Nimechoshwa na tabia za mume wangu na dada yake nisaidieni nifanye nini?

Nimechoshwa na tabia za mume wangu na dada yake nisaidieni nifanye nini?

Mwanzoni wakati wamekuja hawa ndugu zake tulikuwa tunaishi chumba na sebule hivyo dada ake alikuwa analala sebleni

chai.jpg
 
Habari za saa hizi ndugu zangu Mimi ni mgenii humu jamii forum na nimejiunga Ili nitoe ya moyoni na mnisaidie maamuzi kwenye jambo linalonitatiza sana,
Nimeishi na mume wangu kama mwaka mmoja na nusu kisha 2022 akaja dada yake mkubwa ambaye wamezaliwa mama mmoja baba tofauti lakini mama yao amefariki alikuja kukaa na sisi akiwa na mtoto wake ambaye Sasa anamiaka tisa, tulimpokea na kuishi kwa amani tu tangu alipofika kuna baadhi ya maneno aliyokuwa akiongea yalinishangaza hadithi alizoniaimulia pamoja na matendo anayoyafanya.
Kwanza alipofika tu na kuona tunavoishi alikuwa akiniambia kuwa kama mama yao angekuwepo huyo ndugu yake mtu wa kwanza kwake ambaye angekuwa anampa kipaumbele ni mama yake na siyo Mimi, pia alinisimulia kuwa ndugu zake wa kiume yaani binamu zao wote walikuwa wakimtaka kimapenzi na kuna baadhi aliwahi kulala nao.
Pia alinisimulia mambo mengi hata yanayoingiliana na mume wangu kwamba yeye huwa alikuwa anamfulia hadi boxer mume wangu maana wameishi nyumba moja Hadi mume wangu akiwa chuo, mara aseme yeye anamjua zaidi maana ni dada yake mara aseme mume wangu huwa alikuwa akimuwekea vidole mdomoni amnyonye (na hichi kitu huwa huyu Mwanaume ananifanyia na Mimi pia kama sehemu ya kufurahia tendo la ndoa ananiwekea kidole chake mdomoni) Sasa nilishtuka kwanini alikuwa anamuwekea dada yake pia.

Nikajipa moyo lakini alikuwa Kila siku mwanaume akirudi kutoka kazini anaanza kujifanya anaumwa hatakama mchana kashinda mzima anajilegeza anatia huruma kama anaumwa nikaacha sikuongea kitu.
Akaanzisha utaratibu akivaa nguo sanasana anashindia vijora au tshirts na khanga Sasa anavaa bila chupi wala brazia kaka yake akija anaanza kuinama mbele ya kaka yake atatafuta sababu yoyote ile ainame I name pale sebleni , kiukweli hii huwa inanikera na kuniumiza sana.

Kaka yake akiwa hayupo hata akivaa nini hainami hivyo wala hajipitishi lkn akirudi tu kutoka kazini anaanza atakaa jikoni atafanya vitu akiwa Dera au kijora hajakishikilia akitaka tu kwenda sebleni ambapo kaka ake amekaa anaangalia tv anaanza kukishikilia kufanya matako yake yaonekane vizuri mda huo kumbuka hajavaa chupi yoyote, nilimuuliza kwanini huvai chupi akasema amezoea tu,
Kingine sasahivi ameanzisha tabia ya kukohoa mume akirudi kutoka kazini tu anaanza kukohoa na kujifanya dhaifu hatakama mchana kutwa kashinda hakohoi ataingia chumbani kwake ataanza kukohoa kwa sauti hata kama umekaa na mume sebleni hamuongei kwa amani anavuta attention ya huyo kaka ake iwe kwake.

Kiukweli sipendi tabia zake na mbaya zaidi huwa akiwa anajitegesha mume wangu huwa anamuangalia na kuna vitu ambavyo siyo vya kawaida naviona kuna siku yalinishinda nikamwambia mwanaume kwanini unamuangalia dada yako makalio akiwa ameinama hvo , nilimwambia chumbani Ili tuongee kwa Siri ajirekebishe lkn akamuita dada yake aka mwambia halafu wakanigeuka huku akinigombeza sana alisema huyo ni dada yake tumbo moja hawezi kufanya kitu kama hicho.

Lakini kesho tu wakaendelea na huo mchezo wa kutegana. Mwanzoni wakati wamekuja hawa ndugu zake tulikuwa tunaishi chumba na sebule hivyo dada ake alikuwa analala sebleni na mtoto wake lakini mwanaume alikuwa anakaa sebleni Hadi saa 7 usiku eti anaangalia movie dada yake akiwa kajilaza hapo chini huku anabinua vikalio , halafu sebule ilikuwa ni ndogo kwahyo mume wangu analala kochi kubwa hafu chini yake pembeni ndo amelala dada Yake na kuna siku nilifungua mlango kwa kushtukiza nikakuta mkono wa mume wangu upo chini pale kwa dada yake wanajifanya tu wanacheka wanaangalia movie ila sikupenda, nashukuru tukahama pale kwahyo baadhi ya mambo kama hayo ya kuonwa Kila siku akiwa amelala yakaisha.

Kuna siku asubuhi nilikuwa natoka namfata mwanaume nje alikuwa anaenda kazini dada yake akaanza kuniambia kwanini humjibu mtoto wangu amekusalimia shkamoo, kiukweli sikuskia hyo salamu ila akaaanza kuniongelesha kwa kiburi anasema kwanini humjibu Hadi mwanaume akaingia akasema mbona Mimi nilikuwa hapa mlangoni Ila sijasikia hiyo salamu nikapotezea lkn.

Kiufupi nimemchoka sana tabia zake za kujitegesha , na pia huwa ananiambiaga yeye anaishi na mtu kama mtu anavyotaka kuishi nae kwamba kwakuwa Mimi nakaa kwa upole ndomaana sioni ukorofi wake lkn yeye hamuogopi mtu na siku mtu akimtibua ndo atamjua vizuri najua kabisa hapa ananiongelea Mimi.

Sisemi uongo jamani nimeishi nao vizuri kwasababu pia Mimi sipendi magomvi na sipendi mifarakano alikuja akiwa na tension kubwa lkn Hadi sasahivi anakaa tu kama rafiki yangu ila tabia ambayo Bado anayo na inaniuzi ni hyo ya kwamba mwanaume wangu akija nayeye anajiona ni mke anaanza kumtega lazma Kila siku ajioneshe mwili wake Ili mdogo wake amuone ninajiskia vibaya sana rohoni.
Mwanzoni wakati wanakuja kaka yake( lkn mume wangu ni mdogo kwake kiumri kama miaka mitatu au minne) alimwambia hapa hatuna sehem ya kulala nyingine lkn dada mtu akaanza kumwambia unaona huyo mwanamke unaeishi nae ndo Bora zaidi kuliko dada yako wa damu kiukweli sikufurahishwa na hyo tabia, pia walikuwa wametoka sehemu ambayo ni nyumba kubwa tu na wanacho chumba Cha kulala lkn mama yao mkubwa waliekuwa wanakaa nae alimwambia aje akae huku kama anaweza kukaa na mwanamke ambaye syo ndugu yake anaweza kumhudumia ndugu zake , akamwambia wewe nenda hatakama wakikulaza chooni lala ilimradi banana Hadi kieleweke.

Pia mwanzoni kati anakuja alikuwa anatumia nguvu kubwa kuniringishia mtoto wake maana Mimi sija jaaliwa mtoto Hadi sasahivi, hivyo anatumia hyo kama nafasi ya kuonesha kuwa Sina mtoto alikua anafanyaambo mengi yanayonikwaza lkn siwezi kuyaeleza yote na siwezi kumwambia mtu akanielewa mpaka awe anaishi hapo na sisi na anaona Kila kitu jamani nishaurini nifanye nini najiskia kuumia na kuchoka sana tabia hizi za huyu wifi yangu sana na mume wangu haoni tatizo Kila dada yake akifanya mambo kwa vitendo yakujipitisha halafu kaka yake anaangalia nikijiskia vibaya nikanuna kaka ake anasema Mimi Nina roho mbaya watu wana amani lkn Mimi naroho mbaya nisaidieni.
....akamwambia wewe nenda hatakama wakikulaza chooni lala ilimradi banana Hadi kieleweke....🤔🤔🥺🥺🥺.
Hao ni wapenzi na wameshawahi kulalana na wanapendana... Mapenzi ya ndugu ni hatari sana wanaweza kukutoa ndani ya nyumba usipokuwa makini
 
Dunia sasa imeharibika pakubwa sana, hofu na mashaka sio yakupuuzia hata kidogo, huwenda unalohisi kweli lipo. Chakufanya kaa na mume wako muweke mipango kistarabu tu ikiwezekana mumpe hela kidogo akapange chumba, au mshauri nume wako amwambie dadaake arudi alikotoka, na sio kukaa nae hapo.
 
Una tatizo la wivu uliopitiliza, hao watu wangetaka kulombana wasingefanya mbele yako, punguza wi

Weka camera kisha wape nafasi tafuta safari ya kama siku tatu. Ukirudi utajua mbivu na mbichi..!!
Kuna siku niliondoka kusalimia kwetu siku kama nne nilivorudi nilikuta wifi kafua nguo zote za mume wangu Hadi boxer zake kazianika kwenye kamba nilivomuuliza mwanaume akasema nilitaka afue nani kati dada yake yupo
 
Whether ni chai ama lah !!!! Una inferiority complex, huenda huyo wifi ako ni mtu poa tu !!! Kutokuwa na mtoto pia kumekuumiza kiasaikolojia,,, Pole, omba Mungu !
 
Ndyo alimwambia hvo na mume wangu akijua waliyo yaongea lkn hakuna shida alisema tu anamhurumia dada yake
....akamwambia wewe nenda hatakama wakikulaza chooni lala ilimradi banana Hadi kieleweke....🤔🤔🥺🥺🥺.
Hao ni wapenzi na wameshawahi kulalana
 
Back
Top Bottom