Nimedhulumiwa/ kutapeliwa na tajiri na sioni pa kumpeleka

Nimedhulumiwa/ kutapeliwa na tajiri na sioni pa kumpeleka

ndenjii handsome

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2021
Posts
647
Reaction score
706
Husika na mada hapo juu,

Katika harakati za utafutaji nikajikuta nimeuvaa umilionea wa ghafla msishangae jamani mambo ya machimbo, basi nilivyoipata hela nikakimbilia kununua malori ya mizigo aina ya Volvo kama sita hivi nikiwa mchanga kwenye ishu za magari.

Mungu sio John nikapata tenda kwenye kampuni fulani hivi ya kubeba makaa ya mawe ila sikutimiza vigezo maana hiyo kampuni ilikuwa ikiitaji mtu mwenye lori kuanzia kumi basi akatokea tajiri mmoja akaniambia tuingie share kwa sharti yeye awepo muhusika mkuu.

Sikuwa na pingamizi nikamkubalia kwa maana yeye alikuwa ana lori nyingi basi zikaanza kazi mwezi ukapita nikapata gawio langu ila tokea nimepata hiyo pesa sijapata tena na lori zangu zilifanyiwa kazi ndani ya miezi zaidi ya tano mpaka nilipoamua kuzisitisha na kila nikidai malipo yangu natishiwa nitawekwa pabaya na nikashitaki popote mpaka nimekata tamaa na kujilaumu kwanini nimenunua hizi gari hata bora hela yangu ningefanya starehe.

Wakuu msaada wa mawazo yenu hatua gani nichukua.

Asanteni
 
Kwanza kama mlisaini contract wala sio issue kubwa ,tayar apo unapakuanzia. Kusanya evidence zako km vile weigh bridge receipts za kiwandan kila mnapo offload mzgo then mshtaki tu.

We mkomalie tu hayo mambo mengine anakutisha. Halafu mbona kazi ziko nyingi mkuu yanin uhangaike na watu wasiolipa? Km gari hazina kazi, nichek nikupe mchongo.
 
Huna mkataba, mambo ya kufanya kienyeji! Imekula kwako hiyo, pole.

Ni kweli huna pakumpeleka.

Utafilisika, umeishajifunza, songa!

Usilogwe sijui wanasheria nini, wapigaji

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Pole sana,nakusikitikia sababu rais wa wanyonge nae kashakufa...hapo mkuu ni vita tu, tafuta boss mwingine wapambanishe ww ukae kati tu.
 
Back
Top Bottom