Nimechoshwa na huyu mwanaume

Zabibu

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Posts
256
Reaction score
54
Wapendwa, nina mpenzi ambaye simwelewi tabia yake,yeye anataka kila siku mimi nimpe hela pindi anapokuwa na shida, eti kisa mimi nafanya kazi yeye bado anasoma.Na kama ikitokea kakuomba hela afu huna inakuwa ugomvi kwamba simjali najithamini mimi tu.Nimeshajaribu kumweleza kuwa mimi huwa namsaidia kwa kumuonea huruma tu na wala sio jukumu langu na haipaswi yeye kunigeuza mimi ndio mlezi wake ila hailewi.
Asa sijui hata nimwelewesheje? kwasababu jambo hili huzua ugomvi mara kwa mara. Msaada tafadhari
 
I hope wewe ni she!

Vijana wa siku hizi wamegundua hako kamtindo ka kulelewa, tena akitoka hapo anaenda kuwaambia rafiki zake!
 
Umeona juhudi yoyote toka kwake upande wa kutafuta kazi? maana wanafunzi wengi wana fanya kazi pia.
Kama hakuna juhudi, na umemwambia mara nyingi kua sio jukumu lako (which is true) na yeye akaendelea kua mvivu na kukuomba wewe (tena anaomba kama analipisha deni) basi ni bora mtazame uhusiano wenu upya maana swala la pesa ni muhimu katika uhusiano na nibora toka mwanzo watu wawe na mtazamo mmoja kuhusi role, source and place ya pesa katika relation.
 
I hope wewe ni she!

Vijana wa siku hizi wamegundua hako kamtindo ka kulelewa, tena akitoka hapo anaenda kuwaambia rafiki zake!
Not only anawaambia rafiki zake but anaweza pia kuwahonga bibi zake huko nje! (but this is another topic)
 

Endelea kumtunza tu hivyo hivyo, si umependa boga mamaaa! Ila angalia sana, siku kiongozi wa uingereza akija tz hakikisha humuachi atembee peke yake kama wakati huo atakuwa ana shida ya hela. Maana style yake ya kuomba hela toka kwako inatia mashaka sana kwa siku zijazo
 
Mi nadhani inategemea ilikuwaje we ukaanza kumpa hela ?mara ya kwanza alikuelezea shida yake uliipokeaje pengine kama ww ni he ulimuingia kwa gia ya pesa si tatizo maana wengi mnakopaga na kuazima mradi tu uonekane mambo safi then badae ndio hivyo tena ..hapo inategemea na jinsi mlivyoanzana lol kaa naye muelezane ukweli halisi kama anakupenda atakuelewa na akikukimbia basi wako ambao wapo after money !!!wanasemaga hapa hapendwi mtu ....
 
wee mbwage tuu ....maana sijaona sehemu yoyote uliyolalamika kuwa wampenda sana.
soma signature yangu
 
naona ile kumuonea huruma ndo kumeniponza na kuniletea hii dhahama

Ndo hivyo sasa huruma yako.kaigeuza jukumu.Mweke chini mwambie hilo sio jukumu lako na kwanzia sasa hutompa pesa unless mwenyewe umeona haja na umetaka mwenyewe kufanya hivyo.Kama hawezani na hayo aende akatafute ATM kwingine.
 

Mimi ni mdada na nimeshajaribu kumuelewesha mara nyingi lakini ni imekuwa mlalamiko na ugomvi tu kwasababu yeye anaona kama ni haki yake mimi kuwa namsaidia kila siku tu
 

Nilishamweleza swala la kutafuta kazi huku akiendelea na masomo anadai eti hawezi kufanya vyote kwa pamoja.
 
Mapenzi ya chuo hayo kwa nini asisubiri amalize shule....sasa out huwa unamtoa ama anakutoa? aisee pole dada yanngu mwanaume kama huyo hata mkioana itakuwa hivyohivyo maana umeishamzoesha na inabidi umtolee mahali kabisa.
 
Hongera zako uliyejaaliwa mapnz hayo,
Achana na ujinga ww unahongaje mwanaume?kwan ww mzazi wake?
Nakushauri acha mara moja huo mchezo,kwa taarifa yako anakupendea hako kamshiko vinginevyo angekuwa na shukran,
Na kwa kulipima penz lake hebu stopisha hiyo huduma japo kwa mwezi utazijua mbichi na mbivu kwenye hao mapenz yenu,
Namwomba mungu aniepushie kuwa na mapnz ya kuhonga wanaume AMEN.
 
Mimi ni mdada na nimeshajaribu kumuelewesha mara nyingi lakini ni imekuwa mlalamiko na ugomvi tu kwasababu yeye anaona kama ni haki yake mimi kuwa namsaidia kila siku tu

kwani wewe ni mzazi wake? au mpenzi wake tu temana nae hana mpango
 
I hope wewe ni she!

Vijana wa siku hizi wamegundua hako kamtindo ka kulelewa, tena akitoka hapo anaenda kuwaambia rafiki zake!
ndio maana nilipoanza kuona anazoea na kamekuwa kamchezo nikaanza kumwelimisha lakini sasa ukimwambia tu ndio ugomvi unaibuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…