Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujuwe kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!
UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
Sasa atatokaje na gari bila kutazama mafuta as if gari inatumia upepo?
Acha kumtisha mwenzako bana. Gari haina gharama kiasi hicho kwenye kuihudumia. Kuna option nyingi sana za kuweza kuishi na gari mjini.
Changamoto ya gari labda ilete shida kifaa au spare ya gharama ambayo gari haitakiwi kuwapo barabarani kwa muda huo hadi kibadilishwe. Ila mengine ni ya kawaida tu.
Kuna siku mtu unafua ila gari ikiwa na mafuta unatoka vizuri unakwenda kwa wadau mnapeana dili maisha yanasonga.
Watu wengi wanaopiga mikwara au kutoa vitisho juu ya kumiliki usafiri ni kwasababu kadhaa, aidha hawajawahi kabisa kumiliki gari kabisa na hata wazazi wao pia na ndugu ni hivyo hivyo, walimiliki gari kwa muda mfupi sana na hawajawahi tena, waliuziwa gari bovu mkononi likawatesa, wanauwezo wa kununua magari ila vipaumbele vyao kama kuhudumia ukoo, familia na michango ya nyumba za ibada vinawalimit kuamua kununua gari, wanatamani gari ila hawana uwezo so hawataki wengine wanunue kwa kuwatia hofu.
Gari labda kwa mwanamke ndio sio muhimu maana akiwa na mwanaume mwenye gari ataweza kupata usafiri kama kawa. Ila kwa mwanaume baada ya pumbu inafuata gari kwa umuhimu, yaani gari kwa mwanaume ni mwili wake akiwa nje kwenye jamii. Mwanaume akiwekewa M20 aambiwe chagua kujenga au kununua gari ataamua gari sababu ni asili yetu.
Hivi umeshawahi kusimama kituoni unasubiri daladala na mpenzi wako/mkeo halafu anatokea mfanyakazi mwenzake wanafanya ofisi moja anampigia honi anamsalimia na kumpa ishara ya lift, wewe utakataa asipande aendelee kusubiria daladala na anakwenda mbali na muda unakwenda tena kipindi cha jua kali?
Ile feeling huwa ni mojawapo ya sababu why tunasacrife kununua magari, mkeo apate protection unampeleka hadi job unamdrop au anakwenda sehemu unamshusha unakuja mpitia baadae.