Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Ben Saanane nakushauri ufanye editing ndogo sana lakini ya msingi katika huu uzi wako.

Ben,hebu mshirikishe mungu japo kidogo kwa kuongeza neno/maneno haya: "mungu akipenda nitaelekea bungeni" au vyoyoye vile utakavyoona inafaa kwani mungu ndio muweza wa yote na hakuna mwenye uhakika wa kuiona kesho.

Ukisoma tamko lake hadi Mwisho utaona alimtanguliza Mungu katika safari hii
 
Last edited by a moderator:
Bungeni kuna nini? Tafuta chuo ufundishe
 
Mkuu Ben Saanane, kwanza naunga mkono hoja, pili nakukubali kwa ujasiri sio tuu wa kutangaza nia bali pia kutangaza vita na aliyepo!. Nakupongeza kwa dhati kwa vile hakuna jimbo ambalo ni mali ya mtu, wala hakuna mbunge yoyote aliyepo mwenye hati miliki ya jimbo lolote hivyo ni haki yako kutangaza nia na kugombea jimbo lolote!.

Pili nimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kutangaza nia baada ya kufanya utafiti!. Nilipokutana na Dr. Slaa mahali ile 2012, nilimweleza kuwa kuna maeneo CCM imechokwa mpaka basi kiasi kwanza kama Chadema ingesimamisha hata jiwe, jiwe lingechaguliwa!, hivyo nikatoa wito kwake kuhakikisha 2015, Chadema inasimamisha wagombea kila jimbo!.

Jaombo la pili nilimsisitizia, Chadema isisubiri hadi wagombea ndio wajitokeze, bali ifanye utafiti kila jimbo iweke competent man na hata ikitokea jimbo fulani wakajikuta hawana kabisa competent men wa kuwasimamisha, then wafanye head hunting ya grooming watu ili wasikose mtu wa kumsimamisha, hivyo nyinyi ambao ni competent mnavyojitokeza mapema mnakirahisishia chama kazi ya kutafuta watu!. Nlishauri watu wawe encoraged kutangaza nia mapema ili mpate muda wa kuwachambua, kuwapima na kuwashindanisha kile aliye bora zaidi na mwenye chance ya kuleta ushindi ndie apitishwe!.

Na tatu nilimshauri, kuwa miongoni mwa wabunge wa Chadema waliomo bungeni, kuna wabunge wazuri bungeni lakini ni hopeless kwenye majimbo yao, hivyo Chadema ifanye utafiti kwa wabunge wake wote waliomo bungeni, chances zao za kuchagulika majimboni mwao zikoje, ili kuzui kupoteza baadhi ya majimbo na kutolea mfano jimbo langu mimi nililopo jimbo la KAWE, ambalo mbunge wangu ni Mhe. Halima Mdee. 2015 CCM inamsimamisha mtu very competent kupambana na Mdee, hivyo nikashauri Chadema don't just sit and watch jimbo la KAWE likirudishwa CCM, bali lifanya utafiti wa chances za Mdee kuchaguliwa tena na kikiona risk, then Chadema ndio kimreplace Mdee na kuleta mtu more competant atakayelitetea hili jimbo, vinginevyo kama Chadema itabweteke na kutosimamisha watu competent kwenye majimbo kinayoyasikilia kwa hoja ya kutowaingilia wabunge waliopo, kitayarudisha baadhi ya majimbo!. Hivyo naamini kwenye jimbo lako, umeishafanya utafiti wa electability ya incumbent na ukajiridhisha kusipofanyika mabadiliko ya mgombea wa Chadema, jimbo linarudi CCM!, na ndio maana umeamua kujitosa!. Lakini kama mbunge aliyepo amefanya makubwa, na bado anakubalika, kitendo cha wewe kutangaza kuliwania huo sio tuu ni uchokozi bali ni kutaka kuletea fujo kwa mgombea na kuletea fujo kwa chama. Fujo za aina hii ni ZZK Style watch out usijekuitwa -------!.

Hapa Mkuu Ben Saanane haya ni majisifu ya egotistically driven by egotistic desires from egotisim!. Hapa huna tofauti na ZZK!, kutanguliza umimi!. Unaonekana wewe tayari umeisha determine lazime uwe, sasa ikitokea ukakatwa, unaweza kabisa kuamua kuwa kwa vile umeisha determine, ikishindikana kugombea kupiti Chadema, then utagombea kupitia njia nyingine yoyote!. Hii ni hatari!. Nilishauri ili mtu uwe kiongozi bora sio wewe kujiona una sifa, una uwezo na unaweza, bali tekeleza tuu majukumu yako kama kiongozi kwa kuonyesha uwezo, kisha watu waliokuzunguka, wauone huo uwezo wako, wao ndio waje kukushauri kuwa kija unaweza!, njoo huku utusaidie kwenye nafasi hii ya uongozi!. Hii haina maana ukijiona unaweza usijitokeze bali usijisifu kuhusu uwezo, onyesha huo uwezo usifiwe, ushauriwe gombea, ndipo utangaze nia!.

Hii pia ni muendelezo wa ile ile strong determination yako kwenda bungeni, ningeomba pia utupe na options zako iwapo Chadema haitakupitisha kugombea jimbo hilo ambalo tayari ni ngome ya Chadema, jee uko tayari kugombea jimbo jingine lolote ambalo sio ngome mathalan ka Kinondoni?!, au umepania lazima ugombee hapo hapo ulipoamua, na kama Chadema haitakupitisha unaweza ku jump ship na kulitwaa jimbo hilo?!.

Pamoja sana!.

Pasco

Pasco,

Asante sana na nakubaliana na mengi kati ya uliyoeleza hapa.

1: Halima Mdee bado ni mbunge mchapakazi.Hakuna asiyejua hili

2:Kiongozi ni lazima ajipime yeye kwanza na kuona kama anauweza uongozi badala ya kusubiri au kuandaa watu wa kumshawishi/kumlazimisha wakati yeye anajiona hana uwezo au hataki

3:Bado Sijataja Jimbo kaka

4: Ikitokea tofauti kwa kuwa mimi ni muumini wa demokrasia ya kweli katika uwakilishi wa watu nitachukua hatua za kidemokrasia
 
Last edited by a moderator:
Endeleeni kutiana ujinga

“Naelekea Bungeni”

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata

Ben saa9 nimesoma bandiko lako na ninegundua na wewe ni mroho wa madaraka kama wengine katika vyote ulivyoandika sijaona wazo jipya ambalo sijawahi kulisikia tangu nifikishe umri wa kupiga kura 1990 yote uliyoandika hapo umecopy na kupest tu.....!harakati zako zote za kuchafua huku na kusafisha huku ulikua unasaka tonge kumbe!!!!
Asante kwa kuniweka wazi mroho anajua waroho wenzie lazima afanye fitina wapungue ili apate nafasi.......!
 
Naona Bavicha sasa ni ya kuigopa kama ukoma. Imejaa vijana wenye viburi na kujiona bora na hawataki mtu yeyote aulize swali as if kila aliyepo Chadema ni malaika asiye na udhaifu. Kila kijana wa Bavicha anaona yeye ndo ana akili kuliko vijana wote ambao hawapo Bavicha Hii ni trend ambayo inaonyesha kwamba chama kimejaa watu wenye akili ndogo wanaojifanya wanataka kumkomboa mtanzania. Huwezi tu ukaanza kunidharau kisa nimemuuliza maswali Ben. Huo ni upumbavu uliopitiliza. Ni akili ndogo pekee ndo huwa zinashindwa kuengage in intellectuall debate. Ni vijana wachache sana wanajitambua Bavicha ila hawa weliobakia ni wa kuwahofia sana iwapo Chadema itashika madaraka.
Uwe unahoji maswali ya msingi sasa. Unakuta mtu anakula unamuuliza, unakula? Utapigwa na matonge wewe. Jenga swali uheshimiwe kwa swali.
 
Mwenyezi Mungu na akutangulia asafishe njia yako.
Muda ukifika ni inbox details zako nikupe baraka ziongeze na za wengine/zako ukachukue form.
all the best
 
Yericko Nyerere, Asante sana komredi wangu

Comrade Ben

Kamanda wa makamanda

Shushushu wa mashushushu

Jembe wa majembe

Genious wa ma genious

Mtaalam wa wataalam

Msomi wa wasomi

Mwerevu wa werevu

Msikivu wa wasikivu

Mtii wa watii

Kijana mchapakazi na dira ya taifa hili

Salute to You Kamanda.....Big respect
 
Upande huu kuna Ben Saanane
Fraterin Masika
Joseph Selasini

Upande ule kuna
Evodi Mmanda
Notbruga Masikini
Utouh...

Rombo patakuwa patamu sana mwaka huu... I wish nipte fursa ya kwenda kushuhudia mtanange..

All in all nawatakia makamanda wote wa CDM kila la heri. Ni matumaini yangu waomba nafasi na chama kitaheshimu chaguo la wananchi. Nitasikitika sana nikisikia kuna yeyote kati ya wanaoomba nafasi atakayekimbilia chama kingine kwa sababu tu hakupata nafasi kupitia CHADEMA. Ni matumaini yangu pia kuwa chama kitapitisha jina la mgombea aliyepita kwa kura nyingi za maoni...

Kinachonipa moyo ni kuwa hadi sasa wote mlioonyesha nia kugombea kupitia CDM mpo vizuri kiuchapa kazi...

Kwa kuwa jimbo litakuwa na mbunge mmoja, nashauri wale ambao hatutapata nafasi za kuwa mbunge tutumie uwezo na mbinu zetu kusaidia katika maendeleo ya lile jimbo...

PAMOJA TUNAWEZA...
 
Last edited by a moderator:
“Naelekea Bungeni”

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata

Nakupongeza kwa uamuzi huo, Naomba utujuze uzoefu wako nje ya masomo. Umefanya kazi wapi na wapi? unafanya kazi gani halali wakati huu ya kukuingizia kipato?
 
Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata[/QUOTE
ukweli Hapo ndipo tulitaka useme umesema kweli tumelewa
 
Ben ukipitishwa tu...mchango wangu mdogo sana Laki tano uweke hela ya mafuta ya gari....Nitatoa muda wangu pia
 
Kwa kweli nimelisoma hilo andiko, nikaridhika nalo, na limejitosheleza. Kwa hakika umeonyesha kiwango ulichonacho cha uelewa. Mpangilio wa maneno na uwezo wa kujenga hoja sina mashaka nayo. Kwa kweli umetulia. Yatosha kusema, tukisubiri chama kipitishe maamuzi yake kwa kufuata kanuni na taratibu za kisheria. Big up Ben.
 
Here comes The real rebel Ben, hili ndo bunge tunataka sio vibaraka wakutuletea unending dramas like Swiss money
 
Pasco,

Asante sana na nakubaliana na mengi kati ya uliyoeleza hapa.

1: Halima Mdee bado ni mbunge mchapakazi.Hakuna asiyejua hili

2:Kiongozi ni lazima ajipime yeye kwanza na kuona kama anauweza uongozi badala ya kusubiri au kuandaa watu wa kumshawishi/kumlazimisha wakati yeye anajiona hana uwezo au hataki

3:Bado Sijataja Jimbo kaka

4: Ikitokea tofauti kwa kuwa mimi ni muumini wa demokrasia ya kweli katika uwakilishi wa watu nitachukua hatua za kidemokrasia

Ben huyu Pasco ni duplicity ni busara kum-ignore
 
Last edited by a moderator:
Ben ni kiboko aisee....!

Kuna watu walikua wakituma sms kwa viongozi wa wilaya huku Rombo tangu juzi wakiongozwa na Mbunge kuwa unahamia ACT waliposikia tu utatangaza maamuzi ndani ya masaa 72 .hapa umewachapa kisawasawa watu wamepoteana kabisa .naona Rombo ikimpata mbunge makini kabisa na kurudisha heshima.viongozi wa wilaya tuko na wewe kamanda
 
Upande huu kuna Ben Saanane Fraterin Masika Joseph Selasini Upande ule kuna Evodi Mmanda Notbruga Masikini Utouh... Rombo patakuwa patamu sana mwaka huu... I wish nipte fursa ya kwenda kushuhudia mtanange.. All in all nawatakia makamanda wote wa CDM kila la heri. Ni matumaini yangu waomba nafasi na chama kitaheshimu chaguo la wananchi. Nitasikitika sana nikisikia kuna yeyote kati ya wanaoomba nafasi atakayekimbilia chama kingine kwa sababu tu hakupata nafasi kupitia CHADEMA. Ni matumaini yangu pia kuwa chama kitapitisha jina la mgombea aliyepita kwa kura nyingi za maoni... Kinachonipa moyo ni kuwa hadi sasa wote mlioonyesha nia kugombea kupitia CDM mpo vizuri kiuchapa kazi... Kwa kuwa jimbo litakuwa na mbunge mmoja, nashauri wale ambao hatutapata nafasi za kuwa mbunge tutumie uwezo na mbinu zetu kusaidia katika maendeleo ya lile jimbo... PAMOJA TUNAWEZA...
Selasin Nae mpaka abanwe ndipo afunguke,itamcost sana.
 
Last edited by a moderator:
Hujataja Jimbo mkuu au macho yangu?

But all the best.. we must remain focused kama lengo ni kuwangoa hawa wezi
 
Back
Top Bottom