Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nilionya Mapema kwamba ni vema hawa wanaoropoka na kutukana Wagombea wengine, Waitwe, Waonywe na wasamehewe.
Lengo la ombi langu hilo ilikuwa kuepusha mkanganyiko na kudumisha Umoja na Mshikamano, Kwa sababu Kuna maisha baada ya Uchaguzi .
Kwa Bahati Mbaya Ofisi ya Katibu Mkuu ilinipuuza na kuwaachia watu wateme nyongo zao, Imekuja kustuka ikiwa muda ushapita, na kiukweli pande zote zinakashifiana, Lissu anapiga Spana kwa kusaidiwa na wanaomuunga mkono, na huku Wapambe wa Mbowe nao wakipiga spana upande wa pili, hakuna penye afadhali.
Siku zote Minyukano kwenye Chama kilicho hai ni ishara ya kukomaa kwa Demokrasia ndani ya Chama hicho, Lakini kushambuliana kwa kuvuka mistari ya Katiba ya Chama huo ni Uhuni na hatutakubali, Chadema siyo genge la Wavuta bangi.
Naunga Mkono Kuondolewa kwa Ntobi kwenye uongozi kwa kukiuka maadili ya Chama, kama Alijivunia Cheo chake mbona Wenyeviti wengine wa mikoa hawatukani, kwani wao hawahusiki na Uchaguzi huu au wao ni Wajinga?
Sasa maadam tumeamua kuadhibu Watovu wa nidhamu basi tusiishie kwa Ntobi pekee, tushughulikie na wengine wote wanaofahamika, Orodha yao ipo wazi kabisa na mimi ninayo.
Kikubwa ni kwamba Watakaposhughulikiwa tusianze kulialia na kuleta lawama, kama Katiba ya Chadema ni moja basi panga lililotumika kufyeka Ntobi, Lifyeke na Watukanaji wengine.
Mungu Ibariki Chadema.