Nimechoshwa na huyu mwanaume

Nimechoshwa na huyu mwanaume

Wapendwa, nina mpenzi ambaye simwelewi tabia yake,yeye anataka kila siku mimi nimpe hela pindi anapokuwa na shida, eti kisa mimi nafanya kazi yeye bado anasoma.Na kama ikitokea kakuomba hela afu huna inakuwa ugomvi kwamba simjali najithamini mimi tu.Nimeshajaribu kumweleza kuwa mimi huwa namsaidia kwa kumuonea huruma tu na wala sio jukumu langu na haipaswi yeye kunigeuza mimi ndio mlezi wake ila hailewi.
Asa sijui hata nimwelewesheje? kwasababu jambo hili huzua ugomvi mara kwa mara. Msaada tafadhari
Zabibu haimenywi...
 
Hongera zako uliyejaaliwa mapnz hayo,
Achana na ujinga ww unahongaje mwanaume?kwan ww mzazi wake?
Nakushauri acha mara moja huo mchezo,kwa taarifa yako anakupendea hako kamshiko vinginevyo angekuwa na shukran,
Na kwa kulipima penz lake hebu stopisha hiyo huduma japo kwa mwezi utazijua mbichi na mbivu kwenye hao mapenz yenu,
Namwomba mungu aniepushie kuwa na mapnz ya kuhonga wanaume AMEN.

Mamii sio kwamba mimi namuhonga (kwanza hela yenyewe ya kuhonga mtu niipate wapi mie?)tumekuwa na uhusiano kwa muda mrefu tu na tabia hii haikuwepo ila punde nilipopata kazi mapema mwaka huu ndio akaanza mambo ya kunielezea mtatizo na kuniomba hela na mwanzoni nilikuwa nampa kwa ile huruma tu kwamba mpenzi wangu analalamika hana hela basi tugawane hii niliyokuwa nayo kumbe ile sasa ndio ikageuka tabia.
 
Wapendwa, nina mpenzi ambaye simwelewi tabia yake,yeye anataka kila siku mimi nimpe hela pindi anapokuwa na shida, eti kisa mimi nafanya kazi yeye bado anasoma.Na kama ikitokea kakuomba hela afu huna inakuwa ugomvi kwamba simjali najithamini mimi tu.Nimeshajaribu kumweleza kuwa mimi huwa namsaidia kwa kumuonea huruma tu na wala sio jukumu langu na haipaswi yeye kunigeuza mimi ndio mlezi wake ila hailewi.
Asa sijui hata nimwelewesheje? kwasababu jambo hili huzua ugomvi mara kwa mara. Msaada tafadhari

Zabibu,

Majibu yako hapa
https://www.jamiiforums.com/mahusia...2-tofauti-ya-wanaume-na-wavulana-kitabia.html

Kashakufanya sugarmami wake huyo, tatizo vijana wa kiume wa sikuiz wanapenda sana kulelewa, achana nao, njoo kwa vinega hutopata presha!
 
Jamani Zabibu mimi nilijua unanisaidia kwa roho nyeupe kumbe nina kukwaza, jamani dadazangu si kila siku mnalalamika usawa huu ndio usawa wenyewe, lakini maneno hayo hauzungumzi ukiwa na mimi.
 
Duh, pole mwaya. Hata mimi nlipataga wa hivo, ukimwambia tu hela hamna ananuna, nikaamua kumpotezea tu, akinuna na mimi nanuna, mwsho wa siku kikaeleweka, na hiyo tabia ikafa...
 
Duh shostito huo mzigo mpaka unasema nadhani ushakulemea huuwezi tena ushushe uedele na safari yako huyo gumegume hakufai.
wako tele wasokua na dhiki hizo kwanza wala sio raha mwammme kupewa na mwanamke kila mara loh,anakufanya ATM.
 
ndio maana nilipoanza kuona anazoea na kamekuwa kamchezo nikaanza kumwelimisha lakini sasa ukimwambia tu ndio ugomvi unaibuka

Jaribu siku moja akileta ugomvi baada ya kumwambia fanya kama haujali, akiendelea na ugomvi wake jua anakutumia kama ATM na anafanya kusudi sababu anajua akiletaga ugomvi unarudi chini unampatia fedha.

Tabia mbaya sana hiyo na inafanya vijana wa siku hizi wanakuwa irresponsible kabisa na mbaya zaidi kama alivyosema RR unakuta na yeye anahonga kwa pesa hiyo hiyo na ndio maana ukikataa kumpa anawaka kishenzi sababu kashaombwa vocha huko chuoni na 'mwenzie'

Sio lazima iwe kweli lakini ila changanya akili sasa hivi kabla hajawa mzigo huyo
 
Mamii sio kwamba mimi namuhonga (kwanza hela yenyewe ya kuhonga mtu niipate wapi mie?)tumekuwa na uhusiano kwa muda mrefu tu na tabia hii haikuwepo ila punde nilipopata kazi mapema mwaka huu ndio akaanza mambo ya kunielezea mtatizo na kuniomba hela na mwanzoni nilikuwa nampa kwa ile huruma tu kwamba mpenzi wangu analalamika hana hela basi tugawane hii niliyokuwa nayo kumbe ile sasa ndio ikageuka tabia.
Ok,cha kufanya hapo muite na umwambie ukweli vile unavyojisikia kuhusu tabia yake,
Na wala usiongee ukiwa umenuna,ongeeni ktk hali nzuri tu,na umjulishe huna uwezo tena wa kumgaia hela,
Km anakupenda atakuelewa na mtasaidiana kutafuta kazi kwa ajili yake,
Akinuna na kususa,shukuru mungu na endelea na maisha yako wala usihangaike naye akikua ataacha!!
 
Achana naye huyo tapeli anakufanya ww kama mzaz wake? Wanaume wengine hovyooo
 
Huu mfume dume ndiyo tatizo hapa. Wewe kama unamalengo na huyo kijana ni jukumu lako la kumsaidia kwa sababu ni mume wako wa baadae. au mnabipi? kwa mfume dume huu ni kweli unaweza kujivua majukumu ya kumsaidia huyu bwana mdogo ila kimsingi unatakiwa kumsaidia kama madai yake ni ya kweli ya uhitaji wa fedha. Ila huyu bwana mdogo ana tatizo moja ambalo naliona ni la msingi sana, kuwa mgomvi unapomwambia huna pesa. UWE MACHO HAPO, kuna uwezekana huyu bwana mdogo hakupendi na amekufanya wewe DECI anavuna asipopanda! Kwa mfume dume, pesa za mwanamke ni zake ila za mwanaume ni zenu wote, ndiyo mana watu wanamponda huyu dogo.
 
Anaanza ugomvi na wewe bado unampenda ahaaaa aaaa.

ndio maana nilipoanza kuona anazoea na kamekuwa kamchezo nikaanza kumwelimisha lakini sasa ukimwambia tu ndio ugomvi unaibuka
 
Jamani Zabibu mimi nilijua unanisaidia kwa roho nyeupe kumbe nina kukwaza, jamani dadazangu si kila siku mnalalamika usawa huu ndio usawa wenyewe, lakini maneno hayo hauzungumzi ukiwa na mimi.

Kila siku nikusaidia nikikwambia tu sina hela unaleta ugomvi unalalamika kama nini wakati kweli nakuwaga sina hela...sikupi hela tena, mwanzo mwisho
 
Asanteni wote mliochangia kunishauri, naanza kuufanyia kazi leo hii hii ili nione ufumbuzi wa hili tatizo
 
Wapendwa, nina mpenzi ambaye simwelewi tabia yake,yeye anataka kila siku mimi nimpe hela pindi anapokuwa na shida, eti kisa mimi nafanya kazi yeye bado anasoma.Na kama ikitokea kakuomba hela afu huna inakuwa ugomvi kwamba simjali najithamini mimi tu.Nimeshajaribu kumweleza kuwa mimi huwa namsaidia kwa kumuonea huruma tu na wala sio jukumu langu na haipaswi yeye kunigeuza mimi ndio mlezi wake ila hailewi.
Asa sijui hata nimwelewesheje? kwasababu jambo hili huzua ugomvi mara kwa mara. Msaada tafadhari
"ukitaka kula kubali uliwe"- JK
 
Mamii sio kwamba mimi namuhonga (kwanza hela yenyewe ya kuhonga mtu niipate wapi mie?)tumekuwa na uhusiano kwa muda mrefu tu na tabia hii haikuwepo ila punde nilipopata kazi mapema mwaka huu ndio akaanza mambo ya kunielezea mtatizo na kuniomba hela na mwanzoni nilikuwa nampa kwa ile huruma tu kwamba mpenzi wangu analalamika hana hela basi tugawane hii niliyokuwa nayo kumbe ile sasa ndio ikageuka tabia.
nina smell opportunity...zabibu ni pm please faster,usiache kunidondoshea kanamba ka simu mwe
 
Back
Top Bottom