SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

Stories of Change - 2022 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwezi januari mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi,ambae ni mtoto wa kipekee kutoka katika familia hii masikini.

Mama huyu alininyonyesha, akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua kwa kupewa maziwa ya ng'ombe kwa kuwa hawakuwa pia na uwezo wa kuninunulia maziwa ya kopo (lactogen),baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona alishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi. Kiukweli kipenzi mama yangu aliumia na kuteseka sana kwa maisha aliyopitia.

MAISHA YA SHULE
Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza, mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.Na kila wakati mama alipokuwa akiniona alinikumbuka na hali yake kidogo kubadilika lakini ni kwa muda mfupi,hali iliyonifanya kuzidi kupambania ndoto zangu ili ziweze kutimia.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7, nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto"(nyumba za kupanga) waliopitia shule za kata wanayajua maisha haya. Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana , mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo Dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .5 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na akasema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

Kumbuka wakati huo tunaenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hatukwenda na vyeti,hivyo ilinilazimu kuwasiliana na shule nilyomaliza kidato cha nne ambapo kulikuwa na mwalimu aliekuwa karibu yangu sana,kiukweli alinisaidia sana mpaka nikapata vyeti(cha kuzaliwa na kidato cha 4),kuhusu cha kidato cha sita(6) niliprint matokeo kwa sababu yalikuwa tayari yametoka.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine ambayo ilidumu kwa muda wa miezi 6 tu,na kufanikiwa kumaliza nakufaulu vizuri tu,,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masomo ya udaktari,kiukweli kwa mliopita muhimbili mnapajua maisha ya pale ni magumu sana,ilikufaulu inakubidi kusoma kwa bidii sana ,mimi pia ilinilazimu kusoma kwa bidii sana, ndipo nilipofanikiwa kumaliza masomo yangu kwa ufaulu mzuri tu kwa sababu niliamini penye nia pana njia, nilitunukiwa udaktari wangu ambao niliusotea kwa miaka 5 pale lengo ni kumsaidia mama yangu kipenzi ambapo muda wote huo nilikuwa namuomba Mungu azidi kumpa afya ili nije kumtibu salama salimi,na sasa ni daktari nimeajiriwa katika hospitali ya Arusha(Mount Meru)

SAFARI YA KUMTIBU MAMA
Baada ya tu ya kuwa daktari, nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi, nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India(hapa nilipata wafadhili kwa maana nilikuw atayari nimejuana na kufahamiana na madaktari wengi niliosoma nao chuoni, na tukahitimu pamoja) ,Nilifika India na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu, tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
 
Upvote 252
Nilikua nishangae maisha haya s bongo mtu unaanza katika situation ya namna hiyo mwanzo mwisho kwa wepesi na urahisi wa namna hiyo, kumbe ni chai bwana!!!!
 
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
Dogo Kwa vitu unavyoandika humu uko na hallucinations, muda mwingi unawaza kujenga angani kama alivyosema 20 percent
 
Nilikua nishangae maisha haya s bongo mtu unaanza katika situation ya namna hiyo mwanzo mwisho kwa wepesi na urahisi wa namna hiyo, kumbe ni chai bwana!!!!
unadhani watu wote hupitia...njia wapitiazo wengine?
 
nashukuru sana
Dkt Amina
Hii inaitwa airtight revenge, Umepambana ukiwa huna pumzi kabisa , na bado umeshinda..
It takes courages, a lot of blessings and a bit of lucky.
 
Duh pole sana dsda yangu. Mimi ni kaka yako tunatokea kijiji kimoja. Nikupe hongera sana kwa kuwa na mpango wa muda mrefu kuhusu mama yako.
Kila kitu huja kwa makusudi yake. Usijiskie vibaya wewe kupatikana katika tendo haram la ubakaji, ispokuwa shukuru sana Mungu kwa kuruhusu wewe uzaliewe ili mama yako apone ugonjwa aliokuwa nao. Nakusihi sana ulione hilo kwa mtazamo huo huna haja ya kumjua baba sababu kumpata ni vigumu sana pengine ajitokeze, ikitokea hivo pia msamehe kwa kitendo alichokifanya kwani 1. Kimekuleta duniani 2. Kimeleta uponyaji kwa mama japo alifanya upumbavu.
Mwisho endelea kusaidia wengine Amina68
nashukuru sana
 
ITOSHE KUSEMA WEWE DADA NI MWONGO SANA NA SIO VIZUR KUTUDANGANYA

Nilisoma huu uzi nikaskitika sana kuona huyu dada alvo jieleza vzr nkajiskia had vibaya ila nkasema hapana kuna vitu haviko sawa kwenye uwandishi wake naviweka kama ifuatavyo

1. alisema kazaliwa mwaka 1997 uzur na mm nimezaliwa mwaka 1996 nkapiga hesabu mm narafk zangu tumezaliwa mwaka mmoja wenzangu nao walisoma MD sasa hv ndo wana malizia internship kwa maana hiyo MD huu ni mwaka wao wa 6 miaka 5 ya MD mmoja wa internship nkaona isiwe kesi pengne alianza shule mdogo sana

UGUNDUZI
Nimekuta uzi mwngne huyu huyu dada kaulizwa form 6 kamaliza lin akasema form six kamaliza 2009 sasa ukitoa 2009 na 1997(mwaka wake wa kuzaliwa) = 12 years

2. kasema anaitwa amina na alisoma Msalato girls nkasema isiwe kesi range ya mm nilie zaliwa 1996 nime malza form 6 mwaka 2016 na kama ulimalza form 6 2016 ukaenda MD bila shida yoyote sasa hv unakua internship

UGUNDUZI
kwetu mm ni dodoma na hiko kipnd nikiwa mwanafunz nilikua na dem wangu msalato ambae alikua ni GS wa shule msalato girls ikabid nimtafute nikauliza kama kuna mtu alikua anaitwa amina kati ya range ya miaka 2016 had 2018 aliwaha pata div 1 ya 4 PCB akasema hakuna nkamwambie nitumie list ya wanafunz wa kipnd hiko kat ya miaka ya 2016 - 2018 jina amina halipo

sikuishia hapo dada umesema ulisoma Muhimbili MUHAS nikaenda kuangalia watu walio chaguliwa kujiunga Muhimbili kati ya miaka 2016 - 2018 sijaona jina la amina kama jina lingekuwepo la amina muhimbil hua wana chagua na mbele ya jina wana andika index namba yako ya form 6 ningejua umetoka shule gan na ile index namba ningeona had ulipata div ngap

NB kumbuka alie malza form 6 mwaka 2016 hajamalza MD bado yupo internship sa hv ila huyu anajiita Dk.Amina kumbuka ukimalza internship hua kuna mtihan wa lesen na had majb yatoke unajkuta MD unaenda mika 7

3.Alisema kasoma msalato

UGUNDUZI
kwenye uzi mwngne kasema kasoma Tabora girls

stak kuendelea nisiwachoshe mwnye akil atazame ushahid huu ntakao ambatanisha
na kila story ana claim ni yeye na anasema kabisa muhusika mkuu ni mm

sasa wewe dada ni story teller au maana umesema mama mzazi hiv kwel wewe wa kutulisha matango pori sisi
IMG_4454.jpg

IMG_4455.jpg

IMG_4456.jpg

IMG_4457.jpg

IMG_4458.jpg

IMG_4459.jpg

IMG_4460.jpg

IMG_4453.jpg
 
Attachments

  • IMG_4454.jpg
    IMG_4454.jpg
    61.6 KB · Views: 14
  • IMG_4454.jpg
    IMG_4454.jpg
    61.6 KB · Views: 15
ITOSHE KUSEMA WEWE DADA NI MWONGO SANA NA SIO VIZUR KUTUDANGANYA

Nilisoma huu uzi nikaskitika sana kuona huyu dada alvo jieleza vzr nkajiskia had vibaya ila nkasema hapana kuna vitu haviko sawa kwenye uwandishi wake naviweka kama ifuatavyo

1. alisema kazaliwa mwaka 1997 uzur na mm nimezaliwa mwaka 1996 nkapiga hesabu mm narafk zangu tumezaliwa mwaka mmoja wenzangu nao walisoma MD sasa hv ndo wana malizia internship kwa maana hiyo MD huu ni mwaka wao wa 6 miaka 5 ya MD mmoja wa internship nkaona isiwe kesi pengne alianza shule mdogo sana

UGUNDUZI
Nimekuta uzi mwngne huyu huyu dada kaulizwa form 6 kamaliza lin akasema form six kamaliza 2009 sasa ukitoa 2009 na 1997(mwaka wake wa kuzaliwa) = 12 years

2. kasema anaitwa amina na alisoma Msalato girls nkasema isiwe kesi range ya mm nilie zaliwa 1996 nime malza form 6 mwaka 2016 na kama ulimalza form 6 2016 ukaenda MD bila shida yoyote sasa hv unakua internship

UGUNDUZI
kwetu mm ni dodoma na hiko kipnd nikiwa mwanafunz nilikua na dem wangu msalato ambae alikua ni GS wa shule msalato girls ikabid nimtafute nikauliza kama kuna mtu alikua anaitwa amina kati ya range ya miaka 2016 had 2018 aliwaha pata div 1 ya 4 PCB akasema hakuna nkamwambie nitumie list ya wanafunz wa kipnd hiko kat ya miaka ya 2016 - 2018 jina amina halipo

sikuishia hapo dada umesema ulisoma Muhimbili MUHAS nikaenda kuangalia watu walio chaguliwa kujiunga Muhimbili kati ya miaka 2016 - 2018 sijaona jina la amina kama jina lingekuwepo la amina muhimbil hua wana chagua na mbele ya jina wana andika index namba yako ya form 6 ningejua umetoka shule gan na ile index namba ningeona had ulipata div ngap

NB kumbuka alie malza form 6 mwaka 2016 hajamalza MD bado yupo internship sa hv ila huyu anajiita Dk.Amina kumbuka ukimalza internship hua kuna mtihan wa lesen na had majb yatoke unajkuta MD unaenda mika 7

3.Alisema kasoma msalato

UGUNDUZI
kwenye uzi mwngne kasema kasoma Tabora girls

stak kuendelea nisiwachoshe mwnye akil atazame ushahid huu ntakao ambatanisha
na kila story ana claim ni yeye na anasema kabisa muhusika mkuu ni mm

sasa wewe dada ni story teller au maana umesema mama mzazi hiv kwel wewe wa kutulisha matango pori sisiView attachment 2322033
View attachment 2322034
View attachment 2322035
View attachment 2322036
View attachment 2322037
View attachment 2322039
View attachment 2322040
View attachment 2322041
THIS CASE IS CLOSED...... AMESHAKUWA DISCREDITED.
 
na alivo malzia akasema akamaliza chuo akamfata mama ake akampeleka india akutaja source of fund labda kama alifanya harambee hiv anaujua mshahara wa MD anae anza kazi mshahara wa doctor akiwa ana anza kaz ni 1.4M ila makato + kama alichukua na mkopo yanamfkisha had kwenye mshahara wa
890k - 900k nauli ya kwenda india na kurud ni kama 1.6M na mdogo wangu anasoma india chuo LPU hapo kwenye nauli napajua vzr sana nimeenda sana terminal 3 airport yan kwa ufupi ukipiga mahesabu hayaend akiwa muongo ajue hata kujumlisha na kutoa
 
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
Uniwie tu radhi. Nilikupigia kura, ila kutokana ushahidi wa hapo juu, nimeona niitoe tu kura yangu.

Stori yako kiukweli inaonekana ni ya kufikirika. Na jambo hili halikubaliki hata kidogo.
 
Kuna kitu sijaelewa hapa. Umezaliwa 1997, shule umeanza ukiwa na miaka 7 hapo ni mwaka 2004. Ukijumlisha miaka 7 ya shule ya msingi inakuwa shule ya msingi umemaliza 2011. Ongeza miaka minne ya O-level inakua 2015. Jumlisha miwili ya A-level inakua 2017. Degree ya udaktari inatolewa miaka mitano ambapo kwa hesabu mwaka huu 2022 ndo ulitakiwa uwe mwaka wa mwisho wa masomo yako ya udaktari. Hapo bado hujafanya internship kwa mwaka mmoja. Naomba nifafanulie hapo Mkuu.
Na kwa miaka 25 akapata hela ya kumtibu nchini India [emoji1128], labda alipata ufadhili hongera zake binti[emoji122]
 
nimeanza drs la 7 mwaka 2003
nimemaliza drs la 7 mwaka 2009
nimeamaliza kidato cha 6 mwaka 2015,
nimemaliza intern 2021,kazini nimeingia 2021
Heala za india ulizitoa wapi?!
Hongera bidada
 
kuwa mkweli basi?
wewe ni Manka au Amina?

katika uzi huu post #4 ulikiri kuwa wewe ni Manka na ulikuwa kahaba na ukabahatika kuwa dereva wa Ikulu.
huku unajiita Amnina wa Itilima.
Ukiwa muongo jitahidi iwe una kumbuka kuwa jana uliongopa kitu gani mdada
Punguza jaza mkuu 😆 😆 😆 😆 😆 hela inasakwa kwa kila mbinu
 
Back
Top Bottom