Nimeenda kukodi ambulance nikaambiwa hakuna utaratibu huo

Nimeenda kukodi ambulance nikaambiwa hakuna utaratibu huo

lakini kumbuka amesema ni mbali hata wewe huwezi kutembea hata nusu kilomita ukiwa na mimba iliyotayari kuleta ka gen z hapo utasikia kanakwambia acha kunichosha na hakajatoka. Kutembea ni vizuri kama umefka mita kama mia unaweza shuka utembee mimi wangu ni pikipiki mda huo akiniuma mgongo ruka rukisha yeye kwene mabone tukifika ni chap kidogo mpaka sasa nna alama mbili mgongoni moja ya firstborn niling'atwa na nyingne ya kalastborn ka sasa we acha tu. Ya firstborn alining'ata kweli lakin tokana na maupendo nilijikaza tukafika hos mda anaingia labour na mimi naenda kushonwa akijifungua tunarudi kwa gari sasa
Ndio inamsaidia mtoto asogee haraka! Hongera kwa kwa kuwa baba na mume bora! Dah uchungu wa kuuma mgongo jamani😰
 
Habari wana jukwaa, nina mgonjwa(mama mjamzito) mda wake wa kujifungua umekaribia na ninapokaa kuna umbali kidogo mpaka hospitali kwa hofu ya kuhofia asije akapata uchungu usiku ikanibidi niende hospitali ya Vijibweni(Kigamboni) kwenda kuongea nao walau niweze kukodisha ambulance ili mda ukifika niwapigie simu wamfate mgonjwa wangu wamlete hospital.

Nilichoambiwa hapo mapokezi ni kuwa hakuna utaratibu wa ambulance kumfata mgonjwa nyumbani, kazi ya ambulance ni kumtoa mgonjwa hospital A na kumpeleka hospital B, kama mgonjwa atazidiwa usiku itabidi nikodi bajaji nimpeleke hospitali
Yes,
ulipewa jibu sahihi sana gentleman,

halafu,
kwani kurequest gharama ilikua kubwa zaidi gentleman?🐒
 
Ka Junia kanakaribia kuja duniani kaje kudekezwa na baadae kasumue vibinti vyetu..

Mkuu kodi bajaji chap tu....

Otherwise kamata mawasiliano ya ambulance binafsi hapa usisumbue hizo za serikali ni kwa ajili ya critical issue. Mimba sio ugonjwa....

1. E-Plus Tanzania Ambulance Services
📞 0800 01199 (toll-free)
📞 0757 395 395
📞 0684 395 395
2. Dar es Salaam Flying Doctors
📞 0787 747 464

3. Divine Heart Ambulance Services
📞 0699 404 040
 
Habari wana jukwaa, nina mgonjwa(mama mjamzito) mda wake wa kujifungua umekaribia na ninapokaa kuna umbali kidogo mpaka hospitali kwa hofu ya kuhofia asije akapata uchungu usiku ikanibidi niende hospitali ya Vijibweni(Kigamboni) kwenda kuongea nao walau niweze kukodisha ambulance ili mda ukifika niwapigie simu wamfate mgonjwa wangu wamlete hospital.

Nilichoambiwa hapo mapokezi ni kuwa hakuna utaratibu wa ambulance kumfata mgonjwa nyumbani, kazi ya ambulance ni kumtoa mgonjwa hospital A na kumpeleka hospital B, kama mgonjwa atazidiwa usiku itabidi nikodi bajaji nimpeleke hospitali
Ulichoambiwa ndiyo utaratibu wa kawaida . Lakini zipo za binafsi? Au huko vijiweni hakuna?
 
Ambulance mbona zinafuata watu nyumbani.
Ps. Hiyo ya kuandaa ambulance kwa uzazi nalo ni jipya! Andaa tu gari dalili zikianza tu mnaenda. Bila shaka ni uzao wenu wa kwanza!
Na hospital ya vijibweni mbona ni nzuri tu kujifungulia pale labda kama ana complications za kuhitaji kwenda hospital kubwa
 
Wanaume kama nyinyi mnapatilana wapi 🥹
Sisi wengine tulikosea wapi 😭
 
Sio kila mgonjwa anahitqji ambulance. Ambulance ni emergency. Ujauzito sio ugonjwa wala emergency tena wewe umeenda kuwathibitishia kuwa huna emergency.
 
Kuna siku niliwahi kuona wanatangaza app ya kuitisha ambulance kwa mama wajawazito na wagonjwa inafuata walipo na kuwapeleka hospitali (nikasema hakika Tanzania tunafanikiwa tunasonga mbele kwa kasi ). Hii stori yako inanifanya nibatilishe uamuzi n kuona ni sinema walikuwa wanatuchezea.
Jiandae kukodi gari/bajaji siku ikifika mpeleke tena uiiwa na hela mpeleke hospitali binafsi hizi za Serikali ni miyeyusho.
 
Kazi ya Ambulance ni kuondoa wagonjwa nyumbani na kuwafikisha hospitali, maana baadhi ya wagonjwa wanahitaji huduma ya dharula kabla hawajafikishwa kwenye kituo cha afya.
Vinginevyo kumuondoa hospitali ndogo kumfikisha kwenye hospitali ya rufaa.
Majibu kwamba 'hawana huduma hiyo' ndiyo hoja zinapaswa kujibiwa na mamlaka husika.
 
Back
Top Bottom