia njoo migodini ujionee watu wanagundua madini bila hizo theory zenu.
 
Haya mambo haya. Hata sisi 2019 tulikuwa huko tukashindwa tukahamia shinyanga tukapiga mwanzo baadaye hola! Nikajitoa mwenzangu akabaki. Amekula hasara naye katoka mwaka jana. Lakini wengine wako poa kabisa wana make. Mimi hapo kwenye ppm ndipo nashangaa inasoma hivi matokeo baadaye ni tofauti. Sitaki kusikia kabisa hizi habari.
 
Kipimo gani ofsa?

Unazungumzia kitu kama hiki?



Hicho kipimo cha milion 10 ni level za GMT (pichani) ambacho sio mchongo kabisa na siku hizi hakifai hata kwa survey.

Uchimbaji wa madini wa mdau ni wa karasha wa kudili na mawe maana yake hayo mavipimo kwa shughuli yake ni useless




 
Nimekataa kuwa na plan b mkuu, acha nikomae, lkn wengine anapima hata ikipishana ni kidogo sana
 
Wewe uko theoritical sana hayo mambo hayaendi kisomi kama unavo fikilia njoo migodini ujionee watu wanagundua madini bila hizo theory zenu.
Ndio shida yenu wachimbaji wadogo....ujuaji mwingi hivi unadhani Migodi mikubwa kama GGM,Barrick kuwa na maexpert wa kutosha na advanced tools ni wajinga....wewe kama unachimba loko na unapata faida basi jua unajichelewesha sana mkuu....acha kudharau taaluma za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…