Nimechoka mwili na roho mwalimu miye loh!!!

Nimechoka mwili na roho mwalimu miye loh!!!

Nakutumia nauli ya kurudi! Basi la kuja Dar ratiba yake ni lini vile!??
 
Komaaa bill ya vipodozi kuanzia kichwani mpaka kwenye kucha za miguuni niachie mimi.

ha ha! Unadhani hata hivyo vipodozi ntavitumia huku? Si watoto wataniachia darasa! ?
 
Munkari, nakushauri jipe miezi kadhaa utazoea tu mwalimu
 
muandae mdogo wako psychologically miye hapa nshaharibikiwa !
Hakuna haja ya kuchanganyikiwa mkuu,wewe pambana tu, tafuta biashara kama za mazao uwe unaleta mjini wakati unaendelea na kazi. Achana na mawazo ya ki-Dar es salaam, pigana tafuta hela. sisi tunakuja vijijini kutafuta mashamba ili kuongeza kipato wakat tunaendelea na kazi, na inatugharimu kwani inabidi uweke msimamizi sababu tuko mbali. Ila wewe ukiamua kutuliza akili, aaah muda mfupi tu utakua mbali sababu utakua unasimamia vyema. Pole kwa mazingira mapya.
 
Acha uwoga. Komaa na hayo mazingira, na hivi ni damu changa, Mawazo yako na vitendo chanya vinahitajika kuleta mabadiliko katika hayo mazingira.

i wish niwawekee picha vilee ! Mmmh au kwakuwa nimezoea kuyaona magorofa ya posta na kkoo? Aaah hapana bwana huku kwa ajabu!! Nashkuru kwa kunipa moyo!
 
Daaah! Baada ya kufurahia mapokezi yote toka halmashauri mmmmh pozi limeniisha baada ya kufika kituoni!....... Mama wee! kweli na miaka yangu 3 na mavyeti yangu ng'aring'ari na urembo wangu huu !! Niishi huku? Yani daaaah wallah nisijekufelisha watoto wa watu kwa makusudi !......... ,yani nimeangalia sura za wanafunzi naona zimechooka sijui ndo wamekata tamaa khaa!!............ hiyo nyumba sasa tuliyoandaliwa mama wee hapo ndo pamenichoshaa kinyumba kibaya hichoo aisee nicjebakwa huku mtoto wa watu, huo usafiri sasa kwenda mjini mwisho wa mwezi!! Aaagh narudi kwetu sitaki tena watanizeesha !!!

Vumulia bibie kwani mvumilivu hula mbivu.
 
na hapo cjajua masomo yako ni yap kwan km ni sayansi utakutana na lundo la vipindi..
 
Ualimu ni wito jamani sio ukipata 3 ukimbilie ualimu li upate boom.. mtatufelishia wato wetu.
 
kama MWALIMU. kweli utavumilia na wewe ndio utakua wa kuwabadilisha hao wanafunzi na kuwa na sura za mafanikio.... wewe ni kioo kwao mwalimu..... HEBU OKOA TAIFA LISIANGAMIE..... futa usemi wa kuwa "MWALIMU ALIKUA NYERERE WENGINE MATICHA TU" Mwalimu usikate tamaa.
 
Hebu anza kutafuta bei ya mashamba huko tuje tuwekeze sawa mwl ?
 
Back
Top Bottom