Nimechoka kuwa mwembamba

Mkuu hii diet inazidi kipato changu.
hunenepi sio kuwa huna kipato cha kutosha!
HUJARIDHIKA NA KIPATO ULICONACHO!
ukikipata HUTAHITAJI KULA ULIVYOANDIKIWA ILI UNENEPE!
manake mi najionaga nikiwa na hela najikuta tu sisikii njaa!


BUT WEMBAMBA UNA TATIZO GANI LAKIN?
tuanzie hapo kwanza?
 
Mkuu mbona simple sana kuwa na mwili mkubwa. Ishu ni msosi tena msosi wa kutosha tu

Kula vyakula vya wanga kuzidi mahitaji ya mwili wako yaani ww kula wanga mpaka ukinai alafu kula tena uo wanga.(umenielewa?)

Sababu unene ni matokeo ya wingi wa wanga mwilini yaani ule wanga wa ziada ndio unaleta ubonge

Alafu pia kula mayai hasa wakuchemsha 2-3 kwa siku hii idadi ni mujarabu kabisa, hapa kumbuka kitu kimoja mayai hayanenepeshi ila yata control huo ubonge wako usije kuwa bonge nyanya sawa mkuu?

Usisahau bia moja kila siku (siyo kirikuu) kama ni kirikuu basi viwili [emoji3].

NB: Japo hupendi mazoezi nakushauri kwenye huu ulaji upige tumazoezi kidogo kila siku.

UKISHINDWA HUU ULAJI BASI TUMIA HILI LI DUDE NITAKALOLIWEKA HAPO CHINI, HILO NI WIKI MBILI TU UNANUNIA SURUALI MPYA
 
Najifurahia na ubonge wangu

Sasa mkuu ukishaongezeka itakusaidia nini?
 

Hivi mtu unakula vyote hivi?

chapati tatu supu ya n'gombe soda baridiiii na maji baridiii Asubuhi tu?

Asubuhi

-hapo nitakula Chapati mbili na maziwa..supu situmii...soda siwezi kunywa asubuhi... hayo -maji siwezi kuyanywa asubuhi nipo sehemu ina baridi saana.

MCHANA
-ugali nyama hapa nitaula.
-soda sitakunywa..Nitakula tunda.
-maji nitakunywa.

USIKU
-Nyama choma na ndizi.. sitaweza kula nitakuwa nimeshibashiba...nitakula kitu sweet.
-Bia sitaweza kunywa lbda wine ya kutafutia usingizi.

RATIBA YAKO ITANISHINDA MKUU.
 
Best comment man. Aridhike alivyo. Yuko ambae atamkubali the way alivyo .
 
acha kabisa kufanya ngono atleast kwa mwaka mmoja na jitahidi kula vyakula vyenye mafuta kama karanga mbichi,korosho
 
Sasa kama hujikubari basi huo ndo ugonjwa wa kujitakia kunenepa hakulazimishwi
 
Mkuu bei gani hiyo whey

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…