Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Habar zenu, nimekopa milion 30 bank CRDB, nahitaji kununua gari mojawapo katika hizi IST, ALEX, RACTIS, CARINA na pesa itayobaki nikamalizie mjengo wangu chanika (15MIL) na ibaki pesa kidogo ya kula bata .nipen ushauri wadau
Nb:nimechagua hizo gari kwa ajili ya matumizi madogo ya wese

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilidhani unauza figo bandama na mapafu jamaa yangu ataitaji figo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kununua gari ya matumizi binafsi tena kwa mkopo sio wazo zuri...ni uzwazwa daraja la kwanza.

Tumia hela hiyo kuwekeza kwenye miradi midogo ya aina mbili au tatu tofauti....faida yake itumie kulipa marejesho ya bank na kuwekeza zaidi. Baada ya muda tumia kiwango fulani cha faida kumalizia mjengo wako..

Be smart...wewe ni fukara...you cant afford to own a car at this juncture.
 
Bwana mdogo,..mil30 ni hela ndoogo sana ukiishika amini nakwambia,na sikushaur ufanyie biashara hyo hela sabab kwa ulivyo ulivyo tuu nmeona hutoweza,tuanzie hapo kwanza,so hako ka 30 kama ulivosema unataka gar na kumalizia nyumba na hela ya bata,..naona umejitoa muhanga,first of all ushafel so ngoja nikushaur kutoka kwenye hyo failure,..

Subir had december kuna yard nying tu hua wana ofa,mfano pale namanga ile yard ya wa pakistan,acha mbwebwe za IST ziko juu sana mpya,na usinunue gar mkonon,utakuja juta,..nenda pale yard tafta ractis or fun cargo or gar yoyote utakayokuta ,hua ofa znafika had 7.5m..kwa sis wateja wa kudum hua tunapigiwa sim kabsa,kuna gar hii na hii zna ofa..usinunue zaid gar zaid ya m9..then hela inayobak malizia tuu nyumba hyo,namaanisha hela yoteee,usiweke hela ya bata sabab bata hyo na wenge la hela,utapata majanga,ajali,kuibiwa,etc utarud nyuma utatumia hela zilizobak kujiuguza,so hela yote malizia ujenz,tenga 15mil,tafta fund ,tumia budget ndogo uwezavyo,..vifaa vyote nenda dukan usitume mtu..mil6 iliyobak weka bank ipige fixed,huku ukitafta kamrad kakukuingiza sh mbil tatu


Nmeshaur kutokana na experience

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu.
Utakuta hapo mshahara wake laki 6 take home.
Akikatwa mkopo wa benki ibaki laki 3.5.
Halaf hyo hyo alishe familia na nyingine anunue mafuta ya gari.
Wakati huo hapo gari ni mpya then baada ya mwaka gari ikianza kuchoka ataanza kununua spea.
Hivi ndio umaskini hukaribishwa kwenye familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kuwa na mshahara wa 600k take home alafu upewe mkopo wa 30mil. Atakuwa ana mshahara mzuri tu kwa mkopo huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachukuwa mkopo alafu una nunua gari na kujenga nyumba huu ndo ulimbukeni hasa.Alafu baada ya muda munaanza kulalama kuwa serikali haitoi nyongeza za mishahara wakati mnayopata mnashindwa kuitumia vizuri.
Ushauri wangu.Ni huu chukua hiyo pesa alafu wekeza kwenye mradi/biashara inayoendana na wakati ulipo au kama hauna uzoefu basi nunua hisa katika kampuni na hati fungani baada ya muda utavuna matunda and then hiyo returns unaweza kununua gari na kujenga kibanda chako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyakandula hongera kwa chaguzi ulizonazo,kamata IST(kama ulivyosema kusave cost ya mafuta) and the rest money endelea na mchakato wa kumalizia mjengo_
Tatizo watu hupenda kuingilia chaguzi za watu,kila mtu anachoice zake*(afanye nn kwa wakati gani)_mara 30M pesa ndogo,wekeza kwanza iyo pesa,fungua kiwanda(we unaelewaje kama mtu hana hivyo vitu,kama hajawekeza...)_
Watu wa aina hii ndo wale wanaotafuta pesa za mitaji hawapati,mawazo wanayo kibao ya kuanzisha miradi_mwisho wa siku wanakuja kuleta mawazo yao kwa kutojua mtu umejipangaje mpaka kufikia maamuzi hayo ulochukua_

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom