Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

nyakandula

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
1,250
Reaction score
1,727
Habari zenu

Nimekopa shilingi milion 30 bank CRDB. Nahitaji kununua gari mojawapo katika hizi IST, ALEX, RACTIS, CARINA na pesa itayobaki nikamalizie mjengo wangu chanika (15MIL) na ibaki pesa kidogo ya kula bata. Je, mpango wangu unafaa?

Naomba ushauri wadau

NB: Nimechagua hizo gari kwa ajili ya matumizi madogo ya "wese"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushakopa, so wakikwambia umekosea sio haki, haiwahusu, kabla ya kununua gari hakikisha nyumba inaisha vizuri, IST mpya kabisa si mbaya, ni gari nzuri sana.....ila ujawaza hata balance inayobaki uweke genge la chips au chochote mahali kiingize hela kidogo?
 
Ni kweli mkuu.
Utakuta hapo mshahara wake laki 6 take home.
Akikatwa mkopo wa benki ibaki laki 3.5.
Halaf hyo hyo alishe familia na nyingine anunue mafuta ya gari.
Wakati huo hapo gari ni mpya then baada ya mwaka gari ikianza kuchoka ataanza kununua spea.
Hivi ndio umaskini hukaribishwa kwenye familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu
IST mpya kabisa hataipata kwa 15m. Ila atapata IST nzuri showroom.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anzisha kiwanda kidogo, revenue itakayozalishwa malizia nyumba, gari usinunue labda baadae pick up ya kusaidia kiwanda na shughuli zingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio mim mtumishi ila sitegemei kazi kuendesha maisha nina baadhi ya vtega uchumi napia sina familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina vitega uchumi kadhaa ambavyo vinasaidia mwisho wa mwez sigusi mshahara wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina familia inayonitegemea napia nina kitega uchumi kinachonipa pesa ukiachana na mshahara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…