Nimechoka, naenda kununua gari

Nunua gari wapite watu kwa kukaa.
 
Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujue kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!

UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
 
Waleko msalam, hiyo paragraph ya mwisho nimeielewa zaidi 😃😃
 
Wee nunua gari bwana lah sivyo utelezi hutapata kijana. Bongo daresalama bila usafiri pisi kali utaishia wapigia nyeto tuu
 
Pesa yako na unaitafuta mwenyewe we tumia ambapo roho inapenda, ila subaru ni nzuri ila ni gharama kuitunza.

Nasema vuta chuma, vuta ndinga hata used in bongo.
 
Hakuna IST ya 7.5m nzima ndugu.. unaenda nunua matatzo... Utakuwa mteja wa fundi kila siku..

Ni bora ukanunua gari ndogo ya brand nyingne kwa hela hiyo lakini mpya..

Zipo swift, fun cargo.. vi nissan kibao..

Hiyo gari ya mkononi utajuta
 
Ukweli kwa DSM gari si anasa. Gari ni kitu muhimu kwenye kuanzia maisha. Nunua Gari ambayo ni economy ila isiwe chakavu kwani Gari ya kwanza ikiwa chakavu itakufilisi. Hii ni kwa sababu hautakubali kupak utakuwa unapambana kwa namna yoyote kuhakikisha ipo barabarani.

Kuna adha kubwa sana utapata kama huna usafiri ikiwemo swala la matumizi ya muda. Ukiwa na gari kila unapotaka kwenda utafika kwa wakati tofauti na anaetumia daladala.

Hata kama utaamua kuanza na kujenga utakutana na changamoto kubwa katika usimamizi kwani ukiwa na gari unaweza chomoka kazini faster ukafika site na ukarudi kazini. Hata pale utakapokuwa unatakiwa kusafirisha vitu vidogo vidogo kupeleka site.

Changamoto nyingine ukiwa na familia kama huna usafiri unaoeleweka utajuta na gharama za kukodi magari zinakuwa kubwa sana kwani kuna watoto hospitali, mke clinic na ufuatiliaji wa mambo mengine.


Mwisho, mimi ni mmoja ambao niliwahi kuwa na fikra kama zako. Lakini kutokana na changamoto mbalimbali niliamua kujilipua nikakopa. Tena sikuwa na hata ya kuongezea kama wewe. Nusu nilinunua eneo na nyingine nikanunua IST.

Sijawahi juta kwani ilinisaidia sana na iliniwezesha kufanya kazi zaidi ya moja na kuweza kuendeleza kiwanja kuwa makazi.

Gharama za usafiri zilipungua huku nikiwa na privacy kwenye mambo yangu ya kifamilia.

Gari linanunuliwa siku moja. Nyumba inajengwa Miaka kadhaa kama unakipato cha kawaida.

Huu ni ushauri waweza amua vinginevyo
 
We hupaswi kupewa ushaur

Umeshasema ulikuja humu jukwaani ukaomba ushauri watu wakakwambia kabisa kuwa usinunue gari.

Matokeo yake we mwenyewe leo hii umerudi jukwaani na kusema umechoka lazima ukanunue gari tafsir yake ni lwamba umeshapingana na ushauri uliopewa.

Sasa hata leo watu wakikushauri si utapingana nao tena?

sasa wakupe ushauri wa nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…