Nimefuatilia Soka Tanzania tangu 1980s sijaona kama Chama

Nimefuatilia Soka Tanzania tangu 1980s sijaona kama Chama

Chama ni dribbler mzuri, ana vision safi, awareness imekaa vizuri, stamina ipo njema lakini.. anticipation na speed yake ni poor. Shooting zake nyingi pia ni weak (Hana uwezo mzuri sana wa kufungia nje ya 18); hii inapelekea yeye kuforce kupiga pasi hadi sehemu zinazofaa ku shoot kitu ambacho mara nyingi huwa hakileti matokeo chanya (Rejea match ya vipers iliyopita na ile ya horoya).

Kwa maana hiyo timu ikizidiwa, uwezo wake pekee hautoshi kuokoa timu (rejea mechi ambazo Simba ameshikwa kama ya raja pale kwa mkapa). Kwaiyo huwezi kumuweka chama kwenye category ya mchezaji tegemezi kwenye mashindano yenye timu nzuri kama/zaidi ya Simba.

Najua umemsifia sana kwa sababu jana alimchenga beki na kumpiga tobo kipa. Lakini unasahau mtu huyo huyo alimpiga chenga kipa akajiingiza kwenye jopo la mabeki mpaka akashindwa kujua afanye nini na kuishia kupoteza mpira kizembe sana wakati kulikua na kina moses nyuma waliopo kwenye position nzuri zaidi (hii ndio poor anticipation nayoizungumzia).

Ni mchezaji mzuri, ana vitu fulani ambavyo wengi hawana. Ila kusema ni the best ever? Think again.
 
Dua Said na Said Sued Scad ni wachezaji wa matukio hawakuwa na maajabu. Chama ni mchezaji wa kawaida sana hauwezi kumfananisha na wanaume mfano Dani Muhoja ama Michael Paul Mkopo ama Nylon. Huyu Chama zama za akina Method Mogela angekuwa anabeba jezi tu. Utamfananisha na OCD huyu
Bwana Bwana huyu mleta mada ni ushabiki tu
 
Mm sio mzur sana kwenye uchambuzi wa mpira ila Huwa najiuliza kwann Chama asiwe anacheza kama kiungo mchezeshaji pale kati? Maana jamaa ana utulivu, Hana papara, ana hold vizur mipira, anapiga pasi za uhakika, anaweza kupunguza hata wa3 bila wasiwasi wowote
 
Washabiki wa Simba asilimia kubwa ni wajinga sana na malimbukeni, hii michuano kilicho muhimu ni point 3 hayo ya mpira mzur hayana nafas,
 
Mwenye matokeo ya Yanga vs Viper kwenye mwananchi day atuwekee hapa.
 
Back
Top Bottom