Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Bomoa upinzani kazi mnayo.

Suala hapa siyo kubomoa upinzani maana upinzani imara ndio chachu ya maendeleo. Suala ni usiri wa MOU ambao ni kinyume na demokrasia ya ukweli, usiri wa MOU ambao ni kinyume na kilio cha upinzani bungeni kwenye mikataba inayoingia serikali.
 
Kwahiyo lile shina la ccm ulilozindua pale mtaani kwako unalikana?

Pale nimeshiriki kama mwanakijiji wa eneo lile, nimeshiriki kama sehemu ya shughuli za kijamii sawa na zingine kama harusi, msiba na zinginezo. Kwa hiyo wewe ukihudhuria mkutano wa chama fulani tayari unakuwa member? Njoo na wewe fungua tawi nitahudhuria hahahaaa
 
Suala hapa siyo kubomoa upinzani maana upinzani imara ndio chachu ya maendeleo. Suala ni usiri wa MOU ambao ni kinyume na demokrasia ya ukweli, usiri wa MOU ambao ni kinyume na kilio cha upinzani bungeni kwenye mikataba inayoingia serikali.

Hakuna taasisi inayoweka kila kitu wazi, ndio maana hata huko serikalini kuna mambo ya siri tena za levels tofauti.
Formula ya maendeleo ya tbl haiwezi kuwekwa wazi maana sbl anaisaka ili aanzie hapo.
Mikataba ambayo ina maslahi kwa taifa isisainiwe dubai na waziri mmoja aliyelipiwa kila kitu na kampuni anayoisainia, yafaa ikadhibitishwe na bunge. Siri za chama chenu hatuzitaki hadharani, lakini siasa chafu tutazipata tu
 
Pale nimeshiriki kama mwanakijiji wa eneo lile, nimeshiriki kama sehemu ya shughuli za kijamii sawa na zingine kama harusi, msiba na zinginezo. Kwa hiyo wewe ukihudhuria mkutano wa chama fulani tayari unakuwa member? Njoo na wewe fungua tawi nitahudhuria hahahaaa

Mbona chadema ikifanya mikutano hauhudhurii? By the way inshitaji kujiongeza kidogo tu kufahamu your stand hata kama nisingeona hilo.
 
Ben,

Lakini vijana wenzako wa Bavicha walikutukana Sana na kukuponda sana. Walikunanga Sana Na kukulisha maneno Mengi sana.

Nimeamini Chadema hampendani leo wale wale Waliomnanga ati hongera Kamanda Kweli hiyo Hongera inatoka moyoni?

Acheni wivu jifunze kuwa na subra vijana
 
Mbona chadema ikifanya mikutano hauhudhurii? By the way inshitaji kujiongeza kidogo tu kufahamu your stand hata kama nisingeona hilo.

Ili nihudhurie lazima aidha ninywe pombe au nipige bangi kwanza nibakize akili ya kusema powaaaaa.
 
Ili nihudhurie lazima aidha ninywe pombe au nipige bangi kwanza nibakize akili ya kusema powaaaaa.

Kwani huwajui importets wakubwa wa hayo madawa? Wale wale wanaopandidha twiga kwenye ndege bila kionekana na vyombo vya Usalama
 
nahisi kama unauwezo wa kujenga hoja nakuzitetea so unasitahilikuwa mbunge bt am not sure kama ninachokihisi ni kweli.
 
hii singo haiuzi . iliyouza ni ile ya kuhama. bora ungehama tu. every one predicted this. so it is not news at all. and on top.of that. hivi ni lazima kila mtu anayetaka kuonesha mchango wake kwa taifa awe mbunge?? we all know it ia not about that. its about. money . power and fame. unaweza jenga nchi hata ukiwa nje ya bunge.
True. Mkuu umeongea. Sijui Kwa nini hawa watanzania wa enzi hizi hawatangazi nia Ya kukamata mashamba vijijini na kuonyesha mfano halisi kwa walalahoi wa kawaida -
 
Ben Mungu akushike mkono, akuwezeshe, akupe kibali cha pekee, akupe hekima na ufahamu maalumu na zaidi sana akulinde na safari yako aifanikishe. Tunakumbea kwa Mungu. Utakapofanikiwa, ukumbuke kutenda sawa sawa na maneno yako. Tumia nafasi hiyo kurejesha tumaini la uhai kwa watanzania.

Tumia nafasi hiyo kuhakikisha Watanzania wanamiliki na kutawala raslimali zao ambazo sasa ni dhahiri ccm imeziuza kwa wageni ambao ninawaona wanatoka sehemu za mbali wakiwa na nyuso za tabasamu lakini mikono yao yenye makucha ya sumu iko migogoni ikiwa imefunikwa na mavazi yao mapana. Mikono hiyo ndiyo nyenzo yao ya kutimiza azma ya kufuta kizazi cha nchi. Ninaomba Ben ulikomboe taifa. Wakomboe Watanzania na raslimali zao.

Ben pigana kinyume na sera za migawanyiko na ubaguzi wa aina yoyote ndani ya Tanzania. Watanzania ni wamoja na kwa muda wa ubunge wako hakikisha hili linatimia.

Ben, ninaomba ushiriki kwa nguvu kuimarisha mshikamano katika chama. Itikadi yoyote inayojenga fitina, migawanyiko, na mashindano binafsi inadhoofisha chama. Chama kikidhoofu utendaji wake unaathirika na athari hizo zinaishia kuhujumu maisha na ustawi wa Tanzanai na watu wake.

Nnashukuru kwa sababu umesema hutazingatia huduma za afya tu, bali kila huduma ya jamii hakikisha inakuwa bora kuanzia na elimu. Serajinga za 2014, pigana na hakikisha zinafutiliwa mbali kwa sababu zinajenga mazingira ya kuua vizazi vyetu na kuwamilikisha wageni nchi niliosema wameficha makucha yenye sumu migongoni, tena wanakuja kwa wingi na kwa kasi wakituonyeaha meno lakini mioyo yao ina uchungu wa kuishiwa na raslimali muhimu kwao.

Heshima, amani, upendo kwa viongozi wako na watu wote, ndio msingi wa nguvu yako. Mungu akufanikishe.
 
Safiri ya matumain mdogo na Munge atimize ndoto zako tupo pamoja na wewe
 
Safari yako ni safari yangu, Safari yangu ni safari yako, Safari yetu ni safari ya Watanzania.

Twende Bungeni na Ben Saanane
 
hii singo haiuzi . iliyouza ni ile ya kuhama. bora ungehama tu. every one predicted this. so it is not news at all. and on top.of that. hivi ni lazima kila mtu anayetaka kuonesha mchango wake kwa taifa awe mbunge?? we all know it ia not about that. its about. money . power and fame. unaweza jenga nchi hata ukiwa nje ya bunge.

Ni kweli kuwa kila mtanzania siyo lazima awe Mbunge ili awaendeleze watu wake lakini ni kweli pia kuwa kila Mtanzania ( Kama BEN) anayohaki ya kuwaendeleza watanzania kwa kutumia jukwaa la Bunge. Hoja yako ya money and power inakubidi uweke ushahidi, vinginevyo sisi tunalazimika kuamini kile alichoandika mhusika.
 
Safari yako ni safari yangu, Safari yangu ni safari yako, Safari yetu ni safari ya Watanzania.

Twende Bungeni na Ben Saanane!
ndege wafanano huruka pamoja.
kunguru nyie mliozoea kula mizoga na utunzi wa hekaya isingekuwa ajabu kuungana mkono.
nawatakia kila la kheri katika safari yenu ambayo katu haitakuwa na mafanikio.
poleni na bangi zenu
 
Back
Top Bottom