Nimechoka, naenda kununua gari

Nimechoka, naenda kununua gari

Sabb zako za kununua gari ni dhaifu sana uwe na malengo ya zaidi na hilo, gari Dar ina hudumiwa kwa average ya 20,000 kwa kila siku mwezi ni 600k, mshahara wako kama ni 900k monthly, siunaona unaingia kwenye dimbwi la 'urban silent poverty'
Sio kweli. Kuna siku anaweza paki na kutumia bodaboda au daladala.

Kuna siku anaweza pata offer ya mafuta mtu kamuwekea.

Gharama za magari huwa hazifanani.
 
Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujuwe kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!

UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
Sasa atatokaje na gari bila kutazama mafuta as if gari inatumia upepo?

Acha kumtisha mwenzako bana. Gari haina gharama kiasi hicho kwenye kuihudumia. Kuna option nyingi sana za kuweza kuishi na gari mjini.

Changamoto ya gari labda ilete shida kifaa au spare ya gharama ambayo gari haitakiwi kuwapo barabarani kwa muda huo hadi kibadilishwe. Ila mengine ni ya kawaida tu.

Kuna siku mtu unafua ila gari ikiwa na mafuta unatoka vizuri unakwenda kwa wadau mnapeana dili maisha yanasonga.

Watu wengi wanaopiga mikwara au kutoa vitisho juu ya kumiliki usafiri ni kwasababu kadhaa, aidha hawajawahi kabisa kumiliki gari kabisa na hata wazazi wao pia na ndugu ni hivyo hivyo, walimiliki gari kwa muda mfupi sana na hawajawahi tena, waliuziwa gari bovu mkononi likawatesa, wanauwezo wa kununua magari ila vipaumbele vyao kama kuhudumia ukoo, familia na michango ya nyumba za ibada vinawalimit kuamua kununua gari, wanatamani gari ila hawana uwezo so hawataki wengine wanunue kwa kuwatia hofu.

Gari labda kwa mwanamke ndio sio muhimu maana akiwa na mwanaume mwenye gari ataweza kupata usafiri kama kawa. Ila kwa mwanaume baada ya pumbu inafuata gari kwa umuhimu, yaani gari kwa mwanaume ni mwili wake akiwa nje kwenye jamii. Mwanaume akiwekewa M20 aambiwe chagua kujenga au kununua gari ataamua gari sababu ni asili yetu.

Hivi umeshawahi kusimama kituoni unasubiri daladala na mpenzi wako/mkeo halafu anatokea mfanyakazi mwenzake wanafanya ofisi moja anampigia honi anamsalimia na kumpa ishara ya lift, wewe utakataa asipande aendelee kusubiria daladala na anakwenda mbali na muda unakwenda tena kipindi cha jua kali?

Ile feeling huwa ni mojawapo ya sababu why tunasacrife kununua magari, mkeo apate protection unampeleka hadi job unamdrop au anakwenda sehemu unamshusha unakuja mpitia baadae.
 
Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Sasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
Ningeweza kurudisha miaka nyuma ningechagua kutonunua gari na matokeo yake ningefungua biashara ili isaidiane na kazi zangu katika kukuza uchumi.

Gari inalemaza nashindwa kuacha kutumia yaani ni utumwa mkubwa mno.

Nunua tu mkuu tusaidiane maumivu ya wese[emoji16][emoji16]
 
Unakopa Millions 3.5
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]jf raha sana, mabaharia wamempa ushauri sawa na mleta uzi anavyotaka.
Ukweli ni kwamba wanamchora.
Mkopo 3.5m.
Gari sio ya biashara?
Soon ataanza kugongea pesa ya wese
 
Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujuwe kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!

UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
Umeongea kweli tupu.
Mfano hauko vizuri kipesa ukaamua ukapande usafiri wa umma yaani unapotembea kila mtu akikutaza kama vile anatakukuuliza leo gari iko wapi?[emoji28]
 
Angalia unavyoenda kazini kwa daladala unatumia sh. ngapi! Ukiwa na gari yako unatumia mafuta kiasi gani. Ila ujue gari ni gharama, Mimi ninaona ni kitu cha ziada baada ya kukamilisha kikamilifu yale mahitaji matatu ya binadamu (nyumba mavazi na chakula)
 
Sababu zako za kununua gari ni dhaifu sana, uwe na malengo ya zaidi na hilo, gari Dar inahudumiwa kwa average ya 20,000 kwa kila siku mwezi ni 600k, mshahara wako kama ni 900k monthly, siunaona unaingia kwenye dimbwi la 'urban silent poverty'
wewe endelea na maisha yako

unapigiaje hesabu pesa ya mwanaume?

wacha atembelee kalio
 
Kwa Dar gari ni hitaji la msingi...hasa design za ist, vitz, passo...bado kuna watu watakusema unavimba na ki 'baby walker' ila furaha yake utakuwa unaijua wewe...no stress, unaenda nacho hadi gengeni.
 
Pesa ni yako kanunue tu

Na madeni yatakuwa yako sio yetu

Mambo yako tumekuachia mwenyewe.
 
Hakuna IST ya 7.5m nzima ndugu.. unaenda nunua matatzo... Utakuwa mteja wa fundi kila siku..

Ni bora ukanunua gari ndogo ya brand nyingne kwa hela hiyo lakini mpya..

Zipo swift, fun cargo.. vi nissan kibao..

Hiyo gari ya mkononi utajuta
Atafute mazda demio anaweza pata kwa hio bei mpya from japan
 
Nunua gari Mkuu, mwanaume kuishi mjini bila gari ni fedheha kubwa sana aisee
 
Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Sasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
Fanya kitu roho inapenda75% watumishi wenye magar wamekopa
 
Sababu zako za kununua gari ni dhaifu sana, uwe na malengo ya zaidi na hilo, gari Dar inahudumiwa kwa average ya 20,000 kwa kila siku mwezi ni 600k, mshahara wako kama ni 900k monthly, siunaona unaingia kwenye dimbwi la 'urban silent poverty'
Uongo, af wasio wah kumilik magar ndio ushar wao huo yaaan wanataka kila mtu awe kama wao
 
Back
Top Bottom