Nimechukia sana suala la Dokii kusaini Timamu African Media

Nimechukia sana suala la Dokii kusaini Timamu African Media

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Kiukweli mimi ni shabiki wa damu wa dokii tangu enzi na enzi ,ila kwa hili la sasa la kusaini kwa hawa watafuta kiki (Timamu Comedians ) aisee nimemshusha vyeo sana

Dokii ana jina kubwa sana so alipoenda kujiunga na hivi vitoto amejishusha hadhi sana ,maana kwa pale Star wao ni Ebitoke hao wengine wanaonekana si lolote wala si chochote na ndio maana wakaanzisha hiyo " Ebitoke in da house"

Dokii alifiti sana kipindi kile ana igiza zile muvi na wale wabongo wanaoishi South Africa

Walitoa muvi nyingi sana na kila muvi ilibamba ile mbaya na ilikuwa haichoshi kutazama ,kama ile ya " Money Transfer" na nyinginezo

So kama shabiki ninavyoona afanye juu chini ajitoe kwenye hilo kundi halitampeleka kokote zaidi na zaidi hao vijana watatumia jina lake ili wajitangaze na yeye hatopiga hatua yoyote ile
 
Screenshot_2017-06-25-00-22-07_1.jpg
 
Pole mkuu kwa kuchukia, ndio kashaamua sasa tena kwa usawa huu ulivyo mgumu
Amepodoa kichizi yaani

Hakupaswa kabisa kujishusha hivyo

Maana lile ni kundi kwa vijana wachanga wanaotafuta channels za kutoka sasa na yeye kwenda kujibana hapo hapo ,aaaargh amepodoa sana yaani.
 
hamna nadhani italisaidia kundi swala hapo ni maslahi
Dokii anakuwa.kama staa ambaye ataenda kuamsha kundi zaid.
halaf kwa usawa huu mtu akipata kazi yoyote ianyo muongezea hata buku yafaa afanye.
mi nao ni kama wote wawili watafaidika Dokii atarud kuonekana zaid kwenye tasnia yake na hao madogo watapata kufahamika zaid na kujenga majina
 
Ila ninavyoona hawampi heshima yake ipasavyo wanamchukulia kama underground mwenzao
 
Mosi, Timamu sio kundi bali Production Company! Kundi ni kama vile Kaole.

Now, kama Timamu hapana hadhi yake, unadhani angekuwa wapi?!
 
Unataka usainiwe wewe siyo mtoto wa kiume mambo ya kike kike tu
 
Mambo ya kike hayo..ww ulitaka asaini wapi
 
NI SAWA AKISAINIWA TU...MAANA ALICHEZEA UJANA...KWAHIYO VIJANA SASA WATAMRUDISHA KWENYE RAMANI...NA NDIO VIJANA WANAKUJA VIZURI

HALAFU DOKII BINAFSI SIMFEEL ANA MARINGO SANA HAJUI KUISHI NA MASHABIKI WANAOMUWEKA KWENYE CHATI...KUNA MWAKA NILIKUTANA NAYE DODOMA WAKATI HUO ANA HEKAHEKA ZA CCM...TUKAWA TUMEPIGANA KIKUMBO KWENYE VIUNGA VYA MJI..NIKAMSIMAMISHA NA KUMSABAHI...KWA FURAHA KAMA MUIGIZAJI MASHUHURI..LAKINI NILIISHIWA KUPUUZWA NA AKANIPITA ..NKASHANGAA SANA HAWA WASANII WA NCHI ZETU ZINAZOENDELEA WANA MDUDU GANI KICHWANI...KWAHIYO NADHANI MAISHA YAMEMNYOOSHA VIZURI..SASA HIVI SI HAMNA TENA CCM MAMBO YAKUBEBANA..CHEZEA JPM
 
hamna nadhani italisaidia kundi swala hapo ni maslahi
Dokii anakuwa.kama staa ambaye ataenda kuamsha kundi zaid.
halaf kwa usawa huu mtu akipata kazi yoyote ianyo muongezea hata buku yafaa afanye.
mi nao ni kama wote wawili watafaidika Dokii atarud kuonekana zaid kwenye tasnia yake na hao madogo watapata kufahamika zaid na kujenga majina
Upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom