Mpaka miaka mi4 iliyopita nilikuwa mwembamba sana. Yaani nilikuwa sijawahi kunenepa.
Kuna option kadhaa za kunenepa. Best option ni mazoezi, wengi wanachukulia mazoezi ni kwa ajili ya kupungua tu. What I did,
1. Chakula - nilianza kula milo mi 5 kwa siku. Siyo lazima iwe mikubwa ila kula kula haswa. Basically nilikuwa nakula saa 1 asubuhi, saa 4 asubuhi, saa 7 mchana, saa 10 jioni na saa 2 usiku.
2. Mazoezi - ingawa hutaki mazoezi ila kula peke yake utanenepa kwa kuwa na nyama zembe, unahitaji mazoezi kunenepa kwa shape. Ila avoid mazoezi kama ya kukimbia maana yanatumia calories nyingi na hutumika kupunguza unene, nyama zembe na mambo mengine.
3. Protein shakes - kwa kuwa balance diet ni gharama na sometimes siyo rahisi kupata, basi tafuta protein shake. Be careful hapa, kuna fake na utofauti wa content. Pia tumia kiasi, zinahitaji nidhamu.
Sisi wa mazoezi tunapenda protein shake yenye high protein low calories. Kwa kuwa calories(energy) za ziada usizotumia huleta unene/nyama uzembe. Balance is the key. Ukiihitaji contact za anayeuza ni cheki pm.
4. Consistent - usifanye hivyo vitu wiki moja au mwezi ukaacha. Hutovuka. Jipe atleast 4 months. Hakikisha unachukua vipimo mwanzo na kila wiki. Wewe unaweza ona hakuna maendeleo ila yapo.
5. Mapumziko - tunavyoambiwa tunahitaji 8 hours za kulala, si masihara. Ni muhimu sana sana aisee.
Lastly usitake kunenepa tu, nenepa ki afya, maana unene mbaya ni tatizo kubwa mno.
Mfano mzuri wa mwili ni kama mmea. Hauhitaji maji tu, inahitaji pia mbolea, jua, uangalizi.