Nimechoka mwili na roho mwalimu miye loh!!!

Nimechoka mwili na roho mwalimu miye loh!!!

Munkari kumbe na wewe ni Ticha, walimu ni wito kwanini hutaki kuitika lakini? Vumilia bwana, sasa wanangu nani atawafundisha?

ha ha eti wanao,bonge la ticha miye!! Wito uliisha enzi za mwalimuu!! Mzima lakini?
 
Last edited by a moderator:
Kurudi shule kunatatua vp hilo tatizo?

wenye hiyo elimu unayotaka kuongeza hawana changamoto?

inatatua mbona ntakuwa nimetoka huku mazimaa! Chamoto zipo tu ila kwa level nyingine !!
 
Ndo nchi yetu hii tuipende kivyovyote...

Maendeleo huletwa na sisi mi nakuombea kwa mungu akupe Faraja katika wakati huu mgumu

mmmh unavyontia moyo loh asante mwaya!!
 
Utazoea tu, nakumbuka Form V nilichaguliwa shule ipo Wilaya haikuwa imeendelea kivile. Siku ya kwenda tu barabara mbovu gari inazingua kila wakati. Kesho yake kengele ya uji ngri ngriii nikaenda kuchukua but kitu uji wa dona nilishindwa kula nikamwaga jeuri ikaisha baada ya vinyama nilivyofungiwa home kuisha nikawa mpole wiki ya pili tu nikaanza kuzoea.

duu miye ningetoroka!! Yaani Rogie huku hapafai nataman kuweka picha ila natumia simu aisee gari mwisho sa sita ukichelewa unalala mjini afu kuna hayo maondrova sasa eti ndo gari za abiria ha ha hapana kwa kweli!!nimekuwa mpole kama maji ya mtungini!
 
Last edited by a moderator:
Kumbuka kutumia busara kupata tena ajira serikalini ni kazi sana kama utaondoka ulikopangiwa bila utaratibu
 
utawapata tuu...afu najua wanawake huwa ni wavumilivu tofauti na wanaume......piga kazi then uhame mkuu!!!

mmmh uvumilivu na maumivu!! Sijui ngoja nione!! Ila daaaa majangaaa mbona majangaa!
 
bora wewe umepata hata nyumba mimi nimepoteza matumaini kabisa kwenda shule kila siku na usafiri nauli2000.

duuu! Mama polee fanya hima huko uhame wallah utapata retardation loh ujue kinachoniuma kingne hakuna interaction yani wewe na walimu wenzio tu akuuh!! Nsijekupata utindio wa ubongo!!
 
Duuuuuuu!pole sana!wilaya gani hiyo?isije ikawa ninayoenda na mimi.

asante mwalimu ha ha utachokaaa ole wako uje singida v !kuna mwenzangu hapa katoka ruvuma anasema bora ya huko kwao sa huyo anasema hivyo miye mtoto wa darisalama niliyezoea kuku kwa mrija je? Akuu miye!!
 
Dadaangu,ualimu ni WITO..jitahidi tu u-adapt na mazingira,utapata thawabu. Makubwa mengi yaja, kuna kura ya maoni ya rasimu na kuna daftari la uchaguzi 2015-zote pia ni kazi za walimu ktk uandikishaji..Usikimbie!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

mmmh nashukuuru kwa kunipa moyo ila mmmh yani moyo wangu umekufa ganzi kabisaaaaaaaaaaa !!
 
Pole tcha ila pambana tu utazoea, hv ndo kuna wale jamaa wanaitwaje wale wachunga ng'ombe! Ahahaha shughuli pevu!
 
Ha!ha!ha! Mbona nipo nae apa.aache izo mazingira syo mabaya kivile.apa lazima ampate mchumba iliadumu apa.

ha ha ha toka pa! Wachumba gani wanafanana na pori wamechokaaaaa!! Aku miye waniwache !!
 
Mwalimu,fursa ni popote,kuna watu unawaona mjini leo ila wameibukia kijijini sana tena kwa mazingira tata sana,piga moyo konde,jipe moyo,najua baada ya miezi mitatu utani PM,nakutakia uvumilivu mwema!

mmmh haya bwana ubarikiwe!
 
Kuna mdogo wangu yuko Udom 1sr year, Education..akipitia huu uzi ataacha chuo.
Ila kuwa mbunifu wa kuendana na mazingira. Usitegemee kila mahali Tanzania ni pazuri, Kaa chini tafakari jinsi ya kuongeza kipato kwa kwenda huko ulipopangiwa kwani naamini uko vizuri kiakili na kiujasiriamali zaidi ya hao wanakijiji. Changamka, usilaumu na kuangalia vitu vidogovidogo. Pole kwa kubadili mazingira.

muandae mdogo wako psychologically miye hapa nshaharibikiwa !
 
Back
Top Bottom