Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Aisee tena ukavibebe bila chombo ufungiwe kwny gazeti la udaku na unavyopenda udaku , ukinogewa na habari za udaku si vitamwagika.

Bado tena uanze kusubiri shilingi Mia hapana kwa kweli huku ushike vitumbua mara chenchi na umevaa mwachoma kumoyo mwishowe ujikwae bure ufe na kazi ukosee kiatu kichafuke, suruali pamoja na shati la kung'aa .
Kifupi umeupiga mwingi asikusumbue utapiga hata umachinga
 
Hahaa pole sana sasa kajiajiri mbele ya ofisi ya boss kuchoma vitumbua hahaaa,alafu kila asubuh unaingia kuchukua oda kwa boss. inaonyesha ofisi yenu ni ya kimaskini ivi hata mshahara ulikua unafika 200k kweli. Au alikutafutia sababu tu haiwezekani mpo posta uambiwe kalete vitumbua vya mia tisa . Ungemwambia boss acha ujinga vitumbua jero jero. Au kama ungetaka kumkomoa ungeenda uko unamaliza lisaa lixima
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri kama kazi inavyotaka

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana kwasababu sio majukumu yangu na ni kama dharau kwangu,

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli? nakusudia kwenda kwenye vyombo vya sheria
😂😂😂😂
Ila watu
 
Haya ndio nisiyoyapenda kwenye kuajiriwa yaani kuwa chini ya kima fulani.
Mimi hiyo kwangu ni dharau kubwa sana na lazima ningekupiga kichwa hata kama najua nitakosa hela ya kula.

Ni bora ufanye kazi kwa ajili yako mwenyewe au wewe ndio uwe boss.
 
Back
Top Bottom