Nimefanyia kitendo hiki kwenye daladala

Nimefanyia kitendo hiki kwenye daladala

Hahahahhaa mtoa mada umenifurahisha sana looh
Huyo Konda nae alikuwa na lake jambo, we unamuoneshea kuwa akate mmoja kimya kimya yeye anajifanya haelewi ili utoe sauti. Hahahahaha.
Ila siku nyingine kuua soo na kutomfanya mdada ajisikie vibaya unamwambia konda ntakupa nauli yako hapa kwenye siti nimekaa vibaya a hahahahh ila husemi kama utamlipia dada au laah. Kisha saa ya kushuka unamwambia konda kata mmoja. Hahahahha

Au kuzuga ungejidau kumwambia bidada kwa lugha ya utani, daah nimekutana na wewe leo bora ntalipuwa nauli kisha unajikausha bosi ledi nilipie hehehehh
 
Ni swala la umasikini tu! Au ni kukosa ukarimu? Au ninini? What is 400 kwa mwanaume ambaye unaenda kutafauta unajua katika hii dunia unaweza ukaona umaefanya jaambo la kishujaa na wengine wanakupa hongera nyingi as if umefanya jambo la maana sana, kumbuka tunaishi kwa kutegemeana no matter unapesa au huna ipo sehem unaweza kukutana naye na ukiwa na shida ukakosa pa kuanzia pia 400 ! Kwa maisha haya is not a big deal.
Hiyo ni kwako
 
Hahahahhaa mtoa mada umenifurahisha sana looh
Huyo Konda nae alikuwa na lake jambo, we unamuoneshea kuwa akate mmoja kimya kimya yeye anajifanya haelewi ili utoe sauti. Hahahahaha.
Ila siku nyingine kuua soo na kutomfanya mdada ajisikie vibaya unamwambia konda ntakupa nauli yako hapa kwenye siti nimekaa vibaya a hahahahh ila husemi kama utamlipia dada au laah. Kisha saa ya kushuka unamwambia konda kata mmoja. Hahahahha

Au kuzuga ungejidau kumwambia bidada kwa lugha ya utani, daah nimekutana na wewe leo bora ntalipuwa nauli kisha unajikausha bosi ledi nilipie hehehehh
[emoji121]
 
Dah mwana wew ni kauzu zaidi ya dagaa yaan umemkazia demu wa watu bila hata aibu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu,

Hii ime_happen leo.

Kuna dada mmoja nilisoma na'e ngazi fulani ya elimu,
Tangu tumemaliza umepita muda mrefu hatukuwahi kuonana.

Sasa leo tumekutana kwenye daladala 1 la *t/segerea-simu2000*.

Ingawa hatukuzoeana sana kipindi tunasoma,
Leo huyu dada alionekana kufurahi sana kuniona.

Kwa kuwa tulikaa siti 1
Tukaanza kupiga stori kadhaa za kitambo,
Na kuulizana kuhusu wana wengine ambao tulisoma nao,

"Hivi _masalago_ yuko wapi?"

"Halafu nilidhani kuwa *seneta* umesharejea mtwara."

Na unajua kuwa yule _christopher maila_ wa kigoma anafanya kazi sehemu fulani?

Hivi yule _john nguchiro_ wa kuuza madesa yule huwa namwona fb sana,
Una mawasiliano na'e yule?"

"Ila _*seneta wa mtwiz*_ una mwili ya ajabu,
Yaani bado kamwili kembambaaaaaa!!!!
Hunenepi hata kidogo!!!"

Tukacheka kiutani
Na stori zingine kibao kama hizo.

Akashika simu yake
Akaniambia
"Halafu *seneta* naomba unipe namba zako za simu zote kabisa,
Ya airtel na ya tigo."

_____
Sasa ile naanza kumtajia
"0786 ........."
Kabla sijamalizia,
Kikafika kile kipengele cha *ndugu konda* kuhitaji nauli katika siti yetu.

Pamoja na kuwa miye nilikaa upande wa dirishani kabisa,
*konda* akanyoosha mkono hadi upande wangu kuhitaji hela ya nauli.
Nikajisachi mfukoni nikatoa 1,000/= nikampa konda
Halafu nikanyoosha kidole kimoja ([emoji121])
Kuashiria akate nauli ya mtu mmoja,
Kisha anirudishie 600/= yangu.

Yule konda akaniuliza kwa msisitizo,
"Blaza wangapi?"

Nikaonesha tena kwa kidole ([emoji121]).

Akaniuliza tena
"Au nikate ya wawili?"

Nikamkazia konda,
Nikamjibu,
"Wewe konda
Tuheshimiane!
Nimekwambia kata ya mtu mmoja,
Lete chenji hapa!
Eeeeeeeboh!!!!"

Watu wote wa jirani wakawa kimya wakitucheki kwa kuibia.

Konda akanipa tiketi na 6,00/= yangu,
Nikapokea,
Nikaweka mfukoni!
Nikatulia.

______
Yule dada akionekana kuwa na donge kali limemkaa rohoni,
Akafungua pochi yake,
Akatoa 400/= (ambayo ilikuwa ni sarafu 1 ya sh. 200,
Sarafu 1 ya sh. 100 na
Sarafu 2 za sh. 50) akampa konda,

Konda akapoke na akahamia siti ingine!
*******

Kukawa na kimya kama cha dakika 3 hivi kati yetu,
Zile stori za wana tuliosoma nao na kuniomba namba za simu zikapotea ghafla.

Hapo
Nikimcheki dada amekunja ndita ile mbaya,
Na mashavu yamevimba ghafla mithili ya kobe mwenye mimba!

Nikajifanya kumuuliza kwa upole,
"Hivi unayo namba ya simu ya *ching hyphen* wa _kimara bucha_ yule wa ps yule??"

Dada kimyaaaaa!!!!

******
Muda si mrefu basi likaingia stendi ya *mawasiliano*,
Baada ya kushuka nikamfuata ili tuagane au hata mawasiliano tupeane,

Nikamwambia
"Sasa ndugu naomba namba yako ya ..."

Kabla sijamalizia,
Alisonya kwa nguvu na kunifokea
"Ishia zako kuleee!!!
Tangu lini wamachame na wamakonde wamekuwa ndugu!!
Kwanza usiniharibie siku!!!"

Daaaaaaaaaaaaaaah!!!!

Nikashangaa sana,
Na kila aliye karibu aligeuka kuangalia!

*****
Sasa sijajua nilichomkosea huyu dada nini,
Wakati kabla ya konda kutembelea siti yetu
Tulikuwa na furaha yenye bashasha tele na amani sana!

Hujui kutunga story hata haueleweki
 
Upo sahihi kabisa,,tena yeye ndo ungemsakizia kuwa analipa ya wawili,,hawa viumbee mi sibembelezii kabisaa
 
Back
Top Bottom