Nimefanikiwa kuacha kunywa soda

Abby Newton

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2017
Posts
1,252
Reaction score
2,253
Mwaka 2017 nikiwa chuoni niliamua kuacha kunywa soda na soft drinks zote baada ya kupima sukari na kukuta ikiwa juu kiasi.

Sasa imetimia miaka 4 bila kunywa na nimezoea kabisa. Najihisi kuwa na afya njema sana na wala sitamani zaidi ya kuwaonea huruma wanaotumia. Asante Mungu!
 
Kongole kwako mkuu, sisi tunajitahidi kuacha supu na chapati mbili lakini wapi tumeshindwa
 
Kama umeacha soda aina zote...basi pia punguza vyakula vyenye sukari nyingi kupindukia.

Tunaishi zama ambazo kuna abuse of sugar and carbs foods...na hii imepelekea magonjwa ya mtindo wa maisha kuongezeka.

Unakuta toka mtu ameamka hadi analala..amekula wanga na sukari za kutosha kuliko mwili unavyohitaji. Matokeo yake ni kunenepeana hovyo na kukaribisha magonjwa yasiyoambukiza.
 
Nipo kwenye hatua hiyo pia nami.
 
Mimi nimepunguza kwa kiasi kikubwa sana ila bado sijaweza kuacha kabisa. Wacha niongeze juhudi.
You can't be serious ati kuacha soda ni zoezi gumu..😂

Hichi mbona kitu rahisi sana, mkuu Kama kuacha soda mpaka upambane vipi uraibu wa pombe je..? Punyeto vipi..?

Mkuu jitahidi uache aisee mi kinywaji Cha kiwandani nilichobakiza sahivi ni grand malt hii sidhani Kama nitaiacha japo huwa siinywi Mara kwa Mara..😅
 

Nimeweza kuacha sigara ila soda aina ya pepsi nimeshindwa kuiacha
 
Hahaaa.. sasa na wewe grand malt si ni soda tu ile? Mimi nimepambana sana mkuu nilianza kuacha sigara, nikaja nikaacha pombe na sasa niko kwenye mkakati wa kuacha kabisa soda.
 
Hahaaa.. sasa na wewe grand malt si ni soda tu ile? Mimi nimepambana sana mkuu nilianza kuacha sigara, nikaja nikaacha pombe na sasa niko kwenye mkakati wa kuacha kabisa soda.
Soda sinywi juice ya kutengeneza nyumbani nakunywa ambayo haina sukari ...pepo limebaki kwenye gambee hii kitu kuacha nimeshindwa acha niendelee kunywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…