Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Nilivyosikia mimi ukianza kutoa, itabidi uwe unatoa,

Kuna pahala nilisikia kuwa kuna hiyo dawa moja inaitwa NGEKEWA hii kila utakachogusa ni hela tu ila sasa kila mwaka inakula mtu mmoja, inachagua yenyewe wewe utashangaa mtu kadondoka mara mzazi, rafiki, ndugu, mfanyakazi
Hapo ndio mnadanganywa Ngekewa ni aina ya mvuto unakua nao, unakumbuka mwenda zake alivyobadili upepo kipndi kile cha uchaguzi??? Na si kila dawa inahitaji damu ya mtu wako... Kwenye madini bila ndumba utaishia kuwasindikiza kina nyanda madirisha
 
Milioni 40 ungewekeza kwenye biashara nyingine saa hii ungekuwa unahesabu faida ya ya laki tatu au nne kwa siku.

Hizi biashara hazifanywi kwa kubeti zinataka utaalamu mzuri wa miamba ambao utaweza kukuonyesha mahala madini yalipo. Vifaa vya kisasa vipo na vinakusaidia kuona madini yalipo. Nadhani unatakiwa kujipanga upya kwenye hii kazi.
Mkuu kama unahisi unajua, nikwambie tu bado, kuna theory na practical si ndo mnasema hivyo kitaalam.
 
Wanajamvi

Leo nimekuja, mwenzenu yamenifika shingoni

Nina miaka mitatu tangu nimeingi kwenye uchimbaji wa madini huku chunya mbeya,

Nimamiliki karasha, nimeshapoteza zaidi ya milioni 40 katika shughuli hii.

Huwa nnajitahidi kupima miamba kila hatua kama inavyoshauriwa lkn matokeo mara zote huwa kinyume na matarajio,

Mfano unaweza kupima mwamba ukaambiwa ni wastani wa ppm 8 lkn unachokuja kukipata ni wastani wa ppm 1

Wadau wengi hawataki kutoa siri ya wapi wanapitia ili kuhakikisha kile wanachotakiwa kukipata wanakipata,

Tafadhali sana, mwenye kujua namna nnaweza kupata msaada wa kweli tafadhali msaada hapo PM
Pole Sana bro km nakuona vile ulivyokata tamaaa, kwa ufupi tu Mtangulize Mungu kwanza ndo uje ufanye maamuzi
 
Waganga wangekuwa na uwezo wa kuwafanikishia mafanikio huko migoni nafikiri hata wao wangeongoza kwa kuchimba madini na Kuwa mabilionea, eti unataka umfuate mganga umlipe laki mbili au tatu alafu yeye akufanikishie kupata dhahabu ya Milioni 200 kweli?

Hivi mnafikiri vizuri kweli
 
Hapo akuna uchawi bob hapo unapigwa eithr plant au illution...napajua chunya na tulishakuwa na mgodi chunya(semi mining) huko kuna michezo hiyo sana vijana wa ilution wanapiga pesa sana...mambo ya stiliwaya yametawala huko na ni kutokana na wachimbaji wa huko wamechelewa kuijua dhahabu tofauti na kanda ya ziwa..changamoto niliyo iona kanda ya ziwa ni uchawi😅 dhahabu inapigwa kiuchawi ukipeleka lundo plant hakuna kitu..so ukitaka kufanya biashara hii jikane nafsi tu
 
Mkuu ninaomba kufahamu baadhi ya vitu kwako, ni kwamba una karasha then una mtaji wako je hyo miamba unayopima unachimba mwenyewe na je duara lako Lina urefu gani? Na je vip maduara ya jirani na wewe yanatoaje pia je unapiga tu na kumwaga rundo au Kuna Wakati huwa unachenjuwa kwa mercury? Kwenye upimaji wa ppm na kusoma juu halafu mwisho kusoma chini Kuna sababu nyingi lazima nijue je mawe yako unayatoa yote sehemu moja tu au unakuwa unachanganya changanya ? Pamoja na kwamba una pima ppm ila jitahid sana kufanya bottle test ama kupima black ya udongo wako itakusaidi pia kujua kama udongo wako unasoma juuu au chini, yaani usije kuridhika eti ppm inasoma 8 ukajua ndo Iko ivo kote , unaweza kufanya bottle test plant ukakuta uhalisia wa ppm ni 4 au 2, nipo tayari pia kusikia na kupokea mawazo mapya kutoka kwa wadau wengine
 
Waganga wangekuwa na uwezo wa kuwafanikishia mafanikio huko migoni nafikiri hata wao wangeongoza kwa kuchimba madini na Kuwa mabilionea, eti unataka umfuate mganga umlipe laki mbili au tatu alafu yeye akufanikishie kupata dhahabu ya Milioni 200 kweli?

Hivi mnafikiri vizuri kweli
Sema nini mkuu, bado hujaijua dunia, tembea uyaone
 
Unatumia njia gani kupima natural au artificial ??je unatumia wataalamu
Binafsi nakushauri mkuu jitahidi kufanya kazi na wataalamu na kuna kamashine kanauzwa milioni 10 nako hutumika kudetect madini aina mbali mbali.Tembea depertment za UDSM na UDOM utawapa wataalamu wa kutosha au nenda GST.

Chunya kuna reserve kubwa sana ya dhahabu so jitahid ufanye kisasa boss


Binafsi nasomea mineral exploration and mining geology.Namaliza mwakani
reserve ipo kiwango gani kama una taarifa
 
Back
Top Bottom