Nimefiwa na Mama yangu usiku wa kuamkia 19.11.2011 na kuzika jana.

Nimefiwa na Mama yangu usiku wa kuamkia 19.11.2011 na kuzika jana.

Pole sana Uporoto01, Mungu akupeni faraja zake katika wakati huu mgumu, Rest In Peace Mama..
 
Pole sana Mkuu, cha muhimu ni kuzidi kumuombea kwa Mungu apumzike kwa Amani, AMEN
 
Inna li Llahi wa Inna Illahi Rajiun.

Poleni sana wafiwa na Mwenyeezi Mungu awape wepesi wa kuhimili kuondokewa na mzazi.
 
Pole sana mkuu,sisi sote tunafuata njia hiyohiyo, mungu alitoa na mungu alitwaa, jina la bwana lihimidiwe! Amen.
 
Wakuu naishi Upanga mtaa wa Mindu plot 480 kutakuwa na lunch Jumatatu saa saba na nusu(siku ya tatu)wote mnakaribishwa sana.

Dunia ni ndogo sana, nilikuwepo mazikoni jana, nilikuja kwa kutokea upande wa Mariam Zialor, uporoto kumbe ni mtu wangu wa Karibu sana. Tuko pamoja.
 
Ni pigo lisilo na mfano, lisiloweza kuelezeka kwa urahisi, lakini Mungu atakupa nguvu ya kukabiliana na majaribu hayo makubwa katika maisha. mama apumzishwe mahali pema, Amina
 
Pole sana Ndugu yetu Uporoto!
Mwenyezi Mungu akupe nguvu wa kustahamili msiba huu mkubwa kwako na familia yako!
Sote hiyo ni njia yetu.Yeye katangulia sisi tutafuafa wakati ukifika.
 
Pole sana Uporoto ..
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mama...
Those we love don't go away , they walk beside us everyday .


.....................................
 
Back
Top Bottom