Utazoea tu, nakumbuka Form V nilichaguliwa shule ipo Wilaya haikuwa imeendelea kivile. Siku ya kwenda tu barabara mbovu gari inazingua kila wakati. Kesho yake kengele ya uji ngri ngriii nikaenda kuchukua but kitu uji wa dona nilishindwa kula nikamwaga jeuri ikaisha baada ya vinyama nilivyofungiwa home kuisha nikawa mpole wiki ya pili tu nikaanza kuzoea.
bora wewe umepata hata nyumba mimi nimepoteza matumaini kabisa kwenda shule kila siku na usafiri nauli2000.
Duuuuuuu!pole sana!wilaya gani hiyo?isije ikawa ninayoenda na mimi.
Dadaangu,ualimu ni WITO..jitahidi tu u-adapt na mazingira,utapata thawabu. Makubwa mengi yaja, kuna kura ya maoni ya rasimu na kuna daftari la uchaguzi 2015-zote pia ni kazi za walimu ktk uandikishaji..Usikimbie!
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Kuna mdogo wangu yuko Udom 1sr year, Education..akipitia huu uzi ataacha chuo.
Ila kuwa mbunifu wa kuendana na mazingira. Usitegemee kila mahali Tanzania ni pazuri, Kaa chini tafakari jinsi ya kuongeza kipato kwa kwenda huko ulipopangiwa kwani naamini uko vizuri kiakili na kiujasiriamali zaidi ya hao wanakijiji. Changamka, usilaumu na kuangalia vitu vidogovidogo. Pole kwa kubadili mazingira.