Nimefiwa na BABA Yangu Mzazi

Nimefiwa na BABA Yangu Mzazi

X-Paster

Pole sana, kwa kweli ni majonzi kumpoteza mzazi, ila nikufariji kwa ukweli kuwa wewe pamoja nasi tulimpenda ila Mungu amempenda zaidi


Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la bwana libarikiwe

Amina
 
Japo tumechelewa...Pole brother kwa msiba...sisi wote wa M/Mungu na kwake tutarejea...."Allahuma ghfirlau warhamhu waskinhu fil jannah...Allahummwa Fakakallahu minal nnar..wamin adhab kabri wamin adhabi yaumil Kiyama..."
 
Aslm'Alykm,

Nachukuwa nafasi hii, kuwapa ahsante na shukrani za dhati mimi na familia yangu, kwa faraja na rambi rambi zenu kwangu... Mtanisamehe kwa kuchelewa kutoa ahsante hizi hii ni kutokana na nilivyo azimia kwanza nifike Dar Es Salaam na kuona Kaburi alilo zikwa Baba yangu, kisha ndio niingie hapa JF kuja kuwapa shukrani zangu kwenu. Kwa hakika nimefarijika sana sana baada ya kuona jinsi wanachama wa JF walivyo jitokeza hapa na wachache walio udhuria mazishi pale nyumbani Sinza, kwa kweli sina cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu ndiye atakaye walipa ila mimi naomba mpokee ahasante na shukrani zangu mimi na familia yangu... Kwa kweli faraja nilio ipata siwezi kuielezea kwa maneno na ikakamilika, naomba mtosheke tu kwa haya machache na tuendelee na mapenzi mlio nionyesha mimi baada ya kufiwa na Mzee wangu. Hali hii ya mapenzi isiishie kwangu tu bali iendelee kwa kila mwanachama bila ubaguzi wa aina yoyote ile. Mweneyezi Mungu Insha'Alla atawalipa yalio mazuri sana mimi na nyinyi pia.

Shukrani

X- Paster
 
Pole sana mkubwa.... Allah Amempenda Zaidi....!
 
Pole sana ndugu yangu, tupo pamoja. Inna lillah wa ina illahi rajiuun
 
Pole sana mkuu nilikuwa sijaiona post hii. Mungu akutie faraja katika wakati huu mgumu.
Michango ya ubani twafikishaje?
 
Pole sana kwa msiba mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Pole sana mkuu nilikuwa sijaiona post hii. Mungu akutie faraja katika wakati huu mgumu.
Michango ya ubani twafikishaje?
Nashukuru ndugu, ila tushazika na msiba tulisha maliza tunacho subiri ni arubaini tu... ndio nami nipo Dar kwa muda ili kufanikisha mambo kidogo.
 
pole sana mkuu japo nimechelewa. namshukuru Mungu kwa kukupa subira ulipokuwa katika wakati mgumu.
 
Pole sana ndugu japo nimechelewa kutoa pole
 
Pole sana mpiganaji. Sikuiona post hii kabisa. Mungu awatie nguvu. Roho ya marehemu ilishalala mahali pema peponi.
 
Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Rajiuun.Tunamwombea marejeo mema kwa Mola wake.
 
Poke pole mkuu, MshukuruMuumba kwa kuwajalia kuwa naye muda wote huu.
Kila la heri.
 
Back
Top Bottom