Mwana kulitafuta, mwana kulipata. To each his own.
Kujitambua wewe mwenyewe unataka nini tangu awali na kuishi bila kufuata mkumbo ni kitu muhimu sana.
Mimi niliamua kuhama nchi (Tanzania to US), si kuja ughaibuni kujaribu maisha halafu nikishindwa nirudi Bongo.
I was "America or Burst" like
Balki Bartokomous from "
Perfect Strangers"
Nilikuwa kama yule Jemedari aliyevuka bahari halafu alivyofika ng'ambo ya pili akachoma mashua moto ili vita iwe mbele kwa mbele bila option ya kurudi nyuma na kuvuka kwenda ng'ambo ya kwanza kwa mashua.
Na kwa sababu nilishaamua mbele kwa mbele, nimefanikiwa kwa kiasi changu na sina mpango wa kurudi Bongo kimoja, labda likizo tu.
Kwanza sioni mtu/ deal la kunilipa $250,000 kwa mwaka Bongo, as a minimum, not counting real estate portfolio, bila kuhangaika sana, bila hata kutoka nyumbani kwangu, na bila wizi au rushwa, vitu ambavyo sivitaki. I am talking squeakly clean money.
Sasa nikiacha michongo yangu huku ambapo nina uhakika wa kupiga US $1,000 kwa siku, at a minimum, kabla sijaangalia mingo zangu za real estate and other investments, nirudi Bongo, niache access ya kuwekeza New York Stock Exchange na world markets zote, nirudi Bongo nikahangaike na umeme wa TANESCO, internet ya manati, tozo zisizotabirika, na ujinga mwingine wa jumla na rejareja kama huo, nitakuwa mjinga kiasi gani hapo?
Eti niache a minimum of US $1,000 kwa siku (ambayo ndiyo around GDP per capita ya Bongo by the way), kwa sababu na miss vijiwe vya kahawa vya Bongo. Hata huko kwenye vijiwe vya kahawa wakisikia hivyo mbona naona kama watanipiga mawe? Vijiwe vya kahawa siku hizi si ndo hivi tunakutana JF?
Yani wana wananiangalia mimi ndiye balozi wao, kaka mkubwa, wakija US wanafikia kwangu, ma cousins wanaokuja kusoma na wao wajue wana address ya mtu wa nyumbani US, wana sehemu hata za kufikishia barua na kutumia address kuanzisha kampuni, halafu na mimi balozi wao tena nirudi nyumbani wakija huku wafikie wapi?
Kikubwa zaidi, nilishaamua kuondoka Bongo na kuishi Marekani na uamuzi wangu ulikuwa wa kubadili makazi kimoja, si wa kujaribu maisha ughaibuni na kurudi nyumbani.