Nimechoka maisha ya ughaibuni

Rudi kama boma liwanza mkuu
 
Badala ya kutafuta pesa na ku save unataka vijiwe vya kashata kama wale wacheza draft na bao kutwa nzima?!

Mtafute Mkenya uone kama ana mawazo kama haya ya kwako.

Ukiona huwezi hayo maisha. Basi fanya kazi. Save money, rudi bongo kuwekeza.
 
Ww hauna shukrani.
 
Ni mwiko kukata tamaa, ila jifunze kuyasoma mazingira kama ni rafiki au sio rafiki.

Inawezekana wewe ndo kikwazo kwenye maisha yako, aidha una tabia zinazokwamisha mafanikio yako.

Wewe ndo mtu unayejijua zaidi, tafuta connection nzuri za kukuvusha hapo ulipo kwenda hatua nyingine.

Usikae na watu ambao wote mna lingana akili mpaka mafanikio, tafuta watu watakao kupa msimamo wa kufanikiwa zaidi.
 
Anayetoboa akienda ughaibuni ni yule ambaye angetoboa hata akibakia Tanzania. Nimekaa nje ya Tanzania(Europe 6yrs, Middle East 2yrs) lakini nimeona asilimia kidogo sana ndo wanatoboa.

Unahitaji kuwa smart na uishi maisha halisi, ufanye savings sana starehe iwe kidogo sana. Mtu akiwaza maisha ya Bongo yalivyo magumu kiutafutaji kama huna wazazi ambao ni well off, halafu akapata nafasi ya kwenda nje kutafuta, halafu akatumia anachokipata kwa magari ya kukodi, gamble na maisha ya Rick Ross, huyu binafsi namuweka kundi moja na mbweha pori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…