Nimechoshwa na tabia za mume wangu na dada yake nisaidieni nifanye nini?

v
Mwanamke mwenye na mtoto anakuja nyumbani kwako, unawalea kisa dasa yako, baba yake mzazi yuko wapi? Na baba wa mtoto yuko wapi?

Kumlea dada yake naweza kufikiria, ila sasa kumlea na mtoto wake ...hilo jamaa kubwa jinga
vp kama ye ndo baba wa mtoto,...
 
Umeulizwa kabila la hao watu

Kwa ile kauli ya nenda ukabanane, hata kama ni chooni lala, lazima kieleweke. HAPO KUNA JAMBO

1. Hao ni wapenzi
2. Mtoto ni wake

Yanawezekana.

Ushauri.
Muulize mume wako. Hao watu wanakuwepo hapo mpaka lini?
 
Umeandika kwa uchungu sana.
Huo mtego ni mgumu. Mungu akusaidie kikwazo hicho kisikuangushe.
 
Waaoo mgeni wa Jf.

Thread yako nimeisoma kwa umakini mkubwa na kuielewa.

Wewe upo katika sonona iliyosababishwa na tabia za umalaya za mmeo.

Huyo wifi yako kwa maelezo yako ni mke mwenza pia kutokana na ushahidi wa mazingira.

Hukumu hii naitoa kutokana na maelezo yako.

Huyo wifi yako nina wasiwasi kuhusu huyo mwanaye, yaweza kuwa alizaa na kaka yake huyo mmeo, kama sivyo basi watakuwa na historia chafu ya kimahusiano huko nyuma tangia utoto wao.

Cha kufanya:
Ninajua mmeo yupo upande wa hawara yake na anakukandamiza wewe.

Fikiria vizuri mahali unapoweza kulipeleka jambo hili ukaweza kusikilizwa kwa haki bila upendeleo ndiyo ulipeleke huko.

Kama mlifunga ndoa za kidini, basi huko huko, kama kuna wazazi wake wenye busara, basi huko huko, kama kuna mshenga wake mwene busara, huko huko ilimradi jambo hili litafutiwe ufumbuzi na watu wenye busara litapata muafaka.

Nionavyo mimi, huyo wifi yako akiendelea kuishi hapo, future ya ndoa yenu huko mbeleni ni giza totoro hamtoboi.

Kwani ni lazima aishi hapo mbanane?

Si aende akaishi maisha yake akapange ama akaishi kwa wazazi wengine ama ndugu wengine huko, ni lazima aishi kwenu tu?

Akiendelea kukaa hapo ndoa yenu haipo.

Ukifika katika vikao vya usuluhishi usije ukaficha neno lolote, pia weka msimamo wako kuwa haumchukii, lakini kwa viashiria vya hatari ulivyoviona aende akaishi kwa ndugu wengine ama akapange ni mtu mzima yule.

Ukiona mumeo anapingana na msimamo wako, elewa kuwa huyo siyo wifi, ni mke mwenza uliletewa kijanja, bila kujali ni dada yake ama nani yake, hapo uamzi utakuwa kichwani kwako.
 
Mie ningeondoka nimuache na Dada yake au ningetoa sura ya upole nikiwa she mpaka aondoke.
 
Ugonjwa ulionao ni ugonjwa mlionao wanawake wembamba wote huwa mnawivu sana na wanawake wenzenu waliojaaliwa , ukijiangalia umenyooka kama fagio ya buibui unaanza kuhisi kila mwanamke mwenye mzigo akiongea na mumeo basi wanakulana au mkitembea barabarani akakatiza mwanamke aliefungasha mumeo akageuka kuangalia gari ili avuke barabara we unahisi kamuangalia huyo mwanamke.

Kama ni Dada yake tumbo moja tulia , ila kama ni binamu yake hapo fresh kaa kwa password, mabinamu wanaliwa kimasihara.
 
Mimi siyo mwembamba ni mnene na ki umbo ninalo kubwa kuliko huyu wifi yangu , ila tabia tu ndo huwa zinaniumiza
 
Mumeo ni mchagga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…