Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

oooh nataka kuwatumikia....wananchi wameniomba....oooh mie mzalendo...bra...bra kibao...
fuateni taratibu za chama...subiri kiwapitishe kwanza...ikumbukwe kuna UKAWA pia.
We unadhani Lipumba au Mbowe akisema kaamua nae kugombea urais itakuwaje...epukeni kutengeneza makundi.
 

Rudia kusoma comment yangu, utagundua kuwa yote unayoyasema kwenye comment yako hii nimeyajibu. Aidha ukinifatilia kwenye ule uzi sijacomment maana siyo yeye aliyeanzisha ule uzi, wakati huohuo alikuwa hewani hakujibu ule uzi akisoma.
Ni hulka ya binadamu kukiweka zaidi kichwani kitu ulichokifanya mlipoonana mara ya kwanza, though sio wote maana sio lazima. CHADEMA haimuogopi zitto ndio maana yeye alienda mahakamani kupinga kumjadili. Yeye ndie anaogopa.
You just wait, time will tell
 

Sijasema wewe ila michango ya makamanda wenzako ilijaa lugha za kejeli, uropokaji na mengineyo pasipo kutafuta ukweli. Bahati mbaya hii tabia haijaanza kwa ben tu ila hata kwenye uzi wa shibuda, mdee na wengineo. Ndio maana nasema kuna harufu ya uchafu mwingi ndani ya chadema ila hausemwi hadi mtu ahamie chama kingine

Lingine ni kwamba huwezi kuchukua dolla kwa kutukana au kukejeli wapinzani wako kwa sababu hujui nani atakayekufaa na wakati gani. Bahati mbaya hizi lugha zenu hata viongozi wanaitumia. Mlisema CUF ni CCM B sijui waaaliti na mengineyo. Mfano Wakati waziri kivuli wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi wenye akisoma bajeti yake ya 2013/14 bungeni alitamka kuwa CU..F ni liberals so kwa ideology hiyo wanaruhusu ndoa za jinsia moja ushoga na usagaji (nenda youtube utaiona) lakini leo mmeungana. je mmeungana kwa kufuta kauli yenu au vinginevyo? ???.

ipo siku chadema itakaa meza moja an act siyo miujiza ni siasa tu.
 

Ukiiisoma MOU ya UKAWA utagundua kuwa malengo ya umoja huu ni tofauti na unavyodhani na kuandika hapa.
Ukitaka kujua UKAWA ipo kwa misingi na makubaliano yapi ni vema ukaisoma ili uelewe. Sitashangaa kuona hayo unayosema maana mazungumzo yakifikia mnaweka mwafaka na makubaliano.

Vilevile hata CCM inaweza kaa meza moja na UKAWA yakifika maji ya shingo. Zotto alipogeresha kutaka kumuondoa PM, hata wabunge wa CCM walisaini.
 

Vipi kuhusu lugha? Naomba hiyo MOU kama siyo top secret
 
Vipi kuhusu lugha? Naomba hiyo MOU kama siyo top secret

Kuhusu lugha we jiongeze mwenyewe maana lugha za Kibajaji i.e Lusinde unazijua.
MOU fuata taratibu zilizopo katita ofisi za vyama wana um9ja wa UKAWA utapata.
 
Naunga mkono vijana wote wanaotaka kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika Taifa letu, lakini sasa acheni nyimbo za kupigana vita Vijana wenyewe kwa wenyewe hili ni jambo la aibu. ni matumaini yetu kwamba kutoka kwako na Yeriko Nyerere hatutasikia tena mkiwapiga vita vijana wenzenu popote walipo, katika siasa popote duniani kutofautiana mawazo hakumfanyi mtu kua -------. Tumeona vijana wengi DEO, BULAYA na wengineo wakienda kinyume na Chama chao lakini hatujasikia kwamba ni --------. Vyama vyenu viige hili kama CCM inavyo chota SERA za vyama vya upinzani katika utekelezaji. Ongezeni mwendo lakini bila kupiga vita Vijana wenzenu...

 
Ben tunawahitaji viongozi wanaojua ABC za maisha yetu, ambao watawania nafasi za uongozi, si kwa kuwa wanataka maisha mema kwa familia na ndugu zao tu bali kutumia fursa na nafasi walizopata kusaidia wengine kujikwamua kimaisha....

Heko Ben... umefanya vyema kutangaza nia, binafsi nataka upate nafasi kisha uwakilishe wananchi kwenye chombo kikuu cha maamuzi na sisi tukiwa nyuma yako kukukumbusha pale tutakapoona umesahau jambo ili kwa pamoja tufikie malengo...
 
Kuhusu lugha we jiongeze mwenyewe maana lugha za Kibajaji i.e Lusinde unazijua.
MOU fuata taratibu zilizopo katita ofisi za vyama wana um9ja wa UKAWA utapata.

Kama Una justify huo upuuzi (hizo lugha chafu) kwa sababu ya kibajaji???? After all anachofanya kibajaji ni kuwaonesha kuwa kila mtu anaweza kutukana nothing else. ..........

Na kama MOU ni siri ngoja ngoja nijiandae for Manchester derby
 
Tunahitaji wengi wenye nia na maono kama hayo, ili Watanzania wapate walau nafuu kwa mzigo waliobebeshwa!

NENDA KIJANA.
 
Zito alipoonesha nia ya kugombea nafasi ya mwenyekiti ndani ya chama, aliitwa ------- na baadae kuundiwa zengwe na kufukuzwa. Lakini Ben kutangaza nia ya kugombea jimbo ambalo bado lina uwakilishi na hatujasikia kama mhusika kutangaza kutogombea tena, hakuna kauli za usaliti wala mikakati ya kufukuzwa Chama, hii ni sawa?? je kanuni za demokrasia zimetumika sawa kwa hawa watu wawili. Kama bado huyu nae hajafikia huko alipopelekwa mwenzake, inamaana na yeye atafukuzwa uanachama. Kwahiyo tunaweza kusubiri chama kipya cha Ben kama akishindwa kupata nafasi ya kugombea ubunge. ama ni kweli atahama ili atimize ndoto yake.
 
Kama Una justify huo upuuzi (hizo lugha chafu) kwa sababu ya kibajaji???? After all anachofanya kibajaji ni kuwaonesha kuwa kila mtu anaweza kutukana nothing else. ..........

Na kama MOU ni siri ngoja ngoja nijiandae for Manchester derby

Umeambiwa "jiongeze" this doesn't make a sentence justified. Hiyo inamaanisha "think" or use your capabilites. MOU inatolewa kwa application rasmi yenye constructive reasons for need of it.
 
Umeambiwa "jiongeze" this doesn't make sentence jusfied. Hiyo inamaanisha "think" or use your capabilites. MOU inatolewa kwa application rasmi yenye constructive reasons for need of it.

Okay nitajiongeza lakini waambie hao wenzako siyo fresh.
Hahaaa MOU ni siri???? sasa kwanini mnapiga kelele bungeni kwamba mikataba iwekwe wazi kama hata ile wanayoingia viongozi wenu ni siri kwa wanachama???
 
Okay nitajiongeza lakini waambie hao wenzako siyo fresh.
Hahaaa MOU ni siri???? sasa kwanini mnapiga kelele bungeni kwamba mikataba iwekwe wazi kama hata ile wanayoingia viongozi wenu ni siri kwa wanachama???

Unataka iwekwe wazi ili chama chako kipate gear? Hilo sahau.
Kamwambie Katibu mkuu kiongozi awapewanahabari nakala ya hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Okay nitajiongeza lakini waambie hao wenzako siyo fresh.
Hahaaa MOU ni siri???? sasa kwanini mnapiga kelele bungeni kwamba mikataba iwekwe wazi kama hata ile wanayoingia viongozi wenu ni siri kwa wanachama???

Bomoa upinzani kazi mnayo.
 
kaka umefanya uamuzi sahihi wakati muafaka...mungu aendelee kuwa na wewe. wana mrere tunakuahidi kila aina ya ushirikiano....keep going kamanda...nitupie namba yako pls.
 
Maelezo mengi lakini hakuna la maana hata moja hapo. Imekushinda BAVICHA, jimbo utaliwezea wapi wewe?

Hamy dada ulichokitegemea sicho, ulitegemea huyu kamanda atangaze kuwa kahamia Against Chadema Tanzania basi hapo roho yako ingekuwa kwatu! Hata angeandika page tatu.
 
Nawatakia kila la kheri makamanda wangu na mimi nipo kwenye safari moja na nyie ijapokuwa mimi nitachelewa kufika huko labda mungu akisaidia 2025 Kamanda Ben utaniachia jimbo kwa sasa ngoja nielekeze nguvu zangu council ili nijenge chama, niwe karibu na wananchi na kuongeza uzoefu.

safari yenu ni safari yetu sote. kila la kheri kwenye safari yetu ya mafanikio

Safari yako ni safari yangu, Safari yangu ni safari yako, Safari yetu ni safari ya Watanzania.

Twende Bungeni na Ben Saanane!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…