Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Aisee, dunia inakwenda kasi sana siku hizi. Nimehitaji kubadili laini X kwenye simu yangu ili nipachike laini yenye bando kwa ajili ya kuwatembelea wale ndugu zetu wale.
Kwa bahati mbaya nimekosa kinyofoleo cha laini. Nimesaka nyumba nzima kutafuta pini au sindano pasi na mafanikio. Nikaona isiwe kesi, wacha niingie kwa Mangi. Ile kuulizia tu, watu wamenipiga macho yasiyo na kifani, Mangi akasema hana.
Nikasogea duka jirani, kuulizia akaniambia kuwa anazo lakini hauzi usiku huu. Najihisi sijui wamenichukuliaje aisee ingawa sijajua ni kwanini nimekataliwa kuuziwa.