Nimechoshwa na tabia za mume wangu na dada yake nisaidieni nifanye nini?

Niseme tu wanawake mnamatatizo hamwezi kaa sehem mmja ndo mlivyo umbwa.

"Shangazi zangu walishawahi kupigana sababu mwingine anajifanya anajua kuunga mboga"
Kwa hiyo wewe mwanaume unaweza kuishi na kidume mwenzako ndani ya nyumba kisa eti ni ndugu wa mkeo na anatembea na boxer ndani mbele ya mkeo kisa ni dada na kaka?
 
Hana Sonoma, ana stress tu.
Lakini nafikiri kwa hali ilivyo kumpeleka mime sijui kwa wazazi au mshenga inaweza kupelekea kujiaibisha zaidi kwa huyu mtoa mada,
Maana itambidi Kuanika siri za ndani na bado wakaishia kuwa upande wa mume wakamuambia kuwa anajishtukia tu kwa sababu hajawahi KUWAFUMANIA
Cha msingi hapo ni kumuambia mume achague moja, mke au huyo "dada"
 
Ok, tuchukulie ni dada yake kweli na hawakulani, kwa akili yako unaona ni sawa mwanamke aje kuishi kwa ndugu tena na mtoto kwenye nyumba ya kupanga? Huoni tu hapo hata kama hawana uhusiano ni mzigo mkubwa tena inawaondolea faragha?
Ni akili za wapi hizi...
 
Yaan jaman jaman kama ndugu zangu hawajawah kuja kukaa kwangu basi na ndugu wa mume wasikanyage kama mume anaona dada yake ni wathaman bas akampangie chumba akiona haitoshi basi ahamie na yeye huko tumeona wawili hao ndugu wanaokuja kujazana ndan kwetu sababu ni zipi
Mnaosema wivu sijui vitu gan achen unafki je kama angekua ni kaka wa mke anafanya Ivo Kwa dada yake ingekua ni sawa?
 
Dada yangu wala usiteseke, Ulitakiwa haya unieleze mapema mimi kaka yako yangeshaisha. Usihofu next week namimi nakuja kukaa kwako, Sasa itakuwa kaka na dada (Shemeji na Wifi ) nitakusaidia kumuweka sawa huyo wifi yako.


Hio imeenda na limekwisha.
 
Wazo zuri sana. Vinginevyo akivumilia, huyo dada kaja kuolewa.
 
Una tatizo la wivu uliopitiliza, hao watu wangetaka kulombana wasingefanya mbele yako, punguza wivu.
Huyu shida yake ni wivu na kutokujiamini kwakuwa hajamzalia mtoto mumewe anahisi kila mwanamke atampora mume. Huyu bibie anatakiwa kujiamini, kwa tension hizo anaweza hata asipate mimba. Anatakiwa kutulia na yeye amuonyeshe anavyomshika kakake. 😛
 
Ni kweli nakosa uhuru nakuwa hata nikiwaza kuwa busy sana naogopa huyu atamchukua kabisa mume wangu, pia hata kusafiri mbali naogopa pia kuwaacha hapa wenyewe Yani najiskia vibaya
Kwa dunia ya leo hiki ulichokisema kinaweza kutokea maana kaka na dada kulana ni kawaida aise.

Watu hawana hofu kabisa kwahiyo kuwa makini na hao watu.
 
Ni kweli nakosa uhuru nakuwa hata nikiwaza kuwa busy sana naogopa huyu atamchukua kabisa mume wangu, pia hata kusafiri mbali naogopa pia kuwaacha hapa wenyewe Yani najiskia vibaya
Heheheeee...inamaana ndio tunaogopa kuwapoteza wanaume kiasi hiki yaani tunapigwa matukio tupo tu.Hata kusafiri mbali unaogopa.Ndoa ni ngumu jaman.Woooi tutaponea wapi
 
Ingawa sikuweza kuisoma story yote,nakushauri fanya kila namna huyo wifi yako feki,haondoke haraka sana humo ndani.
 
Mbona mume nae ndio tatizo kubwa zaidi pengine.. Maana ameeleza aliwahi kumuita pembeni na kumuuliza, mwanaume akamuita Hugo anayeitwa Dada na kummwambia mke wangu anakusema hivi na hivi
Ndo maana nikasema dunia ya sasa iko hovyo sana ,yawezekana wote ni changamoto , hata kaka na dada bado walipaswa kuweka mipaka, yaani kwanini dada aseti t#ko kabla ya kwenda sebleni alipokuwepo kaka, alafu kwanini kaka asikemee vijitabia vya hovyo vya dada yake,na kwanini amkazie macho dadaake kwa nyuma
 
Heheheeee...inamaana ndio tunaogopa kuwapoteza wanaume kiasi hiki yaani tunapigwa matukio tupo tu.Hata kusafiri mbali unaogopa.Ndoa ni ngumu jaman.Woooi tutaponea wapi
kupungua kwa idadi ya wanaume na kuongezeka kwa wanawake ni miongoni mwa dalili za Kiyama (Siku ya Mwisho) zilizoelezwa katika Hadith sahihi za Mtume Muhammad ﷺ.

🔹 Dalili hii imo wapi?

Dalili hii inapatikana katika Hadith sahihi zilizopokelewa na Imam al-Bukhari na Muslim.

🔸 Hadith sahihi:

Mtume ﷺ alisema:

"Miongoni mwa alama za Saa (Kiyama) ni kwamba idadi ya wanawake itaongezeka, na idadi ya wanaume itapungua kiasi kwamba kutakuwa na mwanamume mmoja kwa wanawake hamsini."



📚 (Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim)


---

🔹 Maana ya Hadith hii:

Hadith hii inaonyesha kuwa zipo nyakati kabla ya Kiyama ambapo kutatokea upungufu mkubwa wa wanaume na ongezeko kubwa la wanawake.

Sababu za kupungua kwa wanaume hazikutajwa moja kwa moja, lakini maulamaa wamefafanua kuwa inaweza kuwa kutokana na:

Vita vingi,

Magonjwa ya kutisha,

Mifadhaiko au matatizo ya kijamii kama ugumba(infertility) masuala ya kiuchumi,
Vifo vya ghafla (kama zilivyo dalili nyingine za Kiyama).




---

🔹 Maoni ya Maulamaa wa Kisunna:

Wanazuoni wa Kisunni (Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah) wanakubaliana kuwa:

Hadith hii ni sahihi,

Inahusu alama za Kiyama ndogo (minor signs),

NAKUSUDIA HIVI
Linda ndoa yako dada, waoaji wanazidi kupungua kila kukicha, usikubali kabisaaa, yawezekana huyo dada ametafuta wakumuoa kakosa kaamua kumtamani hata kaka yake ,ni hitaji la mwili limemtuma hivyo,kwani kuna kesi ngapi za kaka na dada wakifanya yao
 
Dah🙌...Asante
 
Kwa hiyo wewe mwanaume unaweza kuishi na kidume mwenzako ndani ya nyumba kisa eti ni ndugu wa mkeo na anatembea na boxer ndani mbele ya mkeo kisa ni dada na kaka?
Wanaume anauwezo wa kutongoza demu wa mtu na akanyamaza mwanamke akiwa na mwanaume wa mtu lazima atafanya kivyovyote mke wako ajue baadh lkin mtanielewa
 
Mke mwenzio huyo
 
Embu weka kwanza picha ya huyo wifi Yako akiwa kavaa hicho kijora au kanga na tisheti nikupe ushauri utakaobadilisha Maisha Yako ya ndoa
 
Wambulu hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…