Nimedokezwa na mtu kuwa wapo wengi tu watajiunga NCCR Mageuzi

Nimedokezwa na mtu kuwa wapo wengi tu watajiunga NCCR Mageuzi

Kwani watakua wamevunja sheria? Sasa shida iko wapi mtu akiexercise haki yake kikatiba?
 
Inauma Sana kwa yeyote anayependa haki kuona mnayowafanyia chadema inauma mno naamini hata polisi na VYOMBO VYA dola havipendi mnayoyafanya CCM ila hawana namna ila naamini ipo siku hii Hali itafikia mwisho nothing will prevail to eternity.
 
Natamani 2025 ccm ishinde kwa 100%
Ichukue viti vyote vya ubunge + madiwani
Ili baadae tujifunze faida ya kuwa na upinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa % wanayoshinda bado maamuzi yote hufanywa na CCM. Plus rais ana mamlaka makubwa kuliko hilo bunge na officials wengine combined
 
Sio wasaliti tunamuunga mkono JPM amefanya makubwa kwa muda mfupi sana.
Yapi kwa mfano! Usinitajie Barabara, reli Wala bwawa la kufugia kambale Wala zahanati na shule kwani hizo ni huduma zinazotakiwa kutolewa kutokana na Kodi yangu!
Ukinitajia makubwa aliyoyafanya usisahau kuniwekea kuua upinzani (utadhani upinzani ni paka mwizi japo haujafa), kushamiri kwa rushwa Tena zile grand, kuiparanganya nchi kidini na kikabila, dharau na kupima mapapai!
 
Yapi kwa mfano! Usinitajie Barabara, reli Wala bwawa la kufugia kambale Wala zahanati na shule kwani hizo ni huduma zinazotakiwa kutolewa kutokana na Kodi yangu!
Ukinitajia makubwa aliyoyafanya usisahau kuniwekea kuua upinzani (utadhani upinzani ni paka mwizi japo haujafa), kushamiri kwa rushwa Tena zile grand, kuiparanganya nchi kidini na kikabila, dharau na kupima mapapai!
Hayo uliyoyataja hapo juu kama sio mzakendo huwezi kuyafanya. Maana unaweza kuhamisha mzigo wote Uswisi. Kama anavyofanya mkulu wenu.
 
Kwangu mimi ni habari njema sababu zinatia moyo. Maana wote wanaonyesha moyo wa uzalendo. Maana kipimo kidogo tu cha janga la dunia kimethibitisha Chadema haifai.
Kama taifa tupo vitani lakini wao wamegeuka kuwa maadui. Nasikia kuna wawakilishi walishahama kimoyo moyo. Maana hawtaki kutangaza mapema. Wanasubiri kipyenga kipigwe tar 28 kuashiria bunge limefungwa alafu waje kuunga mkono wazalendo wenzao.
Pia wamenieleza masikitiko mengi sana ikiwemo matumizi ya Chama kama Saccos ya kiongozi wao kujitalisha. Makatibu wa wilaya hawalipwi, wabunge wanachangishwa pesa. Kuna Ford ranger moja iliyotolewa msaada na wafadhili mkulu wa chama alijimilikisha kisa tu baba mkwe ni muasisi wa Chadema.
Kwa ujumla Chadema ni mali ya mtu binafsi na wao wanasubiri kipyenga cha mwisho priii priii. Wapo kama nane wanajiunga Nccr mageuzi na aliyenidokeza simtaji maana mnaweza kumfukuza kupitia teleconference. Nyie sio wavumilivu.
Mkuu bado unaimani na NCCR IYO ATA IKINGIZA WATU 20000 HAIWEZI NYANYUKA TENA bora ingekua CHAUMA
Weka imani kwa sasa kwenye vyama 3 kwa sasa tz
CCM
CHADEMA
ACT WAZALENDO BASI
Maana historia inaonesha tz hakuna chama kimewai kufa badae pata huai hasa vile vilivyo wai kua kwenye peak ,So mbatia asipokua makini hata kwenye jimbo ataangukia. Pua na kubaki subiri ubunge wa kuteuliwa Tuombe mungu covid itupishe mapema na tuwe wazima
 
Taarifa yako inapunguzaje Bei ya sukari..?
Wenyewe wanakwambia Jiwe akinywa chai na familia yake huko mafichonj burigi inatosha. Nyie wengine mtafune hata miwa kama vipi.
 
Sheria ya mbegu kuota lazima ife ndio iote, na inapoota inatoa mbegu nyingi na tena bora zaidi.

Mbegu ya CHADEMA imezikwa, ishaoza, na sasa inaanza kumea taratibu.

Mark my words....mimi CCM ila kwa sasa CHADEMA inaelekea kuwa bora zaidi...ingekuwa dola haifanyi kwa upande wetu leo hii na katika nyakati ngumu na zenye majaribu kama hizi, basi jua kuwa fukuto lingeanzia CHADEMA na mwangi wake ungetua Lumumba kwetu, then, guess what .....the thing called "KUTOKUWA NA IMANI NA KITI".

Je, ni nani mwenye uthubutu wa kufanya haya angali kuna boko, mamba, na simba wamekenua madomo yao tayari kummeza "mhaini" ama mkosoaji?
 
movie nzuri ni ile sterling anapitia magumu meeeni na kuyatatua hivyo sio mbaya wacha mabo yasidi kuwa mengi ili tujue nani ni sterling wa hii movie, na mara zote jambazi huwa na mikogoo na nguvu nyingi hapo mwanzo mpaka anakuwa na uhakika wa kushinda
 
Wajiunge tu, so what? Hakuna jipya, soko la watumwa linaendelea.
 
Back
Top Bottom