Nimefiwa na Mama Mzazi

Nimefiwa na Mama Mzazi

Duh! Hii nilikuwa sijaiona...........Pole sana mkuu, Mwenye Enzi Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mama yako mzazi........
Tupo Pamoja Mkuu.
 
X-PASTER
pole sana mkuu..hiyo ni safari ya kila nafsi.RIP mama
 
Pole sana mkuu X-Paster, nakuombea wewe na familia yako faraja wakati huu wa msiba mzito wa familia. Mungu mwenyewe awasimamie na kuwainua.
 
Yakhe hii habari nzito kwelikweli!
Pole sana mkuu! Kazi ya Mungu haina makosa.
Hakika kwake tulitoka na kwake siku moja tutarejea.
Bwana Alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Poleni sana.
 
[FONT=century
gothic]Assalamu
Alaikum
[/FONT]


Admins, Moderators na
members wote wa Jamiiforums


Kwa masikitiko makubwa
nawataarifu msiba wa Mama yangu Mzazi, amefariki usiku wa kuamkia leo,
na Insha'Allah maziko yatafanyika leo jioni.

___
“Ewe Mwenyezi Mungu
msamehe Mama yangu na ipandishe daraja yake katika walioongoka, na weka
badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa
viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza
ndani yake”
[FONT=century
gothic]
[/FONT]

“Sisi ni wa Allaah
nasi Kwake tutarejea, Ee Allaah Utulipe wafiwa kwa msiba huu na utupe
badili yake bora kuliko huo na utukutanishe tena peponi
Insha'Allah”
Innalillah wainna ilayhi raajiun.
 
Pole sana x-paster mungu akupe moyo wenye uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu yote mapenzi ya mungu apumzike kwa aman.
 
"Sisi ni wa Allaah nasi Kwake tutarejea, Ee Allaah Utulipe wafiwa kwa msiba huu na utupe badili yake bora kuliko huo na utukutanishe tena peponi Insha'Allah"
"Inna lillahi wa inna ilayhi raaji'un"
Pole sana Mkuu. Mwenyezi Mungu awape subira kwa msiba huu na amjaalie mzazi wetu na wote waliotutangulia malzi mema peponi - Amin!
 
Back
Top Bottom