Aslm'Alykm,
Nachukuwa nafasi hii, kuwapa ahsante na shukrani za dhati mimi na familia yangu, kwa faraja na rambi rambi zenu kwangu... Mtanisamehe kwa kuchelewa kutoa ahsante hizi hii ni kutokana na nilivyo azimia kwanza nifike Dar Es Salaam na kuona Kaburi alilo zikwa Baba yangu, kisha ndio niingie hapa JF kuja kuwapa shukrani zangu kwenu. Kwa hakika nimefarijika sana sana baada ya kuona jinsi wanachama wa JF walivyo jitokeza hapa na wachache walio udhuria mazishi pale nyumbani Sinza, kwa kweli sina cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu ndiye atakaye walipa ila mimi naomba mpokee ahasante na shukrani zangu mimi na familia yangu... Kwa kweli faraja nilio ipata siwezi kuielezea kwa maneno na ikakamilika, naomba mtosheke tu kwa haya machache na tuendelee na mapenzi mlio nionyesha mimi baada ya kufiwa na Mzee wangu. Hali hii ya mapenzi isiishie kwangu tu bali iendelee kwa kila mwanachama bila ubaguzi wa aina yoyote ile. Mweneyezi Mungu Insha'Alla atawalipa yalio mazuri sana mimi na nyinyi pia.
Shukrani
X- Paster