Nimefuatilia Soka Tanzania tangu 1980s sijaona kama Chama

Nimefuatilia Soka Tanzania tangu 1980s sijaona kama Chama

Hiv hawa sindio walikubutua hapa kwamkapa au?
uyo haelewi uwe unamfundisha kwa mifano.👇
images.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: K11
Siku hizi sio mpenzi sana wa soka Tanzania. Niliwafahamu kwa kusikiliza RTD, kusoma magazeti ya Uhuru/Mzalendo, na Mfanyakazi la mwandishi James Nhende aliyepigwa na Zamoyoni Mogella kwa madai ya kumuandika vibaya.

Walikuwepo viungo wa maana kama Charles Boniface Mkwasa (Master), Nico Njohole (Mapafu ya Mbwa), Hussein Ngulungu, Said Mwamba (Kizota), Ramadhan Lenny, Athumani China, nk.

Kutoka enzi za hao niliowataja hapa, sijawahi kuona kiungo mwenye akili kama Clatous Chota Chama (Mwamba wa Lusaka). Goli alilofunga leo dhidi ya Vipers, ni yeye pekee katika Tanzania anayeweza kufunga katika mazingira ya namna ile, wengine wangekuwa na papara ya kupiga ama cross au shuti kali kipa apambane nalo, lkn Chama akatulia na kumgeuza beki wa Vipers na kisha kumuangalia kipa na kumfunga kirahisi.

Chama ana akili sana ya mpira, tatizo lake [weakness] ni kutokuwa na haraka, yawezekana pia hawezi kucheza kwa haraka na makocha wengine hawawezi kuvumilia hilo, lakini hiyo kwa kuwa matokeo yake ni chanya inabidi tu makocha hata wasiopenda kasi yake wamkubali tu hivyohivyo. Kwa upande wangutangu nianze kufuatilia soka letu, sijaona kama Chama.

Vv
Majina tu uliowataja kama viungo wewe hujui Mpira wa Tanzania, usivamie historia ya mpira wetu
 
Walikuwa wanaomba mpira uishe licha ya kukutana na timu yenye safu butu ya ushambuliaji, wameshikilia bomba kwa maombi ya kila namna, lakini sio kila mechi watakutana na vipers na hapo ndipo pumba na mchele zitapojitenga
Hamjuagi mpira japo mnaupenda, mpira ni vita lila mtu anapambana.Juzi kati alipopigwa tatu raja mkachoonga, mtu mzimammoja ulaya huko kala saba, mwingine kafa sita.mchezaji anawezs timu hii akafanya vizuri pengne akashidwa.WANAKUJA WATU WANAKWAMBIA TENA KWA NAFSI YAKE HAJAONA OOH BERKANE.kwani chama kazaliwa simba?
 
Reject ya Berkene ni mfalme wa Simba. Mmecheza na timu ambayo ndani ya game 7 hawajaweza kufunga goli lolote. Timu pale hakuna.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Wakati mwingine muwe mnaweka ushabiki pembeni na ku-judge mambo kwa uhalisia. Kwani Chama amewafunga Vipers tu kwenye CAFCL tangu aje Simba? Vipi Nkana Red Devils na wengine (aliowafunga misimu kadhaa nyuma) nao walikuwa vibonde? Yale magoli yake ya visigino, ambayo Aziz hajayafunga hapa nchini hujawahi kuyaona?
 
Kesho nasikia kuna timu ya wanawake, inacheza siku ya wanawake duniani....
 
Back
Top Bottom