Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Ni kweli TAWA....
WALIMTABIRIA ETI ATAJIUNGA ACT IMEKUWA TOFAUTI WHAT DO YOU EXPECT THIS DUDE TO SAY...


Hamy dada ulichokitegemea sicho, ulitegemea huyu kamanda atangaze kuwa kahamia Against Chadema Tanzania basi hapo roho yako ingekuwa kwatu! Hata angeandika page tatu.
 
“Naelekea Bungeni”

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata

Ben saanane nakupa baraka zote,,go for your dream make it happen
 
Zito alipoonesha nia ya kugombea nafasi ya mwenyekiti ndani ya chama, aliitwa ------- na baadae kuundiwa zengwe na kufukuzwa. Lakini Ben kutangaza nia ya kugombea jimbo ambalo bado lina uwakilishi na hatujasikia kama mhusika kutangaza kutogombea tena, hakuna kauli za usaliti wala mikakati ya kufukuzwa Chama, hii ni sawa?? je kanuni za demokrasia zimetumika sawa kwa hawa watu wawili. Kama bado huyu nae hajafikia huko alipopelekwa mwenzake, inamaana na yeye atafukuzwa uanachama. Kwahiyo tunaweza kusubiri chama kipya cha Ben kama akishindwa kupata nafasi ya kugombea ubunge. ama ni kweli atahama ili atimize ndoto yake.

Twende bungeni na Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Unajielewa Ben..... Nakuombea Mungu ufanikiwe katika safar yako hii uliyoianza....Tanzania needs people like you....
 
Maelezo mengi lakini hakuna la maana hata moja hapo. Imekushinda BAVICHA, jimbo utaliwezea wapi wewe?
Wee endelea na ujinga wako,mwenzio anakuzidi kwa kila tasnia tangia elimu,uelewa,maono,badala ya kukaa chini na kutafakari tatizo la umasikini na ujinga ulokujaa uko bze hitting the rock with bare hands hoping it will feel the pain and not you!
Kanyaga kamanda Ben songa mbele kwenye safari ya ukombozi.
 
sijasoma yote uliyoandika ila nimechukua point,ambayo inahusu story za wewe kwenda ACT.Sasa ninaamini za uongo.
 
Mimi nakutakia kila lililo la heri ktk safari yako uliyoianza...!
 
Nilikufahamu zaidi kwa kazi ile ya kuwaibua team wa.sa.li.ti na sasa usaliti wao umekuwa dhahiri,, pia unaweza wasilisha vyema kimaandishi mawazo yako..bila shaka na kwa kuongea utakuwa vizuri. Kila la heri kingozi Ben
 
Unastahili kaka kama unania ya dhati utatimiza malengo yako simamia msimamo wako watu wasikuvunje moyo coz kumbuka si kila mtu atakupenda. Songa mbele na usirudi nyuma.
 
Tunza dhamira yako na subiri mchakato wa chama chako then mchakato wa UKAWA na uwe tayari kukubali matokeo ya uteuzi ndani na nje ya chama chako.
 
kwanza unajaza server kwa kunukuu mhabari wote. Pili ulitaka achimbe barabara na wananchi?

Tatizo lako kubwa ni akili ndogo. Akili kubwa siku zote inahoji haikumbwi tu na mihemko ya ushabiki b-w-e-g-e wewe:biggrin1:
 
Naona Bavicha sasa ni ya kuigopa kama ukoma. Imejaa vijana wenye viburi na kujiona bora na hawataki mtu yeyote aulize swali as if kila aliyepo Chadema ni malaika asiye na udhaifu. Kila kijana wa Bavicha anaona yeye ndo ana akili kuliko vijana wote ambao hawapo Bavicha Hii ni trend ambayo inaonyesha kwamba chama kimejaa watu wenye akili ndogo wanaojifanya wanataka kumkomboa mtanzania. Huwezi tu ukaanza kunidharau kisa nimemuuliza maswali Ben. Huo ni upumbavu uliopitiliza. Ni akili ndogo pekee ndo huwa zinashindwa kuengage in intellectuall debate. Ni vijana wachache sana wanajitambua Bavicha ila hawa weliobakia ni wa kuwahofia sana iwapo Chadema itashika madaraka.
 
Unataka iwekwe wazi ili chama chako kipate gear? Hilo sahau.
Kamwambie Katibu mkuu kiongozi awapewanahabari nakala ya hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Bahati nzuri sina chama mkuu acha kunipakazia, mimi ni mzalendo kwa nchi yangu acha kukwepa mada. aidha chama tawala hakina historia ya kunakili sera toka upinzani ndio maana upinzani unasubiri ccm itangaze ilani ndipo nanyi mtohoe, ndio maana upinzani hautapitisha mgombea hadi ccm ifanye hivyo
 
Bahati nzuri sina chama mkuu acha kunipakazia, mimi ni mzalendo kwa nchi yangu acha kukwepa mada. aidha chama tawala hakina historia ya kunakili sera toka upinzani ndio maana upinzani unasubiri ccm itangaze ilani ndipo nanyi mtohoe, ndio maana upinzani hautapitisha mgombea hadi ccm ifanye hivyo

Kwahiyo lile shina la ccm ulilozindua pale mtaani kwako unalikana?
 
Back
Top Bottom