Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Hapo ndio mnadanganywa Ngekewa ni aina ya mvuto unakua nao, unakumbuka mwenda zake alivyobadili upepo kipndi kile cha uchaguzi??? Na si kila dawa inahitaji damu ya mtu wako... Kwenye madini bila ndumba utaishia kuwasindikiza kina nyanda madirisha
 
Mkuu kama unahisi unajua, nikwambie tu bado, kuna theory na practical si ndo mnasema hivyo kitaalam.
 
Pole Sana bro km nakuona vile ulivyokata tamaaa, kwa ufupi tu Mtangulize Mungu kwanza ndo uje ufanye maamuzi
 
Waganga wangekuwa na uwezo wa kuwafanikishia mafanikio huko migoni nafikiri hata wao wangeongoza kwa kuchimba madini na Kuwa mabilionea, eti unataka umfuate mganga umlipe laki mbili au tatu alafu yeye akufanikishie kupata dhahabu ya Milioni 200 kweli?

Hivi mnafikiri vizuri kweli
 
Hapo akuna uchawi bob hapo unapigwa eithr plant au illution...napajua chunya na tulishakuwa na mgodi chunya(semi mining) huko kuna michezo hiyo sana vijana wa ilution wanapiga pesa sana...mambo ya stiliwaya yametawala huko na ni kutokana na wachimbaji wa huko wamechelewa kuijua dhahabu tofauti na kanda ya ziwa..changamoto niliyo iona kanda ya ziwa ni uchawi😅 dhahabu inapigwa kiuchawi ukipeleka lundo plant hakuna kitu..so ukitaka kufanya biashara hii jikane nafsi tu
 
Mkuu ninaomba kufahamu baadhi ya vitu kwako, ni kwamba una karasha then una mtaji wako je hyo miamba unayopima unachimba mwenyewe na je duara lako Lina urefu gani? Na je vip maduara ya jirani na wewe yanatoaje pia je unapiga tu na kumwaga rundo au Kuna Wakati huwa unachenjuwa kwa mercury? Kwenye upimaji wa ppm na kusoma juu halafu mwisho kusoma chini Kuna sababu nyingi lazima nijue je mawe yako unayatoa yote sehemu moja tu au unakuwa unachanganya changanya ? Pamoja na kwamba una pima ppm ila jitahid sana kufanya bottle test ama kupima black ya udongo wako itakusaidi pia kujua kama udongo wako unasoma juuu au chini, yaani usije kuridhika eti ppm inasoma 8 ukajua ndo Iko ivo kote , unaweza kufanya bottle test plant ukakuta uhalisia wa ppm ni 4 au 2, nipo tayari pia kusikia na kupokea mawazo mapya kutoka kwa wadau wengine
 
Sema nini mkuu, bado hujaijua dunia, tembea uyaone
 
reserve ipo kiwango gani kama una taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…