Ben Mungu akushike mkono, akuwezeshe, akupe kibali cha pekee, akupe hekima na ufahamu maalumu na zaidi sana akulinde na safari yako aifanikishe. Tunakumbea kwa Mungu. Utakapofanikiwa, ukumbuke kutenda sawa sawa na maneno yako. Tumia nafasi hiyo kurejesha tumaini la uhai kwa watanzania.
Tumia nafasi hiyo kuhakikisha Watanzania wanamiliki na kutawala raslimali zao ambazo sasa ni dhahiri ccm imeziuza kwa wageni ambao ninawaona wanatoka sehemu za mbali wakiwa na nyuso za tabasamu lakini mikono yao yenye makucha ya sumu iko migogoni ikiwa imefunikwa na mavazi yao mapana. Mikono hiyo ndiyo nyenzo yao ya kutimiza azma ya kufuta kizazi cha nchi. Ninaomba Ben ulikomboe taifa. Wakomboe Watanzania na raslimali zao.
Ben pigana kinyume na sera za migawanyiko na ubaguzi wa aina yoyote ndani ya Tanzania. Watanzania ni wamoja na kwa muda wa ubunge wako hakikisha hili linatimia.
Ben, ninaomba ushiriki kwa nguvu kuimarisha mshikamano katika chama. Itikadi yoyote inayojenga fitina, migawanyiko, na mashindano binafsi inadhoofisha chama. Chama kikidhoofu utendaji wake unaathirika na athari hizo zinaishia kuhujumu maisha na ustawi wa Tanzanai na watu wake.
Nnashukuru kwa sababu umesema hutazingatia huduma za afya tu, bali kila huduma ya jamii hakikisha inakuwa bora kuanzia na elimu. Serajinga za 2014, pigana na hakikisha zinafutiliwa mbali kwa sababu zinajenga mazingira ya kuua vizazi vyetu na kuwamilikisha wageni nchi niliosema wameficha makucha yenye sumu migongoni, tena wanakuja kwa wingi na kwa kasi wakituonyeaha meno lakini mioyo yao ina uchungu wa kuishiwa na raslimali muhimu kwao.
Heshima, amani, upendo kwa viongozi wako na watu wote, ndio msingi wa nguvu yako. Mungu akufanikishe.